Ikulu yalijibu Gazeti la Dira ya Mtanzania: Yataka watoe majibu au wachukuliwe hatua...

Nafikiri gazeti lilikuwa straight to the point kuwa ni biashara gani analink nayo. Si kazi tena ya gazeti kutoa utetezi bali ni hizo link kujitetea kwamba hazipo.

Tayari team Kikwete imeshakanusha. Sasa ni wajibu wa gazeti kuja na ushahidi wa madai yao.

I like how aggressive team Kikwete is.
 
Hivi Salva anajua anachokifanya? Hivi mkuu akituhumiwa ni kazi ya kurugenzi ya mawasiliano kumjibia? Kama yeye ni mtuhumiwa na hakubaliani na tuhuma ni vema akajibu mwenyewe sio kutuingiza kwenye gharama zisizo na msingi kupitia vyombo vya umma, pia kama kuna haja yakwenda mahakamani si kwa kutumia rasilimali zetu bali anapaswa kufanya kwa taratibu zake binafsi.

Kuna gharama gani kutoa statement kama hiyo?
 


Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.Dar es Salaam.

7 Mei, 2012


Kuna kitu sijakielewa hapa. Hii ni taarifa kwa vyombo vyote vya habari au kwa gazeti lililoandika hii habari? Hii idara ya habari hivi haina watu wanaoweza kuandika kitu kinachoeleweka na kwa ufasaha?? Yaani utadhani taarifa imeandikwa na mtoto wa darasa la 4? Hata angepewa kijana wa shule za kata angeandika kitu cha kueleweka
 
Kuna kitu sijakielewa hapa. Hii ni taarifa kwa vyombo vyote vya habari au kwa gazeti lililoandika hii habari? Hii idara ya habari hivi haina watu wanaoweza kuandika kitu kinachoeleweka na kwa ufasaha?? Yaani utadhani taarifa imeandikwa na mtoto wa darasa la 4? Hata angepewa kijana wa shule za kata angeandika kitu cha kueleweka

Ingekuwa wewe ungeiandikaje?
 
Hivi Salva anajua anachokifanya? Hivi mkuu akituhumiwa ni kazi ya kurugenzi ya mawasiliano kumjibia? Kama yeye ni mtuhumiwa na hakubaliani na tuhuma ni vema akajibu mwenyewe sio kutuingiza kwenye gharama zisizo na msingi kupitia vyombo vya umma, pia kama kuna haja yakwenda mahakamani si kwa kutumia rasilimali zetu bali anapaswa kufanya kwa taratibu zake binafsi.
 
Very disappointing! ila nadhani kwa hili ni vyema tufahamu kuwa wahusika Salva et al wanadhihirisha kwamba hawajui kutofautisha ipi habari ya Ikulu ambayo wao wanapaswa kujibu na ipi ambayo si ya Ikulu wasiyopaswa kujibu.

To make it short they are very white or plain as far their job description is concerned! Inasikitisha sana lakini' kila mtu unapojaribu kuzoea jambo flani linakuja jipya baya zaidi very ennui!
 
Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.


Kwa hiyo ni ruhusa kuichafua Kampuni ya Home Shopping Centre isipokuwa kwa kutumia Familia ya Rais.
Na, kwa nini Ikulu inapenda kukanusha habari na kutoa mtazamo wake wa nini habari husika ililenga? Nadhani hii si sahihi. Inachopaswa kufanya ni kukanusha tu tena kwa maelezo mafupi. Kurugenzi hii ya Ikulu bila shaka ina tatizo.
 
Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

[/QUOTE]
Vipi kuhusu BILILA LODGE ya nani?
 
OK, rais hajawahi, wala hana mpango wa kuendesha biashara yeye na familia yake. Hayo mananasi anayovuna kila siku shambani kwake yanaliwa yote Ikulu, au anatoa msaada kwa baadhi ya taasisi? Miraji ni sehemu ya familia ya Kikwete, hafanyi biashara?

Aje mtu aweke wazi biashara zake hapa na za Riziwan tuondoe doubt, well watakuwa hawaingii front wenyewe may be lkn tutaunga link tu,ukweli haujifichi
 
Wafanyabiashara wanaoingiza ma-container ya bidhaa mbalimbali toka Goungzhou wanamjua sana jamaa. Kuwatolea mzigo/ containers bandarini pasipo kukaguliwa na wazee wa ushuru...unafikiri jeuri hiyo inatola wapi?
 
