Ilani: Mwisho wa kichwa ngumu ni mbaya sana.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani: Mwisho wa kichwa ngumu ni mbaya sana.!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchemsho, Oct 20, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wasalaam, Sasa imethibitika wazi kwa dunia nzima kuwa watawala wababe na vichwa ngumu ambao wamekuwa wakifikiri kuwa nguvu ya risasi na mabomu vitawatisha wananchi wenye kiu ya mabadiliko na haki haifai tena.! Kanali muamari Ghadafi mtawala Jeuri, Mbabe na katili asiye na chembe ya huruma kwa wale aliokuwa akitofautiana nao bado alijiaminisha kwamba angaliweza kuishinda nguvu ya umma wa Walibya aliowakandamiza na kuwadhurumu haki na uhuru wao kwa miaka 42, baada ya walibya wenyewe kumchoka Gaddafi na kuamua kujitolea maisha yao na kumpinga kwa maandano yaliyodumu miezi takribani minane imethibitisha kuwa KAMWE NGUVU YA UMMA HAIKOMESHWI KWA MARISASI. Hatimaye Gadafi ambaye mwanzoni mwa maandamano aliombwa aachie madaraka na kupisha utawala wa kidemokrasia, lakini kwa kiburi na kejeli aliwabeza na kuwashambulia kwa vifaru na bunduki wananchi wake mwenyewe anaowaongoza, hilo tu lilimuondolea uhalali wa kuwaongoza walibya kamwe hakuna mtu atakayejiita kiongozi ambaye wananchi wake wakidai mabadiliko badala ya kujadili wafikie vipi mabadiliko hayo yeye anawamiminia risasi, Hakujifunza kutoka Misri wala Algeria kutii matakwa ya wenye nchi, mwenyewe alidhani Libya ni Mali yake na Familia yake, Sasa angalia mwisho wake umevyokuwa mbaya, familia yake imeteketea karibu yote, mwili wake umeburuzwa barabarani AMEKUFA KIFO CHA AIBU. Ni bahati mbaya sana kwamba viongozi wengi wa afrika wana jeuri kama ya gadafi wasiowepesi kukubali mabadiliko hata kama hayaepukiki.! Wanajifanya Miungu watu walio juu ya kila sheria na Amri, WITO WANGU: viongozi wa afrika chukueni hilo somo kutoka Libya na mkubali kuwa nchi ni mali ya wananchi wenyewe, wao ndio katiba na kila sheria, Rule Of The People. Tusubiri tuone baada ya Libya Nchi gani itaamka tena na kuendeleza haya Mageuzi mapya ya siasa za Afrika..Naomba kuwasilisha.
   
Loading...