Uchaguzi 2020 Ila jamani sehemu alizopita Tundu Lissu ama kwa hakika CHADEMA ina makamanda, CCM sasa ijifunze kuishi na chama mbadala!

dikteta2020

JF-Expert Member
Aug 14, 2018
482
1,000
Aisee haya mambo eti ya nunua nunua kwanza yanaikuza bure Chadema, unajikuta umenunua garasa halafu linakuwa replaced na CHUMA!

Emb anzia Momba, Sumbawanga mjini, Mbeya mjini, Iringa mjini, Njombe mjini, Bikoba mjini, Mara yoteee, Nyamagana, Shinyanga, Arusha mjini, Karatu,Hai, Rombo, Handeni, Mlimba, Mikumi yani hadi unashindwa umtaje nani na nani umuache. Ni full makamanda

Ifikie tu hatua CCM ikubali kuwa sasa ina mshindani halali wa Jamhuri ya muungano na ijifunze namna ya kuishi naye. Tukubali tu kuwa zama za CCM ndiyo kila kitu zimepitwa na wakati! Chama tangia 2005 kinakuhenyesha na kila siku kinaongeza dozi mara dufu bado hukubali tu?

Yani haitokaa itokee tena kudhoofika Chadema! Huo ni ukweli na utabaki hivyo.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,136
2,000
Tangu mwaka 1992 ofisi ya chama ndio ile ya ufipa, sidhani kama CDM imeshafikia hadhi ya kuwa chama mbadala.

Bado ni chama chenye kumezwa na haiba za mtu mmoja mmoja kuliko kuwa ni taasisi yenye nguvu kuliko mtu.
 

MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,565
2,000
Tangu mwaka 1992 ofisi ya chama ndio ile ya ufipa, sidhani kama CDM imeshafikia hadhi ya kuwa chama mbadala.

Bado ni chama chenye kumezwa na haiba za mtu mmoja mmoja kuliko kuwa ni taasisi yenye nguvu kuliko mtu.
Ndio mfano halisi ya maendeleo ya watu badala ya vitu, wewe una nyumba nzuri halafu ndugu zako hohehahe inakufaa Nini?????
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,136
2,000
OFISI za CCM zilijengwa wakati wa chama kimoja. Na pia CCM mpya inafuata maono ya mtu mmoja(rejea hata kauli ya Polepole leo).
Mnatumia nguvu nyingi kuhalalisha udhaifu wenu kichama.

Magu ni muongoza njia tu ifikapo 2025 anamkabidhi uenyekiti mtu mwingine, CCM sio chama cha kisultani kama hicho cha Mbowe.
 

TheWiseMan

Member
Nov 17, 2017
36
125
Tangu mwaka 1992 ofisi ya chama ndio ile ya ufipa, sidhani kama CDM imeshafikia hadhi ya kuwa chama mbadala.

Bado ni chama chenye kumezwa na haiba za mtu mmoja mmoja kuliko kuwa ni taasisi yenye nguvu kuliko mtu.
Umejawa na ushabiki na huijui historia ya nchi vizuri. Wakati nchi inapata uhuru, TANU ilikuwa na ofisi..!?

Afu nani alikwambia ofisi ni ishara ya ukombozi au uongozi..!?

CCM yenye ofisi nzuri Hapa Dodoma, hiyo ofisi yao imesaidia nini kutatua tatzo la ajira kwa hii miaka mitano..!?

Hiyo ofisi na ofisi zote za CCM zimesaidia vipi kubadili mfumo wetu wa elimu uliopitwa na wakati..!?

Ofisi zenye malu malu na mataa ya kisasa za CCM zimesaidia vipi kuongeza mishahara na kupandisha watumishi madaraja..!?

Kwa taarifa yako, ofisi za CCM zimekuwa ni majengo ya kupangia mikakati ya kudhulumu na kupora rasilimali za nchi hii.

#elimika.
 

TheWiseMan

Member
Nov 17, 2017
36
125
Mnatumia nguvu nyingi kuhalalisha udhaifu wenu kichama.

Magu ni muongoza njia tu ifikapo 2025 anamkabidhi uenyekiti mtu mwingine, CCM sio chama cha kisultani kama hicho cha Mbowe.
Ona ulivo mjinga, mbona sheria zipo wazi kabisa, kama chadema kingekuwa cha kisultan unadhani msajili angekuwa amekiacha mpaka leo bila kukifuta..!?

Kuana kikundi dhaifu nchi hii kama CCM!? Katibu mkuu wenu kathibitisha mara nyingi jinsi mnavotegemea dola kubaki madarakani, utasema hicho ni chama kweli..!? Chama kinachotegemea dola..!?

Chama lazima kiwe na ushawishi kwa wananchi, CCM kama kikundi cha wahuni kimepoteza uwezo wa ushawishi.

Afu ulivokosa ufaham unashindwa tambua CCM imekufa, kwa aina ya viongozi wake ni wazi lazima watumie njama chafu, fikiria watu kama polepole, kibajaj, nape, Makonda, Kigwangala, Ndugai, Bashiru nk. Hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kujenga hoja na ushawishi wote ni empty kwenye ushawishi na mikakt ya hoja.

Ndiyo wamepata kuwepo, Nyerere, Mkapa, Sitta, Kikwete na baadhi, ila kwasasa CCM imebak na watu waliokosa weredi
 

TheWiseMan

Member
Nov 17, 2017
36
125
Mbowe anawapiga kisawasawa halafu anafurahia sana akili kama za kwako, zisizohoji masuala kwa kina.
Kuna mpigaji nchi hii zaidi ya Mwenyekiti wa CCM TAIFA?
Mwenye tuhuma za kupora nyumba za serikali, mwenye matamshi machafu kwa jamii.

Fikiria hii sentensi "pipo yuzidi tudai ini ze leki". Huyu alietoa hyo sentensi ndio Genius wa chama chenu, ambaye mnaona anafaa kuwaongoza milele mpaka wajukuu zenu wawe mababu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom