Ikulu yazuia mawaziri kwenda nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yazuia mawaziri kwenda nje ya nchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by shiumiti, May 21, 2010.

 1. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana jamii asubuhi hii wakati napitia magazeti, nimeona kichwa cha habari kikisema "kuelekea kampeni, Ikulu yazui mawaziri kwenda nje ya nchi...... Hii ikanishtua kidogo, nikasema ngoja niiweka hapa tuweze kujadili..... sijui hii mnaionaje majameni???????
   
 2. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nadhani wanatataka kuweka nguvu kwenye kampeni na kusaidiana wale ambao wana uhakika na majimbo yao wawasaidie wengine ambao wako kwenye hati hati kama kupokonywa. hizo ni kampeni za sisiem tu. Huo ni mwanzo wa michezo michafu.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa hapo tujadili nini na hicho ni kichwa cha habari tu, wewe huyajuhi magazeti ya kibongo?, kichwa cha habari kingine na habari yenyewe nyingine, lete habari kamili tujadili kwa kina
   
 4. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hizo fedha kwa ajili ya ziara hizo zilitengwa kwenye bajeti? Au ndio wanatafuta namna ya kumalizia fedha nyingi zilizotengwa kujinufaisha wenyewe badala ya maendeleo ya taifa. Kuna maana gani kufanya mikutano nchi nzima badala ya kujenga barabara, zahanati, masoko nk.

  Nchi hii imekuwa ikitenga fedha nyingi katika bajeti bila kuwa na evaluation ya bajeti husika. Inabidi wananchi tuombe mchanganuo wa matumizi ya kila wizara na idara za serikali. Kwani ni haki yetu sisi walipa kodi.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wasije wakajikuta wanazomewa tena kama kipindi kile! Hivi mafanikio si huwa yanaonekana kwa nini mpaka uwafungie safari wananchi kwenda kuwahubiria kuhusu ulivyoongeza shule, ulivyoboresha barabara zao as if hizo ni zawadi kumbe that is what you were voted for. Shame on you ikulu na muungwana wenu!!!!!!
   
 6. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari kamili hiyo hapo kaka

  YATOA WARAKA KUWAAGIZA WAZUNGUKE MIKOANI KUKUTANA NA WANANCHI
  KATIKA kile kinachoonekana ni kujipanga vema na kujihami kwa maswali magumu wakati wa kampeni za uchaguzi, Ikulu imetoa waraka wa kuzuia mawaziri kusafiri nje na badala yake kuwaagiza kuzunguka mikoani kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

  Ramadhan Semtawa
  Waraka huo, ambao umepewa jina la "Mlitutuma, Tumetekeleza, Tumerudi Kuwaelezeni Tulivyotekeleza na Kuwasikilizeni", pia unawaagiza mawaziri kukutana na watu wa aina mbalimbali kwenye ziara hizo, wakiwemo viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

  Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Ikulu kutoa maagizo kama hayo baada ya ziara ya kwanza iliyofanywa mwaka 2007 ya kutetea na kuelezea bajeti ya mwaka 2007/08, ambayo ilikuwa ya kwanza kwa serikali ya awamu ya nne, kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za walipakodi na kampeni za mawaziri kupata ujumbe kwenye halmashauri kuu ya CCM, chombo ambacho ni cha pili kimamlaka kwenye chama hicho kikongwe baada ya mkutano mkuu.
  Pia katika ziara hizo, mawaziri walijikuta wakiishia kufanya vikao vya ndani ya chama kutokana na wananchi kuwazomea kila walipotaka kufanya mikutano.
  "Huko nyuma, tumepata kuwaandalia Outreach Programmes angalau mara mbili. Zote mbili zilianza vizuri lakini zikaishia njiani kabla ya kumalizika," inasema sehemu ya waraka huo.

