Ikulu yatoa 'Nembo Rasmi' ya sherehe za miaka 50 ya uhuru

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,345
29,146
attachment.php

Wadau,
Hiyo ndiyo nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo imepitishwa rasmi na Kamati ya Taifa ya Madhimisho hayo chini ya Katibu Mkuu Kiongozi..



 

Attachments

  • D - NEMBO YA MIAKA 50 (SWAHILI).jpg
    D - NEMBO YA MIAKA 50 (SWAHILI).jpg
    22.5 KB · Views: 617
hatuna la kujivunia,ni heri mkoloni alileta maendeleo kuliko utawala wetu uliofuata!!!50yrs of independence for what?
 
Haina mashiko kwa kupoteza pesa za walipa kodi kufanya sherehe ya nchi ambayo haijawahi kupata uhuru kwani iliyopata uhuru ni
Tanganyika na siyo story za Tanzania bara. Maadui wa Tanganyika maradhi, ujinga, na umasikini bado yapo na tumeongezewa na ufisadi na janga la umeme still tunasherehekea what for?
 
Nchi yenyewe iko wapi mimi siku hiyo nitavaa kitambaa cheusi mkononi kuomboleza.
 
Nasikia mbunifu wake ni muhindi ameshakula million hamsin tsh 50, kwa ajili ya kubuni hicho kitu..... Tanzania tanzania tanzaina.....
 
attachment.php

Wadau,
Hiyo ndiyo nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo imepitishwa rasmi na Kamati ya Taifa ya Madhimisho hayo chini ya Katibu Mkuu Kiongozi..




Wameweza nini? Kuiba Rasilimali zetu? Ikulu sikuhizi imegeuzwa Kichaka cha Majambazi sugu 1 kikoongozwa Fisadi Papa Kikwete. Hebu watutolee upumbavu wao huko. watasheherekea wajinga na wapumbavu hiyo siku, Tunachodai ni Uhuru wetu wa kweli na haki zetu za uttu
 
hivi tanzania zipo mbili?yaani tanzania bara na tanzania visiwani?kwanini wasiseme TANGANYIKA?au tanganyika ni dhambi.yangu macho.
 
Mimi sikubaliani na hao walioipitisha hiyo nembo kwa sababu inaupotosha umma wa watanzania...Kwa nini tunalazimishwa kuukataa UKWELI,kwa kupindisha historia?Kwa nini nembo iwe na alama ya bendera ya TANZANIA,wakati tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa TANGANYIKA?
 
hivi ni miaka 50 ya tanganyika au tanzania ??? hainiingii akilini kama ni tanzania wana miaka 46 na si hamsini jamani hata hesabu za kujumlisha magamba hawawezi?????
 
Haina mashiko kwa kupoteza pesa za walipa kodi kufanya sherehe ya nchi ambayo haijawahi kupata uhuru kwani iliyopata uhuru ni
Tanganyika na siyo story za Tanzania bara. Maadui wa Tanganyika maradhi, ujinga, na umasikini bado yapo na tumeongezewa na ufisadi na janga la umeme still tunasherehekea what for?

CCM ndiyo kiongozi wa maadui hao ndiyo that is why wanaposema 'Rushwa ni adui wa haki' ina maana kwamba katika maadui wenye haki ya kuwepo katika nchi hii ni pamoja na Rushwa. Tia akilini.
 
Mwenge wa uhuru upo wap siku hz? then zile nyimbo zake nshazisahau. Kweli dunia hii ya utandawazi!
 
Wadau,
Hiyo ndiyo nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo imepitishwa rasmi na Kamati ya Taifa ya Madhimisho hayo chini ya Katibu Mkuu Kiongozi..



NA HII BENDERA KWENYENEMBO INA MIAKA MINGAPI MPAKA 9/12/2011! NAOMBA MWENYE CV YA LUHANJO AIWEKE HAPA JF TUONE SHULE ALIZOSOMA ZINAITWAJE NISIJE KUPELEKA MTOTO WANGU HUKO.HIYO BENDERA KWENYE NEMBO NA JINA LA TANZANIA BARA WAPI NA WAPI HAYA SALVA NJOO UTOE UFAFANUZI.MSITUKUMBSHE MBALI JAMANI TANGANYIKA YETU TUTAITAFUTA TU MKISHA TUNGA SHERIA YENU YA URAIA WA NCHI MBILIMTAKWENZA NA TANZANIA BARA YENU SISI TUTARUDISHA TANGANYIKA YETU.
 
Nembo hiyo ni idea nzuri ila tu bendera iwe ni ya Tanganyika badala ya hiyo ya Tanzania hapo juu.
 
Hivi kuandika neno Tanganyika ni uhaini? kwanini tusijivunie hilo jina ningeshauri badala ya kuandika Tanzania Bara ambayo haikupata uhuru iandikwe miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
Jamani naona nimesahau historia. Naomba mnikumbushe. Hivi kuna nchi ilipata uhuru mwaka 1961 inayoitwa Tanzania bara? Iko wapi kwenye ramani ya ulimwengu wa wakati huo? Naomba mnisaidie ili niwasaidie watoto wangu kujua historia ambayo huenda nimeisahau.
 
attachment.php

wadau,
hiyo ndiyo nembo ya miaka 50 ya uhuru wa tanganyika ambayo imepitishwa rasmi na kamati ya taifa ya madhimisho hayo chini ya katibu mkuu kiongozi..




tunataka madawa hospitalini; hatutaki nembo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom