Ikulu, Zanzibar: Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ni mzima wa afya

Walaaniwe wanaomchulia Mzee Mwinyi. Mwendazake alikuwa dikteta. Mzee Mwinyi hakuwa kuwa na chuki ya Mwendazake...
 
IKULU YATOA TAARIFA KUHUSU MZEE ALI HASSAN MWINYI

Idara ya Habari na Mawasiliano Ikulu inatoa taarifa ya kukanusha habari zisizokuwa rasmi zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Mzee Mwinyi yupo salama, mwenye afya na anaendelea na majukumu yake ya kila siku.

View attachment 1813862
Kwa nini taarifa hii inatolewa na ikulu ya zenji wakati mwinyi alikuwa ni rais wa Jamhuri?
 
Amekuwa jobless 😃
Ndo ubaya wa kupata cheo through political chances, religion, tribe and regionalism. Angekuwa Civil servant ange chance in kwenye former position nakuendelea kula mshahara japo sijui kama ungeshuka kutoka hiyo 8mil.
 
Mzenji huyo...

Amesema samia aangalie umakini aliokuwa nao magu (nadhani kuhusu uhuru wa (vyombo vya habari)) maana watu wanazusha sana mambo. Pia akasema wanampenda sana samia na japo kuna wanaokarahisha
Shukraan mkuu!
 
Kuna kitu hapo umekiweka kama mzaha ila mimi kilikuwa kinaniumiza akili tangu muda sana tangu samia ashikilie usukani

Maneno mengi tumetohoa kutoka kwenye kiarabu sasa vipi kwa neno rais samia tusiite raisat samia?
Lugha ndugu Hata Mimi, ni msemeno. Lakini wajua kwamba, baada ya Raisat kuapishwa naye akawaapisha VIONGOZI mbali mbali, ni sherehe kwao wateule; vile kuukwaa Uwaziri, ukuu wa wilaya, ukurugenzi n.k. Hawana muda hata wa kuangalia umuhimu wa Majina ya vyeo vyao na UKWELI wake.

1- NENO KIONGOZI:

Duniani na Mbinguni, kiongozi ni mmoja tu - MUNGU. Atakaye dai kuwa yeye ni kiongozi, hiyo ni batili. Ndiyo maana katika utawala wa Mungu hapa duniani, tuna -
1) baba katika familia,
2) babu katika ukoo
3) diwani katika kata,
4) mjumbe katika tarafa au jimbo,
5) waziri wa hazina,
6) waziri wa fedha, madini na gesi
7) waziri mkuu msaidizi wa Mfalme,
8) mfalme katika taifa.
Hakuna tena mlolongo wa bwana wakubwa wenye kupewa mishahara minono, alawansi kebe kebe, marupurupu lukuki. Bila kusahau viiinua mgongo. Lakini Leo duniani, mfumo huu umepinduliwa - baba katika familia na babu katika ukoo, imekuwa ziii!

Kwa hiyo jambo kuu na muhimu maishani mwa watu - ULEZI, umejengewa shule (neno lenye kutoholewa kutokana na lugha ya kijerumani SCHOL).

MALEZI:

Watu tuishi vipi kwenye mgongo huu wa ARDHI sambamba na matakwa ya Muumbaji (dini), imekuwa ni suala LA mtu binafsi. Kwa hiyo, malezi yamekuwa ni kujifunza kusoma, kuandika na Kuhisabu.Kinachofuata hapo ni kusomeshwa masomo lukuki, ambayo mwishilio wake ni kupewa cheti cha kuhitimu KUAJIRIWA.

AJIRA:

Tunaajiriwa kukidhi utatu mtakatifu usiokuwa fumbo LA imani-
1. Serikali isiyo na dini,
2. Bunge la nchi lisilo na dini, na
3. Mahakama ya waingereza
Mihimili mitatu hii huwa kwa Wazungu ni MIRADI yao {baraza LA mawaziri likishaapishwa tu, wao huko ulaya hufungua madirisha ya bidhaa zao kungojea idara za manunuzi kutuma mahitajio ya maofisi yao. Hutupa msaada kwa ajili ya chaguzi zetu. Pesa hiyo huchangwa na wafanya biashara wa ulaya}. Na kwetu wachache tuliohitimu SHULE (0.000001% ya RAIA wote), ni AJIRA (Mji mkuu, Mji mkuu wa mkoa na wilaya):

AJIRA SERIKALINI-
1) Urais,
2) Uwaziri mkuu na Uwaziri mkubwa na mdogo ajira 60 na ushei
3) Uwaziri kurejelewa mikoani (mkuu a mkoa) na wilayani (mkuu wa wilaya),
4) Ukurugenzi wa mkoa. Wilaya na miji.
Vivyo hivyo, tunaweza kuandika juu ya mihimili hiyo mingine- kama vile BUNGE, MAHAKAMA; ndio uje mashule, mahosipitali, majeshi Tisa, n.k, n.k. Wazungu na hivi sasa Waasia nao, wana soko kwetu au LA? Sisi ni damping ground wa bidhaa za viwanda vyao. Haitoshi! Mali ghafi Hawana. Tunawauzia kwa bei wanayopanga wao.