Ingetosha tu kukanusha bila kutumia maneno mengi ambayo ama yanajichanganya au yanazua maswali.

Kusema kuwa familia haihusiki kabisa na tuhuma hizo na hapohapo kulitaka gazeti liende moja kwa moja kwa kumtaja mhusika exactly ni kujichanganya na kuonyesha hali ya kutokuwa na uhakika.

Kusema kuwa raisi kikwete hajawahi kabisa kufanya biashara ni baada ya urais au hata kabla ya urais?
Ni ipi mipaka ya kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu?Kama inadili hata na kashfa binafsi za familia ya rais?Kama kurugenzi inahusika mpaka na mambo ya familia ya rais ni kwanini ilikaa kimya kipindi kile jina la rais "kuchafuliwa" kutokana na matokeo ya kidato cha nne ya Mwanaasha?
 
Kama kweli. Raisi wetu na Familia yake hawafanyi biashara kabisa, basi tuna raisi wa kipekee sana, na wa kuigwa. Lakini kwani biashara ni dhambi?

Biashara si dhambi. Ila kama biashara hiyo inafanywa na familia ya mtu mwenye dhamana kubwa kitaifa basi ni lazima iwekwe hadharani ili umma ufahamu. Maana ni lazima kuwa kutakuwa na mgongano wa kimasilahi. Yaani kuhakikisha dili zote muhimu zinaelekezwa kwa kampuni hii.

Unajua mkuu unapoongelea good governance maana yake ni lazima kuwe na separation of ownership and management ili kuwe na usimamizi. Rais kama country manager anatakiwa kusimamiwa ili asi abuse dhamana aliyopewa na owners (wananchi). Haya mambo ya kufanya biashara IKULU yanafanya usimamizi wa sheria kuwa legelege, maana kama wewe unafanya basi na mimi ntafanya. Matokeo yake unakuta mpaka wafagia ofisi za serikali wana kampuni za biashara na kuhakikisha sabuni za kusafisha maofisi zinanunuliwa kwenye kampuni zao kwa over and above the market price.

Uchumi wa Tanzania haukuwi kwa sababu watu wachache wanajilimbikizia madili yote ya serikali na kuacha biashara za wasiokuwa na connection kufa kifo cha kawaida. Hebu fikiria mfano serikali ingekuwa wazi kwa mfano kwenye sector ya ujenzi na kuhakikisha kuwa kampuni zote za vijana waliomaliza vyuo na kuamua kujiajiri at least zinakuwa katika mzunguko wa kupewa tenda kulingana na madaja ya kampuni zao nini kingefuata?. Hawa ndiyo watumiaji wakuu na kuwawezesha maana yake unaandaa ajira kwa mama ntilie vijana watakoajiriwa kufanya muuza nyanya mbaye atapata mteja yaani trickle down economy inakuwa realised. Lakini kwa ulafi wao viongozi wapo tayari kuanzisha kampuni leo na kuipatia tenda ya mabilioni ili mradi tu ziingie mifukoni mwao. Na hiki hasa ndicho kinachoonekana kuwa ubaya wa kuwa kiongozi huku ukifanya biashara.
 
Jamani mbona maeneo ya kibaha riz1 anajenga kituo cha mafuta, tana na hoteli kishirikiana na swahiba wake? na pia anamiliki godown kubwa sana maeneo ya tanita ambalo nje utakuta wamedisplay magari 2 tu bali humo ndani wana masemitrela kama 20 hivi. na yana fanya kazi ya kusafirisha mafuta? au labda yeye ni wakili w hizo kampuni tu na siyo zake?
 
Hata mwizi aliyeshikwa na bata wa kuiba manzese alikanusha kuhusika na wizi huku akiwa naye mkononi na akikili kuwa si wake!!
 
Duh! Kwa hiyo hata nikimtuhu Mwanasha au Miraji, Salva atatoa ufafanuzi? Wanaojua protocal hizi watuambie
 
Back
Top Bottom