  "Ili kuhakikisha kila waziri anatekeleza wajibu wake katika hili, tunashauri ziara zote za mawaziri za nje ya nchi zisimamishwe hadi kila waziri atakapokuwa amefanya ziara yake."

  Waraka huo umetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa amewatangazia vijana, viongozi na wana CCM wote kujiandaa kujibu tuhuma za ufisadi ambazo zitaibuliwa na wapinzani kama silaha kwenye kampeni za uchaguzi wa Oktoba.
  Agizo hilo la Kikwete alilolitoa juzi mjini Iringa wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM), limedhihirishwa na waraka huo ambao umeambatana na ratiba ambayo inaonyesha ziara za mawaziri hao mikoani kueleza wananchi mafanikio ya serikali katika kutatua kile walichoituma.

  Katika waraka huo wa Mei 11, Ikulu imeelekeza na kutoa mapendekezo ya wadau husika ambao kila waziri atapaswa kukutana nao katika mikutano yake mikoani kwa mujibu wa ratiba.

  Waraka huo, ambao Mwananchi imeona nakala yake, umeelekeza kwamba katika mkutano wa kwanza waziri atapaswa kukutana na wafanyakazi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa CCM.

  Agizo hilo la waraka limetaja wadau wengine wakuu wanaopaswa kukutana na mawaziri kuwa ni pamoja na wajumbe wa nyumba kumi, wawakilishi wa sekta za wizara zilizopo mkoani humo, wawakilishi kutoka sekta ya biashara mkoani na wawakilishi wa sekta nyingine za uchumi.

  Sehemu ya waraka huo ambao unatokana na maamuzi kati ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu) na wasemaji wa wizara za serikali, imetoa pia ratiba ambayo kila waziri atapaswa kutembelea mkoa mmoja kwa tarehe maalum iliyopangwa.

  "Inapendekezwa katika programu hii kila waziri atembelee mkoa mmoja kwa tarehe zilizopangwa...," inaeleza sehemu ya waraka huo.

  Waraka huo umeelekeza madhumuni mawili ya ziara hizo ambayo ni pamoja na kila waziri kueleza mafanikio ya wizara yake katika miaka mitano ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne na kusikiliza kero na shida za wananchi katika maeneo wanayotembelea na kujibu hoja.

  Ikulu imeeleza katika waraka huo ikisema: "Kabla na baada ya ziara ya waziri, kila wizara itatakiwa kufanya mambo yafuatayo, kutengeneza vipindi maalumu viwili in the form of Documentaries (katika mfumo wa vipindi vya makala (redio na TV))."

  Kazi nyingine kwa mujibu wa waraka huo ni pamoja na "kuandaa tangazo fupi (public service announcement) kutangaza mafanikio ya wizara katika miaka hiyo mitano kwa ajili ya redio na televisheni na matangazo hayo yaanze kutumika mara moja".

  Pia wametakiwa "kuandaa retreat na wahariri wakuu na wahariri waandamizi wa vyombo vya habari nchini kwa nia ya kujenga uhusiano na vyombo hivyo na pia kuwaelezea wahariri hao mafanikio ya serikali ya awamu ya nne".
  "Kabla ya kuanza ziara, kila waziri aandae mkutano mkubwa wa waandishi wa habari kuelezea mafanikio na shabaha ya ziara yake," unaeleza waraka huo.

  "Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inapendekeza kuwa ofisi zote za wakuu wa mikoa zifuatilie ratiba hiyo ili kuandaa na kufanikisha mikutano hii na waziri husika.

  "Pia taarifa kwa vyombo vya habari iandaliwe kabla ya kuanza na ratiba nzima ya waziri na mkoa itolewe kwa wana habari."

  Ratiba ya ziara iyo inaonyesha, mawaziri Muhammad Seif Khatibu (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Mei 13 hadi 16, 2010, William Ngeleja (Waziri wa Nishati na Madini) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Shinyanga (Ziara ya kwanza) kuanzia tarehe hiyo, Profesa David Mwakyusa (Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) naye alipaswa kuanza ziara mkoani Arusha katika muda huo (ziara ya kwanza).