2- MALKIA:

Ndugu Hata Mimi, neno Raisat katika lugha ndio hasa lingemfaa Samia. Lakini kwa sharia ya kimaumbile, Yeye Muumbaji wetu Mwenyezi Mungu, kaweka mkuu wa nchi awe ni MFALME. Ikiwa ni mwanamke, anakuwa ni MALKIA. Ndio maana ulaya Uingereza sana MALKIA, Ureno, Spain, Nchi tatu za Skandernavia, Denmark, Uswiz n.k sana Wafalme au MALKIA. Hizo zingine zenye marais cheo cha heshima.

Kwa vile watawala wetu kwenye nchi zetu hizi ghushi, ni uzao wa malezi ya USHULE, tunajua nini isipokuwa kile wakoloni walichotufundisha na kututayarishia?

USHULE ni kasumba. Wajiona na kujitambua kiutoto utoto tu. Hukai ukajiona umtawala ofisini mwako, bali waona ni AJIRA. Mwisho wa mwezi upokee mshahara, basi. Suala LA kujenga nchi halipo. Rais ni muajiriwa namba moja. Jiulize nani anayemuajiri?

Ndio MAANA Magufuli alijitambua kuwa yeye ni MFALME, kwa muda mfupi alitenda mengi na mazuri. Yale aliyokosea, tumkubali kuwa naye ni binadamu. Sote tuna mapungufu.

Kwa hiyo MALKIA Samia, kama hatajitambua hivyo akatenda, ole wetu. Na kama akijihesabu kuwa yeye ni Rais; chochote atakachotaka kufanya kiidhinishwe na MUHIMILI WA BUNGE, hizo ni nyayo za Kikwete na Mkapa. Mkapa aligundua kosa hilo na akalirekebisha kupitia MAGUFULI.

TAHADHARI:

Kosa kubwa tulilolifanya katika ufalme wa Magufuli ni kuwa -Mungu tulimsahau. HATUKUFANYA IBADA YA MUNGU Q22:34 ~nukuu "Na kila UMMA Tumewafanyia mahala {IKULU} pa kuchinjia mihanga ya IBADA ili kulitaja Jina LA Mwenyezi Mungu juu vile alivyoturuzuku katika wanyama hao wenye miguu minne. Basi (tukifanya hivyo), Kiongozi wetu ni Kiongozi mmoja tu {kwa kushika mihimili mitatu Mungu Anayoiridhia Q22:32 a) Mjumbe ajaye na
b) Katiba akaingia
c) ikulu iliyotakaswa Q57:25} (Eeenyi Waswahili) hapa Kwake huyo, ndipo tujisalimishe (tupaelekee kwa uongozi). Na wape habari njema sisi Wanyenyekevu (wana wa mama weusi -BLACK PEOPLE)".

3- Hii ni elimu ya KITABU. Shuleni na vyuoni haipo. Sasa! Mama Raisat Samia ATACHOMOKAJE?

4-Sijui kijana huyu mwana wa Mzee Ruhsa akiliona hili, si ataambiwa amekuwa jiwe. Kwa sababu yeye ni mteule wa chama cha kisiasa na sio mteule wa Mungu. Atahitaji umagufuli, naye ajaribu kwa akili hii kutoka MBINGUNI.

Kwa jina la Mola wa JMT, kazi iendelee Mwanzo wake na Mwisho wake,
MUNGU WETU ATULINDE, AMLINDE SAMIA NA HUSENI, kwa thubutu Q5:67

Mie si hayo tu mwanangu Hata Mimi, tuna shughuli kubwa, ili ni nyepesi kuliko maelezo kwa idhini ya MUUMBA wetu.
Kuna kitu hapo umekiweka kama mzaha ila mimi kilikuwa kinaniumiza akili tangu muda sana tangu samia ashikilie usukani

Maneno mengi tumetohoa kutoka kwenye kiarabu sasa vipi kwa neno rais samia tusiite raisat samia?
 
Back
Top Bottom