IKUNGI, Singida: Wafanyabiashara wa asali wapewa mwezi mmoja kuacha kutumia chupa za Konyagi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
ee084cb785c1f6f96fcb6b9cf2249a40.jpg
Wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikungi, mkoani Singida waliopo kando kando ya barabara kuu Singida - Dodoma, wamepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia sasa, kutumia vifungashio halisi badala ya chupa za Konyagi, ili kulinda afya za walaji
8c87776ce2e98ad8456fa2d3e650359c.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturi, ametoa agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa matumizi sahihi ya vifungashio vya asali, iliyofanyika katika kijiji cha Issuna tarafa Ikungi

Alisema ufungaishaji wa asali unaofanywa na wafanyabiashara wa asali katika wilaya ya Ikungi, sio wa kuridhisha na kwa namna moja au nyingine, unachangia kuharibika kwa asali

"Ufungaishaji unaofanywa na wafugaji wetu wa nyuki, unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa soko la asali. Wafanyabiashara hawa wanaouzia asali pembezoni mwa barabara, wanafungasha asali bila kuzingatia sheria na kanuni za biashara ya mazao ya nyuki hususani asali. Nawapeni mwezi mmoja mbadilike katika ufungaishaji", alisisitiza Mtaturi

Mkuu wa Wilaya hiyo, pia amewataka wauzie asali ndani ya jengo maalum la kuuzia mazao ya nyuki ambalo toka limalizike kujengwa mwaka 2013, hadi sasa halijawahi kutumiwa.
 
Back
Top Bottom