  Waziri mwingine ambaye alipaswa kuanza ziara katika tarehe hiyo ni Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha na Uchumi), ambaye alipaswa kuwa mkoani Lindi.

  Kundi la pili ambalo limetajwa katika ratiba hiyo linajumuisha mawaziri John Magufuli (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) ambaye alipaswa kuanza ziara mkoani Mara kuanzia Mei 17 hadi 20, 2010.

  Wengine ambao wamepangiwa katika tarehe hiyo ni Dk Diodaurs Kamala (Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki) ambaye alipaswa kuwa mkoani Ruvuma, Sophia Simba (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora) ambaye alipaswa kuwa mkoani Tanga na Profesa Jumanne Mghembe (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi) ambaye alipaswa kuwa mkoani Iringa, katika tarehe hiyo.

  Kundi la tatu ambalo limetajwa kwenye ratiba ya waraka huo linahusisha mawaziri Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) ambaye kuanzia Mei 21 hadi 24, 2010 atapaswa kuwa mkoani Morogoro, Mathias Chikawe ( Waziri wa Sheria na Katiba) ambaye atapaswa kuwa mkoani Rukwa, Philip Marmo (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge) atapaswa kuwa mkoani Singida.

  Waraka huo umeeleza kuwa kundi la nne litamjumuisha Profesa Juma Kapuya (Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), ambaye kuanzia Mei 25 hadi 28, atapaswa kuwa mkoani Mwanza, wengine ni Stephen Wassira (Kilimo, Chakula na Ushirika) ambaye atapaswa kuwa mkoani Tabora.

  Katika ratiba ya tarehe hiyo, Lawrence Masha (Mambo ya Ndani) atapaswa kuwa mkoani Kagera na Shamsa Mwangunga (Maliasili na Utalii) atapaswa kuwa mkoani Arusha (mara ya pili).

  Kundi la tano, kwa mujibu wa ratiba hiyo, litamuhusisha Profesa Mwandosya (Waziri wa Maji na Umwagiliaji) kuanzia Mei 29 hadi Juni mosi, atapaswa kuwa mkoani Dodoma, Celina Kombani (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi) atapaswa kuwa mkoani Shinyanga (mara ya pili), Prof Peter Msolla (Mawailiano, Sayansi na Teknolojia) atapaswa kuwa mkoani Kilimanjaro.

  Kundi la sita ambalo limetajwa katika ratiba hiyo, litahusisha mawaziri, Dk Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mtwara kuanzia Juni 2-5, George Mkuchika (Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mwanza, Dk Shukuru Kawambwa (Miundombinu) atapaswa kuwa mkoani Manyara, Magaret Sitta (Maendeleo ya Jamii, Jinsi na Watoto) atapaswa kuwa mkoani Mbeya na John Chilligati (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) atapaswa kuwa mkoani Kigoma.

  Utaratibu huu uliwahi pia kutumiwa wakati wa bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne, ambayo mawaziri walitawanywa mikoani kuinadi na kuitetea.

  Source: Mwanachi ta leo 21.05.2010
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli inashangaza!
   
 8. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I thought JK said he doesnt need TUCTA???????
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Basi ujinga wetu tutawasikiliza hawa mafisadi na kukubali wamefanya walichokiahidi, tusiwe wadanganyika jamani tuwapige chini hawa jamaa
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kwa nini ewe CCM unanilazimisha nikuchukuie kila siku?
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi hizo pesa za mizunguko hiyo wametoa wapi? TUCTA walitaka kuandamana wenyewe wanadai hakuna pesa! sasa hizo zimetoka wapi?
  Tuwaulize hawa viongozi ? Wasije kufuja pesa zetu hovyo? Wandugu tuwazomeeni tena safari hii.
   
