Ikulu yawajibu walimu, yasema mgomo ni Batili, kesi iko mahakamani

Kwanini Ikulu imejibu haraka lakini wakakaa kimyaa kwenye mgomo wa madaktari? Na iwejue Ikulu ndio itoe tamko na sio wizara ya Elimu? Dr Shukuru Kawambwa yuko wapi?

Nchi hii huijui mkuu!!,ikulu ndo kila kitu, hadi kuzindua gereji ya kampuni binafsi,hii ndo maana ya serikali SIKIVU!
 
Kama suala liko mahakamani, kwa nini lisitoe tamko la kuharamisha mgomo badala ya kumwachia mlalamikiwa kutoa TAMKO!
 
Ngoja wanajeshi nao wanataka kugoma, maana wao hakuna anayestafuu na miaka 55, SSRA mpo?
 
ITV habari

Kama kawaida Ikulu ya Jk imetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mgomo wa walimu unatarajiwa kuanza ni batili na hautakiwi kuwepo kwani haujafuata taratibu na kesi yake iko mahakamani.

Hivi kesi ya Walimu na Serikali si ilikuwa CMA?
 
Kwa niwajuavyo walimu mkwara huo ni tosha kabisa kuwawafanya wa'retreat. Hiyo kesi mahakamani inachukua muda gani? Naona sasa mahakama imekuwa kichaka cha serikalli na Bunge kukwepa hoja za msingi za madai ya raia wake.

MATICHA ni muhimu sana kuliko hata hao madokta lakini tatizo lao umoja ni SIFURI!
 
umelewa gongo au umevuta bange ww..! Mie nina wadogo zangu 3 ni walimu wenye masters na mmoja ana phd. Vyeti vyao kama havitambuliwi basi ni ww na sirikali yako! Koma kuwadhalilisha walimu hivyo.

vipi mkuu! Mbona umeruka shahada ya kwanza angali wanahitajika sana kwa general kagame?
 
Mahakama si ndio sehemu yao ya kukimbilia, kweli jk dhaifu na ccm ni uozo mtupu badala ya kushughulikia madai ya walimu wanakimbilia mahakamani? Kama noma na iwe noma..............!!!!mgomo pale pale
 
Umelewa gongo au umevuta bange ww..! Mie nina wadogo zangu 3 ni walimu wenye Masters na mmoja ana PhD. Vyeti vyao kama havitambuliwi basi ni ww na sirikali yako! Koma kuwadhalilisha walimu hivyo.

Chifu,nafikiri alimaanisha mfumo wa serikali hii kuchukua watu waliopata divisheni 4 katika kidato cha 4. Utaratibu huo upelekea watu ambao katika jamii uonekana 'failures' kuingia ualimu. Hivyo,pengine jamaa alimaanisha kwamba kwa mfumo huo ni dhahiri walimu watakuwa wanaogopa.

Lakini si walimu wote ni 'failures',wengine walifaulu vizuri sana kidato cha 4.
 
Napata taabu kidogo kuelewa kuhusu suala la utendaji kijumla. Kwanini kila kitu ni lazima kijibiwe na ikulu?. Wizara husika zinafanya nini?. Mh. Raisi alichagua mawaziri na makatibu wakuu wa ma-wizara kwa lengo la kumsaidia kufanya kazi, sasa inakuwaje kila kitu ni lazima kisemewe na ikulu?. Mawaziri na makatibu wakuu wa wizara husika wako wapi na wanafanya nini?. Jamani mpeni nafasi Mh Raisi afanye mambo mengine mazito na kama hamuwezi kazi basi acheni mara moja ili wanaoweza wafanye hizo kazi.
 
Hivi nani mkweli kati ya serekali na chama cha walimu? Chama cha walimu walisema mazungumzo yamekwama na hawakusema kama yameenda mahakamani sasa hapa mahakama inaingia vipi au ndio kificho cha serekali kwa kila tatizo ?
 
Unategemea nini kwa serikali ambayo imeshashindwa kujibu hoja na kubaki na vitisho. Haya kazi kwenu walimu LIWALO na LIWE
 
kwa mujibu wa ITV ikulu
imetoa kauli kuwa mgomo wa waalimu unaotarajiwa kuanza jumatatu ni
batili kwa kuwa suala hilo liko mahakamani.serikali imewataka waalimu
nchini kupuuza taarifa ya CWT.

Kama inataka walimu waipuuze cwt basi isiwakate mishahara yao kilazima kuchangia cwt!
 
Hiyo kesi ilifunguliwa lini na Serikali, mahakama ipi, tarehe gani, file number, hakimu/jaji yupi? Walimu wameshapewa taarifa kwamba kuna kesi ipo mahakamani na anayetakiwa atoe taarifa kwa CWT ni nani kati ya Serikali na mahakama. Wahuni bana
 
Hiyo kesi ilifunguliwa lini na Serikali, mahakama ipi, tarehe gani, file number, hakimu/jaji yupi? Walimu wameshapewa taarifa ya maandishi kwamba kuna kesi ipo mahakamani na anayetakiwa atoe taarifa kwa CWT ni nani kati ya Serikali na mahakama. Wahuni bana
 
Natoa wito kwa Rais Kikwete kuwa ubabe, ujeuri na kiburi cha kuwa Rais kitalipeleka Taifa pabaya, Rais ujue kuwa cheo ni dhamana. Hivyo tunakushauri kama walimu kuwa kukimbilia mahakamani na kutoa vitisho havitasaidia Taifa hili. Bila kuwepo walimu leo hii wewe usingekuwa hivyo ulivyo na hata wale majaji bila walimu wasingekuwa hivyo walivyo.

