Mwanandani
Senior Member
- Apr 5, 2012
- 195
- 44
We choko kwelikweli.na pia dk slaa ashitakiwe au atoe ufafanuzi haraka ile issue ya R1. Hatuwezi tukawa tunachafua majina namna hii.
We choko kwelikweli.na pia dk slaa ashitakiwe au atoe ufafanuzi haraka ile issue ya R1. Hatuwezi tukawa tunachafua majina namna hii.
Ukisoma hizo sentence mbili ni wazi kuwa Kurugenzi ya mawasiliano hawana uhakika na wanachosema. Sentence ya kwanza wanakanusha kuwa raia na familia yake hawahusiki. Lakini sentence ya pili wanataka gazeti limtaje mwanafamilia anayehusika! Pengine wao Kurugenzi wangejiridhisha hakuna mtu anayehusika na hivyo watoe kanusho la ama YES au NO.
Ingekuwa wewe ungeiandikaje?
kumbe hawa taarifa wanazipata kila siku ..kamateni mafisadi basi na wanaosafirisha wanyama wetu au?
kumbe hawa taarifa wanazipata kila siku ..kamateni mafisadi basi na wanaosafirisha wanyama wetu au?
mkuu nyani Ngabu, hivi unaweza kuuchafua mkaa?
ama waweza kuyachafua mavi, ni kwamba hii familia ni chafu!!!!!! kurugenzi ya habari iache kupelekeshwa.
Imejibiwa kienyeji.Huwezi amini kama imejibiwa na Ikulu.
Nivema Ikulu ikawa inatumia wanasheria wake kujibu jambo zito kama hili, kuliko kuwaachia makarani wajibu.
There is no seriousness in it.
Ikulu imetoa taarifa kukanusha kuhusika kwao kwenye biashara na Home shopping centre.
Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012, limechapisha habari yenye kichwa cha habari, "Familia ya JK yachafuliwa".TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.
Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake.
Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.
Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.
Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.
Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.
Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria. ……..Mwisho…..
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.Dar es Salaam.
7 Mei, 2012
MY TAKE: Hivi Kurugenzi ya mawasiliano ni msemaji wa IKULU ama msemaji wa Familia ya JK?
Kwa kweli hii statement ya Ikulu imekaa kienyeji sana!
Duh Nyani Ngabu, unatisha mada ulivyoivalia njuga! Nimeipitia thread yote lakini sijasoma sehemu yoyote CCM imetajwa. Anyway mapenzi pia hupofusha au kuna zaidi!Tatizo watu wengi JF ni anti-everything CCM.
Duh Nyani Ngabu, unatisha mada ulivyoivalia njuga! Nimeipitia thread yote lakini sijasoma hata sehemu yoyote CCM ikitajwa. Anyway mapenzi pia hupofusha au kuna zaidi!
wakiona ina maslahi kwao wanakuwa wepesi kujitokeza kujibu na kujitetea
Much ado about nothing. The response is spot on.