 12. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  I am getting mad about this! Oh my God, how dare Ikulu aandae ratiba ya kuteketeza fedha zawalipa kodi in such a silly way! Watnzania nilazima sasa tuamke, tuache kuwa bong lala. Hawezekani Kikwete atumie hela kiharamu hivi. Jana tuu tumembiwa wanafunzi wa elimu ya juu hawajapata pesa kisa bodi haijapata hela. Hii ni dhambiii!
   
 13. d

  damn JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Those in red ni mirindimo ya pwani, mafanikio yapi? Kueleza walivyotajirika kipindi hiki kwa kuiba na kuuza maliasili? or Kiranja wao si amesema hahitaji kura za wafanyakazi?
   
 14. S

  Samat Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikisema hizo ni kampeni tu nitakuwa nakosea? Sioni kikubwa kilichofanyika mpaka zifungwe safari za kuelezwa wananchi. Ni unafiki tu na njia za kuwarubuni wananchi na october wachaguliwe tena..... Fumbueni macho wananchi, viongozi wetu wamejaa ujanja tu ili muwape kura tena... na baada ya kuwapa kura, mbio zile zile za kukaa Daresalam na kusahau majimbo yao zitarudi tena.
  Nachukia sana SIASA za ulangai za Tanzania.!!!!
   
 15. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapa ndio tatizo la kuchanganya watendaji wa serikali na wanasiasa, mlango wa kutumia chama kuendeleza siasa ukifungwa, wanafungua mlango wa serikali kuendeleza chama. Inabidi nafasi za uwaziri ziwe ni kwa wenye sifa wanaopendekezwa na sio hawa wa sasa.
   
 16. R

  Ramos JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Good. Good sana...

  Ndo wakati mzuri wa CHADEMA kupiga counter attack. Si wameamua kushambulia wote...
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya kikwete akiongoza kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana kujadili mchakato wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

  KATIKA kile kinachoonekana ni kujipanga vema na kujihami kwa maswali magumu wakati wa kampeni za uchaguzi, Ikulu imetoa waraka wa kuzuia mawaziri kusafiri nje na badala yake kuwaagiza kuzunguka mikoani kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

  Waraka huo, ambao umepewa jina la "Mlitutuma, Tumetekeleza, Tumerudi Kuwaelezeni Tulivyotekeleza na Kuwasikilizeni", pia unawaagiza mawaziri kukutana na watu wa aina mbalimbali kwenye ziara hizo, wakiwemo viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

  Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Ikulu kutoa maagizo kama hayo baada ya ziara ya kwanza iliyofanywa mwaka 2007 ya kutetea na kuelezea bajeti ya mwaka 2007/08, ambayo ilikuwa ya kwanza kwa serikali ya awamu ya nne, kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za walipakodi na kampeni za mawaziri kupata ujumbe kwenye halmashauri kuu ya CCM, chombo ambacho ni cha pili kimamlaka kwenye chama hicho kikongwe baada ya mkutano mkuu.
  Pia katika ziara hizo, mawaziri walijikuta wakiishia kufanya vikao vya ndani ya chama kutokana na wananchi kuwazomea kila walipotaka kufanya mikutano.
  “Huko nyuma, tumepata kuwaandalia Outreach Programmes angalau mara mbili. Zote mbili zilianza vizuri lakini zikaishia njiani kabla ya kumalizika,” inasema sehemu ya waraka huo.

  “Ili kuhakikisha kila waziri anatekeleza wajibu wake katika hili, tunashauri ziara zote za mawaziri za nje ya nchi zisimamishwe hadi kila waziri atakapokuwa amefanya ziara yake.”

  Waraka huo umetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa amewatangazia vijana, viongozi na wana CCM wote kujiandaa kujibu tuhuma za ufisadi ambazo zitaibuliwa na wapinzani kama silaha kwenye kampeni za uchaguzi wa Oktoba.
  Agizo hilo la Kikwete alilolitoa juzi mjini Iringa wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM), limedhihirishwa na waraka huo ambao umeambatana na ratiba ambayo inaonyesha ziara za mawaziri hao mikoani kueleza wananchi mafanikio ya serikali katika kutatua kile walichoituma.

