Ikungi, Singida: Gari la mbunge Lucy Magereri(CHADEMA) lapata ajali. Dereva apoteza maisha!

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Gari la mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro, amepoteza maisha papo hapo.

Katika gari la Mbunge alikuwepo dereva mwenye na alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar.

Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.

IMG_20180809_121959_557.jpg
 
Gari ya Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri namba T 348 CSR imepata ajali eneo Issuna wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida ambapo dereva amepoteza maisha hapo hapo,dereva aliyepoteza maisha anaitwa Thomas Maro.

B4CAD7B2-CAE9-49B8-A6DB-2FAC528B2436.png
 
Back
Top Bottom