Ilani ya CCM 2005 iliyomuingiza JK; na ya 2010 iliyomrudisha tena - WaTZ ni Wepesi Kusahau? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya CCM 2005 iliyomuingiza JK; na ya 2010 iliyomrudisha tena - WaTZ ni Wepesi Kusahau?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 20, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  CCM iliwaambia Watanzania ukweli ufuatao kuhusu tatizo la nishati na Watanzania wakakubali na kumpatia mgombea wa CCM asilimia 80 ya Kura zao.

  Ulipofika Uchaguzi wa mwaka 2010 (miaka mitano baadaye) Chama cha Mapinduzi kijajivunia "mafanikio makubwa" katika sekta ya nishati. Katika Ilani yake ya 2010-2015 CCM kikatutangazia mafanikio hayo:

  Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi imeshughulikia maendeleo ya sekta ya nishati na kupata mafanikio makubwa yakiwemo yafuatayo:-
  (a) Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Songo Songo na kuanza kutumia gesi asilia katika kuzalisha umeme.
  (b) Mikoa ya Mtwara na Lindi kupata umeme wa uhakika unaozalishwa kwa gesi asilia ya Mnazi Bay.
  (c) Kuongezeka kwa uzalishaji umeme nchini kutoka kwenye miradi ya Kihansi MW 180, Songas MW 180, Ubungo MW 100 na Tegeta MW45.
  (d) Kukamilika kwa miradi ya upelekaji umeme katika Makao Makuu ya Wilaya za Serengeti, Ludewa, Mbinga, Simanjiro, Kilolo, Bahi na Mkinga.
  (e) Kukamilika kwa Sheria ya Nishati Vijijini na kuanzishwa kwa Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini.
  (f) Kuweka mfumo wa mikopo ya muda mrefu kwa waendelezaji wadogo wa nishati vijijini.

  Utaona kuwa hawakesema lolote walilofanya kuhusu Stielgers Gorge kama walivyoahidi miaka mitano nyuma.

  Hata hivyo, chama kile kile, chenye watu wale wale, kikaja na mapendekezo mapya ya nini cha kufanya kwa miaka mitano ijayo. Ahadi ambazo ziliweza kuirudisha CCM Bungeni japo si kwa kishindo. Ni kana kwamba Watanzania walianza kuelewa kuwa CCM inahusiana na matatizo yao na hivyo kuanza kuikataa. Kutoka asilimia 80 mgombea wao akapata asilimia 61 ya kura zote; kwa mara ya kwanza CCM ikapata anguka ambalo haijawahi kupata tangu kuuasisiwa kwake enzi za TANU. Ikapoteza viti vingi zaidi, ikapoteza halmashauri nyingi na sera zake zikakataliwa kutoka pwani ya Bahari ya Hindi hadi kwenye kingo za Ziwa Tanganyika; kutoka kwenye miguu ya Mlima Kilimanjaro, hadi kwenye maji yameremetayo kama fedha ya Ziwa Tanganyika; na kutoka kwenye ardhi ya udongo mwekundu ya Kusini mwa Tanzania hadi kwenye vilima vya Mawe vya Ukanda wa Ziwa Viktoria CCM ilikataliwa.

  Lakini wapo waliowakubali; kwa sababu waliahidi mambo yafuatayo kwenye Ilani yao:

  Mradi wa Ruhudji peke yake ulikuwa umekadiriwa kugharimu karibu dola milioni 800 hivi na kukamilika ndani ya miaka mitatu. Hii ilikuwa mwaka 2007.

  Ukiangalia ahadi zote hizo unalazimika kujiuliza tatizo liko wapi? Hivi ni kweli hawajui vyanzo mbalimbali vya umeme nchini? Ni kweli kwamba wanatakiwa kuambiwa au kushauriwa kuhusu njia tofauti? Je lengo la kuongeza MW 671 katika miaka mitano ijayo itaondoa tatizo la nishati ya umeme na linaendana au linaproject kuendana na ongezeko la watu na uzalishaji?

  Kwanini CCM na viongozi wake wasiliombe radhi taifa kwa hali iliyopo sasa na kukubali kuwa wao ndio waliosababisha hali hii? Kwanini, wapinzani hawataki kuwaambia CCM wakubali kuwajibika kwa tatizo hili?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,904
  Trophy Points: 280
  ngoia tunywe supu tuliyoipika wenyewe
   
Loading...