  Katika waraka huo wa Mei 11, Ikulu imeelekeza na kutoa mapendekezo ya wadau husika ambao kila waziri atapaswa kukutana nao katika mikutano yake mikoani kwa mujibu wa ratiba.

  Waraka huo, ambao Mwananchi imeona nakala yake, umeelekeza kwamba katika mkutano wa kwanza waziri atapaswa kukutana na wafanyakazi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa CCM.

  Agizo hilo la waraka limetaja wadau wengine wakuu wanaopaswa kukutana na mawaziri kuwa ni pamoja na wajumbe wa nyumba kumi, wawakilishi wa sekta za wizara zilizopo mkoani humo, wawakilishi kutoka sekta ya biashara mkoani na wawakilishi wa sekta nyingine za uchumi.

  Sehemu ya waraka huo ambao unatokana na maamuzi kati ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu) na wasemaji wa wizara za serikali, imetoa pia ratiba ambayo kila waziri atapaswa kutembelea mkoa mmoja kwa tarehe maalum iliyopangwa.

  “Inapendekezwa katika programu hii kila waziri atembelee mkoa mmoja kwa tarehe zilizopangwa...,” inaeleza sehemu ya waraka huo.

  Waraka huo umeelekeza madhumuni mawili ya ziara hizo ambayo ni pamoja na kila waziri kueleza mafanikio ya wizara yake katika miaka mitano ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne na kusikiliza kero na shida za wananchi katika maeneo wanayotembelea na kujibu hoja.

  Ikulu imeeleza katika waraka huo ikisema: “Kabla na baada ya ziara ya waziri, kila wizara itatakiwa kufanya mambo yafuatayo, kutengeneza vipindi maalumu viwili in the form of Documentaries (katika mfumo wa vipindi vya makala (redio na TV)).”

  Kazi nyingine kwa mujibu wa waraka huo ni pamoja na “kuandaa tangazo fupi (public service announcement) kutangaza mafanikio ya wizara katika miaka hiyo mitano kwa ajili ya redio na televisheni na matangazo hayo yaanze kutumika mara moja".

  Pia wametakiwa "kuandaa retreat na wahariri wakuu na wahariri waandamizi wa vyombo vya habari nchini kwa nia ya kujenga uhusiano na vyombo hivyo na pia kuwaelezea wahariri hao mafanikio ya serikali ya awamu ya nne".
  “Kabla ya kuanza ziara, kila waziri aandae mkutano mkubwa wa waandishi wa habari kuelezea mafanikio na shabaha ya ziara yake,” unaeleza waraka huo.

  “Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inapendekeza kuwa ofisi zote za wakuu wa mikoa zifuatilie ratiba hiyo ili kuandaa na kufanikisha mikutano hii na waziri husika.

  “Pia taarifa kwa vyombo vya habari iandaliwe kabla ya kuanza na ratiba nzima ya waziri na mkoa itolewe kwa wana habari.”

  Ratiba ya ziara iyo inaonyesha, mawaziri Muhammad Seif Khatibu (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Mei 13 hadi 16, 2010, William Ngeleja (Waziri wa Nishati na Madini) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Shinyanga (Ziara ya kwanza) kuanzia tarehe hiyo, Profesa David Mwakyusa (Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) naye alipaswa kuanza ziara mkoani Arusha katika muda huo (ziara ya kwanza).

  Waziri mwingine ambaye alipaswa kuanza ziara katika tarehe hiyo ni Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha na Uchumi), ambaye alipaswa kuwa mkoani Lindi.