Hivi hata huyo mama Salma hakupi ushauri maana naye ni mwalimu? Au ndo kasahau kuwa naye alikuwa mwalimu. Hivi inakuwaje walimu ndo wanapata mshahara mdogo kuliko sekta zote nchini.

Jawabu la mgomo wa walimu ni kusikiliza madai yao, ubabe na udikiteta hautakusaidia bali utazidisha chuki kwa watanzania maana wanaelewa jinsi walimu tunavyoonewa wakati wabunge wanalipwa mishahara mikubwa kwa kulala bungeni. Hiv Rais hili hulioni au unasubiri kila kitu kiharibike katika Taifa letu?

Kama Rais utaacha nini cha kujivunia? Migomo? ufisadi?au matumizi mabaya ya madaraka na mali ya uma? Ujue umepewa dhamamana acha kuitumia vibaya.

Enzi za Nyerere watanzania tulijivunia umoja na mshikamano kwani yeye mwenyewe alikuwa mwadilfu na ndiyo uzalendo ukawepo, wakulima waliishi vizuri na walimu waliheshimika sana.


Enzi za mzee Ruksa wafanyabiashara walifaidi sana maana maisha yao yaliimarika.


Mzee mkapa, uchumi uliimarika kiasi kwamba mfumuko wa bei ulishuka sana. sekta ambayo walijiskia vema ni wafanyakazi wote.

Wewe je ni lipi UBABE? Jirekebishe jaribu kuona aibu kidogo kututishia walimu na ofisi yako. Usalama wa Taifa umegeuka mali yako. Hii ni aibu kubwa. Hata watu wa nje wanakufahamu nilisoma hapa kuwa watanzania kwa wema wetu hatustahiri kuongozwa na dikiteta kama wewe.

Hata hao wanaokuunga mkono kila ukitoa hotuba za kibabe wanakupoteza ni wanafiki wakubwa. Bora uambiwe maneno ya kweli ili ujirekebishe kuliko sifa ambazo zitalipeleka Taifa pabaya.

Hivi serikali haioni vibaya kuwalazimisha walimu waende kazini bila kutimiziwa madai yetu. Tunaweza kwenda na kufundisha tofauti hapo tatizo litakuwa limetatuliwa au tutaenda darasani na walinzi kukagua tunafundisha nini.

Natamania kusema mengi ila najiuliza hivi hata wewe hujui kuwa ukimlazimisha mwalimu ataderiver mabaya baadala ya yanayotakiwa kufundishwa.

Tuache walimu tugome kama hutaki kutupa kile tunachodai, ni mgomo upi uliowahi kuonekana ni halali. KWA UFUPI UBABE HAUTATUSAIDIA!
 
kwa mujibu wa ITV ikulu imetoa kauli kuwa mgomo wa waalimu unaotarajiwa kuanza jumatatu ni batili kwa kuwa suala hilo liko mahakamani.serikali imewataka waalimu nchini kupuuza taarifa ya CWT.

ikulu ndio wizara gani sikuhizi? Ni elimu au mahakama au ya migomo.
Inaonekama ukitaka kugoma sikuhizi ukaombe kibali ikulu.
 
hivi kwa nini? Walimu hatufaidi Keki ya Taifa Afya, Kilimo, Sheria, Jeshi Hao wanafaidi malipo ya nyumba, usafiri sisi ndo watumishi ambao tunaishi kwa plain salary bila posho yeyote bila nyumba wala usafiri. Kwa nini sometime Nawish kinuke wote TUWE katika taharuki, coz katika chaos wanaofaidi Keki ya Taifa na tusiofaidi tutakuwa Hali moja... Bora kinuke tuanze UPYA
 
Mwalimu ndiye anadharauliwa kuliko hata mzibua vyoo mjini. Inasemekana kuwa cheti kimoja hutumika kwa walimu zaidi ya watano, ndiyo maana hamthubutu kugoma! Mtakimbilia wapi? Mko zaidi 51% ya watumishi wa umma, lakini hamna maamzi yoyote nyie. Mazobe wakubwa, ipo siku mtatandikwa mboko matakoni na mkasema asante kwa kututia adabu. Wasomi gani nyie?????
 
Habari nilizozipata ni kwmb mgomo wa walimu uliotarajiwa kuanza jumatatu,Serikali imetoa onyo kupitia vyombo hbr ya kwmb ni marufuku kwa mwalimu yeyote kufanya mgomo kwani JAMBO HILI LIKO MAHAKAMANI.

Hiyo ndiyo kauli ya serikali yetu tawala kwa walimu wetu.

TUTAFIKAAAA!!
 
Back
Top Bottom