Ikulu yalijibu Gazeti la Dira ya Mtanzania: Yataka watoe majibu au wachukuliwe hatua... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yalijibu Gazeti la Dira ya Mtanzania: Yataka watoe majibu au wachukuliwe hatua...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, May 7, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ikulu imetoa taarifa kukanusha kuhusika kwao kwenye biashara na Home shopping centre.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012, limechapisha habari yenye kichwa cha habari, "Familia ya JK yachafuliwa".

  Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

  Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake.

  Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.

  Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

  Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

  Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

  Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria. ……..Mwisho…..

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.Dar es Salaam.

  7 Mei, 2012

  MY TAKE: Hivi Kurugenzi ya mawasiliano ni msemaji wa IKULU am
  a msemaji wa Familia ya JK?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  kumbe hawa taarifa wanazipata kila siku ..kamateni mafisadi basi na wanaosafirisha wanyama wetu au?
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni wasemaji wa familia ya JK na Riz
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...teheeeeee,,,,,,kaaazi kwelikweli!
   
 5. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Interejensia yao ni kuangalia CDM wako wapi na nani anamfatilia rais lakin si mambo ya umma
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  wakiona ina maslahi kwao wanakuwa wepesi kujitokeza kujibu na kujitetea
   
 7. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  Hii ni taarifa kutoka familia ya rais au kutoka Ikulu au kutoka Ofisi Binafsi ya Rais (OBR)? Du! Haya.
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Inamaana hata biashara za Riz1 wanazikanusha!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukisoma hizo sentence mbili ni wazi kuwa Kurugenzi ya mawasiliano hawana uhakika na wanachosema. Sentence ya kwanza wanakanusha kuwa raia na familia yake hawahusiki. Lakini sentence ya pili wanataka gazeti limtaje mwanafamilia anayehusika! Pengine wao Kurugenzi wangejiridhisha hakuna mtu anayehusika na hivyo watoe kanusho la ama YES au NO.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  si ndio hapo magazeti yakiandika na kulalamikia ufisadi wanakaa kimya...Rais akiandikwa anafanya biashara wanatoa statement kwani kufanya biashara ni kosa??... ikulu watuambie kukiwa kuna ushahidi kua Bosi wao anapiga madili na HSC atajiuzulu?? sio watu wanakuja na evidence afu bado anabakia tu pale anakenua
   
 11. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  what a shame to the state department!
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hata Kiwira ilikanwa hivi hivi yatajulikana tu, we will leave no stone unturned.
   
 13. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,727
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  na pia dk slaa ashitakiwe au atoe ufafanuzi haraka ile issue ya R1. Hatuwezi tukawa tunachafua majina namna hii.
   
 14. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha ha! nimependa hiyo mh ni mkulima na mfugaji.
   
 15. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Yaani Ikulu imepoteza credibility.. Serikali yote ya Tanzania imepoteza credibility.. Hatari hii..
   
 16. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana yake mkuu.
   
 17. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tetesi nilizosikia from a person who is close to the Said guy ni kwamba in 2010 hsc ilitoa mil 500 kwa ajili ya kampeni za jamaa
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama kweli. Raisi wetu na Familia yake hawafanyi biashara kabisa, basi tuna raisi wa kipekee sana, na wa kuigwa. Lakini kwani biashara ni dhambi?
   
 19. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
   
 20. Eliza wa Tegeta

  Eliza wa Tegeta JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unakuwa kama humfahamu Salva?
  hajuu hata kukanusha!
   
Loading...