Ikulu yawajibu walimu, yasema mgomo ni Batili, kesi iko mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yawajibu walimu, yasema mgomo ni Batili, kesi iko mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jul 27, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ITV habari

  Kama kawaida Ikulu ya Jk imetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mgomo wa walimu unatarajiwa kuanza ni batili na hautakiwi kuwepo kwani haujafuata taratibu na kesi yake iko mahakamani.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  Madaktari au Walimu?

   
 3. S

  Skype JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu vipi tena? Mbona heading umeandika walimu lakini content unazungumzia madaktari? Au nimekunukuu vibaya? Naomba mwongozo wako tafadhali!
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwa mujibu wa ITV ikulu imetoa kauli kuwa mgomo wa waalimu unaotarajiwa kuanza jumatatu ni batili kwa kuwa suala hilo liko mahakamani.serikali imewataka waalimu nchini kupuuza taarifa ya CWT.
   
 5. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kuregenzi ya ikulu imejibu notes ya masaa 48 waliyotoa chama cha waalimu hadi j3 kama hakitaeleweka mgomo utaanza rasmi,kawa kawaida yao serikali imesema suala hilo liko mahakamani na imetoa onyo waalimu kuangalia athari watakayopata once wakijiusisha na huo mgomo.

  Source:TBC habari
   
 6. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nimerekebisha mkuu thanks
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwanini Ikulu imejibu haraka lakini wakakaa kimyaa kwenye mgomo wa madaktari? Na iwejue Ikulu ndio itoe tamko na sio wizara ya Elimu? Dr Shukuru Kawambwa yuko wapi?
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama kawaida serikali imekimbilia kichaka chake cha mahakamani.
  Kilichonishangaza ni kuwa tangazo limetolewa na ikulu badala ya mahakama ya kazi.pia serikali imeliongelea suala liloko mahakamani!
   
 9. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSUDIO LA WALIMU KUGOMA
  ____________________________________________
  SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Ijumaa, Julai 27, 2012 majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saa arobaini na nane (48) ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusu asubuhi.

  Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha maslahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwa kutumia vyombo na ngazi mbali mbali za kisheria.

  Kwa sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012 saa sita mchana, ili kuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi.

  Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hili bado liko Mahakamani.

  Kwa msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwa mgomo kabla ya kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakama ambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.

  Serikali inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwa kujihusisha na mgomo huu ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi. Hivyo, walimu wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikali inawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wote wanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.


  Peniel M. Lyimo
  KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  27 Julai, 2012
   
 10. w

  wikolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Taarifa ya ikulu imesema mgomo wa walimu uliotarajiwa kuanza jumatatu baada ya walimu kutoa notisi ya masaa 48 ni batili kwa sababu suala hilo linaendelea kujadiliwa mahakamani. Taarifa hiyo ya ikulu imesema mahakama imeziagiza pande zote mbili kwenye mgogogro huo zipeleke taarifa zao siku ya jumanne kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka ikulu, walimu wote wanatakiwa kuendelea na kazi kama kawaida kwa vile mgomo ni batili!

  Source TBC1.
   
 11. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kila kitu kipo mahakamani...kweli hatuna serikali
   
 12. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mhh jamani kunani serikali ya JK mbona migomo ya namna hii haikuwepo wakati wa BWM?? wanamuonea? kuna nini cha kujifunza kwa serikali kuhusiana na series ya migomo katika kipindi chote cha serikali ya awamu ya nne?
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  atakayegoma kufukuzwa
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kila kitu ni batili ni kwa serikali kwa sababu yenyewe ndiyo inayogomewa, ulitegemea wasemeje zaidi ya mbinu za suala lipo mahakamani.
   
 15. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Kweli serikali tunayo... Kha!
   
 16. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,945
  Trophy Points: 280
  Mkoba ndiyo mchawi wa walimu.
   
 17. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  haah haaah haah Kunji mwanzo mwisho.
   
 18. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kama walifukuzwa madokta kisha baadae mnataka kurudi kwenye mazungumzo tena. Wasikilizeni hoja zao walimu badala ya kukimbilia kuwatisha.
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ni mgomo batili hata kuliko ule wa madaktari.

  mfupa uliomshinda fisi (daktari) mwalimu ataweza.

  huu ni mgomo wa kuigiliza ...eti waligoma madaktari na sisi waalimu tugome.... hauna nguvu
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa niwajuavyo walimu mkwara huo ni tosha kabisa kuwawafanya wa'retreat. Hiyo kesi mahakamani inachukua muda gani? Naona sasa mahakama imekuwa kichaka cha serikalli na Bunge kukwepa hoja za msingi za madai ya raia wake.
   
Loading...