Ila wabongo wabishi aisee, tozo na mfumuko wote huu wa bei bado sikukuu zimefana kama kawa!!!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Nazungumzia sikukuu zote za hivi karibuni; x-mas, mwaka na hii eid el fitr ya leo. Yaani...
-majumbani mapilau yametawala
-watoto wamewaka kwa mavazi mapya
-kuna maeneo bidhaa kama viazi mpaka vilikwisha kwa jinsi vilivyonunuliwa kwa wingi.
-wanawake walivaa
-shows za wanamuziki kama zote
-kumbi za starehe watu wamejaa mpaka wamepwakuka.

Aisee wabongo wabishi!!!
 
Sina hakika kama ni kweli, kijjjini kwetu hakuna aliyefuturisha, mtandaoni sijaona wale wanaojikweza kufuturisha....na leo kijiji kipo kimyaaaa, hata mwaliko wa kinafiki tu haujapatikana!

Labda kama una ujamaa na kina waliokwapua!
 
Nazungumzia sikukuu zote za hivi karibuni; x-mas, mwaka na hii eid el fitr ya leo. Yaani...
-majumbani mapilau yametawala
-watoto wamewaka kwa mavazi mapya
-kuna maeneo bidhaa kama viazi mpaka vilikwisha kwa jinsi vilivyonunuliwa kwa wingi.
-wanawake walivaa
-shows za wanamuziki kama zote
-kumbi za starehe watu wamejaa mpaka wamepwakuka.

Aisee wabongo wabishi!!!
Mkuu miaka ya 2000-2006 ulikuwepo duniani??(samahani lakini) kama ungekuwepo hasa maeneo ya mijini ndipo ungejua kuwa kwa sasa watu hawasherekei bali,kuliwazana tu kwa matatizo!!ile ilikuwa kufuru,wanywaji wanatoka eneo fulani kwenda maeneo mengine kutafuta bia,baada ya eneo zima walilopo bar zote bia zimekwisha!!!watu wanashindana kupanga creti za bia kilingana na urefu wa mtu.
 
Uongo Mkuu
Mwaka 2021 Katika Eid mubarak nilpokea saani tano lakini leo nimepokea moja tu.
We umetoa ngapi mkuu katika kipindi hicho?!!!!

inawezekana tatizo lipo hapo, kuna upungufu wa kisocial😄😄😄
 
imeshindikana kabisa
Dah pole sana pia mungu akufanyie wepesi, nakumbuka hiyo situation kipindi naenda kununua maandazi 10 asubuhi wamama wananambia we kaka unakula jamani kumbe maskini mimi maandazi hayo nakula matatu matatu asubuhi, mchana na jioni mungu ni mwema sana nilipita salama kile kipindi sikukufuru
 
Amen, Mungu ni mwema
 
Back
Top Bottom