  Kundi la pili ambalo limetajwa katika ratiba hiyo linajumuisha mawaziri John Magufuli (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) ambaye alipaswa kuanza ziara mkoani Mara kuanzia Mei 17 hadi 20, 2010.

  Wengine ambao wamepangiwa katika tarehe hiyo ni Dk Diodaurs Kamala (Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki) ambaye alipaswa kuwa mkoani Ruvuma, Sophia Simba (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora) ambaye alipaswa kuwa mkoani Tanga na Profesa Jumanne Mghembe (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi) ambaye alipaswa kuwa mkoani Iringa, katika tarehe hiyo.

  Kundi la tatu ambalo limetajwa kwenye ratiba ya waraka huo linahusisha mawaziri Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) ambaye kuanzia Mei 21 hadi 24, 2010 atapaswa kuwa mkoani Morogoro, Mathias Chikawe ( Waziri wa Sheria na Katiba) ambaye atapaswa kuwa mkoani Rukwa, Philip Marmo (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge) atapaswa kuwa mkoani Singida.

  Waraka huo umeeleza kuwa kundi la nne litamjumuisha Profesa Juma Kapuya (Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), ambaye kuanzia Mei 25 hadi 28, atapaswa kuwa mkoani Mwanza, wengine ni Stephen Wassira (Kilimo, Chakula na Ushirika) ambaye atapaswa kuwa mkoani Tabora.

  Katika ratiba ya tarehe hiyo, Lawrence Masha (Mambo ya Ndani) atapaswa kuwa mkoani Kagera na Shamsa Mwangunga (Maliasili na Utalii) atapaswa kuwa mkoani Arusha (mara ya pili).

  Kundi la tano, kwa mujibu wa ratiba hiyo, litamuhusisha Profesa Mwandosya (Waziri wa Maji na Umwagiliaji) kuanzia Mei 29 hadi Juni mosi, atapaswa kuwa mkoani Dodoma, Celina Kombani (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi) atapaswa kuwa mkoani Shinyanga (mara ya pili), Prof Peter Msolla (Mawailiano, Sayansi na Teknolojia) atapaswa kuwa mkoani Kilimanjaro.

  Kundi la sita ambalo limetajwa katika ratiba hiyo, litahusisha mawaziri, Dk Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mtwara kuanzia Juni 2-5, George Mkuchika (Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mwanza, Dk Shukuru Kawambwa (Miundombinu) atapaswa kuwa mkoani Manyara, Magaret Sitta (Maendeleo ya Jamii, Jinsi na Watoto) atapaswa kuwa mkoani Mbeya na John Chilligati (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) atapaswa kuwa mkoani Kigoma.

  Utaratibu huu uliwahi pia kutumiwa wakati wa bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne, ambayo mawaziri walitawanywa mikoani kuinadi na kuitetea.
  Serikali yahaha Uchaguzi Mkuu, IKULU YAZUIA MAWAZIRI KWENDA NJE
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Wakati wote walikuwa likizo kwenda mikoani eti sasa ndio wanagundua umuhimu wa kutangaza mafanikio yao. Yako wapi mbona hayaonekani? Au mkutano wa sullivan na huu wa WEF? Barabara za Mkapa, Uwanja wa Mkapa, Madaraja ya Mkapa! Awamu ya nne imetuletea iflation about 15%, maisha magumu kwa kila mtanzania, uongozi legelege na usanii uliotukuka! Haya ndio naona waende kuyaelezea
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yah kuwaweka sawa wanainchi ndio hivyo ,sort of campaign.
  Watatumia kiasi gani kuzunguka ,hizo pesa si zinaweza kuwa relocated for other issue zenye tija kwa inch kama yetu ambayo tunakopa na kufadhiliwa sehemu ya bajeti.!!Kwa nini wasitumie wakuu wa wilaya na mikoa kutoa taarifa hizo.Ama ktk campaign wanaweza kueleza mafanikio hayo ,save them money idiota!!!!!!!!
   
Loading...