Ilala: DC Sophia Mjema athibitisha wagonjwa wa COVID-19 hospitali ya Amana kuleta fujo na kutaka kuondoka wakajitibie nyumbani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,459
2,000
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema athibitisha wagonjwa kulazimisha kuondoka katika Hospitali ya Amana kurejea nyumbani.

Pia soma > Wagonjwa wa Corona wadaiwa kuvunja geti hospitali ya Amana na kutoroka. Mwananyamala waleta vurugu wakitaka waruhusiwe


---------

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Simba amesema kuwa kulikuwa na wagonjwa ambao walikuwa hawataki kuendelea kukaa hospitali kwa kuwa walikuwa wanajihisi hawaumwi sana.

Hivyo akasema ikumbukwe kuwa mtu akifika hospitali kwa kuhisiwa kuwa na maambukizi ni lazima akae aangaliwe kwanza ndipo aruhusiwe lakini wao walikuwa hawataki bali walikuwa wanataka kurudi nyumbani.

Akasema pia hana hakika kama kweli kuna vurugu zilizotekea isipokuwa wagonjwa walikuwa wanapiga kelele wanataka kurudi nyumbani.

Pia akasema hana hakika kama kweli kuna wagonjwa ambao wametoroka hivyo wanafuatilia swala hilo kwa walinzi wa hospitali ili kujua kama ni kweli wametoroka basi wafatilie ni wagonjwa wangapi na wawafatilie wapo wapi.

''Hili hatuna taarifa hiyo bado hivyo ngoja tulifatilie kwa upande wa wenzetu maaskari wanaolinda hapo na kama wametoroka watakuwa wameendea wapi maana kama mtu alikuwa amehisiwa na anajulikana alitokea wapi hivyo atakwenda kufatiliwa kwenye mtaa aliotekea na atapatikanaili asiweze kwenda kueneza magonjwa kwa watu wengine''

Kwa sasa hospitalini hapo hali ni shwari hakuna tatizo lolote hivyo watulie tu wafatilie taratibu za hospitali na wale ambao wataonekana hawana tatizo wataruhusiwa na kuondoka.

Anasema kuwa watu wana hofu hivyo mtu akijiona hana dalili za ugonjwa kama mafua, kukohoa na kichwa kuuma ni kawaida kwa binadamu kutamani kuondoka, lakini kama alichukuliwa kwa kuwa na viashiria basi ni vyema wakatulia hospitali mpaka taratibu rasmi.

Na wale walio na viashiria hata wakirudi mtaani nako huko watu watawakimbia watawaambia warudi kwanza hospitali wapone ndipo warudi hospitali.

Na pia Amesema wananchi watulie wasikilize serikali inawaambia nini maana kama mgonjwa amepelekwa hospitali kwa kuwa na viashiria vya ugonjwa basi ni bora akatulia asubirie taratibu za hospitali, maana unaweza kaa siku mbili ukijiona kuwa u mzima na na baada ya siku mbili ukawa mgonjwa, hivyo ni bora kusubiri uruhusiwe kwa taratibu zilizowekwa maana hospitali sio jela bali ni kwa aliji ya kuangalia afya.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,528
2,000
Nilisema Jiwe ameshaamua Nature to take its course, Darwins natural selection theory to take its course.... survival for the fittest! Atakayejenga immunity akaponyoka kifo, basi anabaki namtawala huyo huyo! Next pahse ni maiti kutupwa barabarani!
 

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,459
2,000
#BreakingNews:Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi.Sophia Mjema athibitisha wagonjwa kulazimisha kuondoka katika Hospitali ya Amana kurejea nyumbani.

ITV habari
2377028_Screenshot_20200423-111857-1.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom