Ikulu yakanusha taarifa ya mali za taasisi ya WAMA inayoongozwa na mama Salma Kikwete kupigwa mnada

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
WhatsApp Image 2016-12-04 at 1.07.23 PM.jpeg



TAARIFA KWA VYONIBO VYA HABARI


Katika siku za karibtmi baadhi ya wombo wa habari na mitandao ya kijamii imechapisha taarifa zinazomhusisha Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Mama Salma Kikwete naa Taasisi anayoiongoza ya Wanawanke na Maendeleo (WAMA) kwamba

imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoiingiza nchini na hiwo kuwa hatarini kupigwa mnada.
Taarifa hizo zimemhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa anahusika kuzuia mizigo hjyo bandarini mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

Tunapenda kuutalifu umma kuwa taarifa hizo sio kweli na ni uzushi, na Rais Magufuli hajawahi kuzuia wala kuagiza kuzuiwa kwa mizigo ya Mama Salma Kikwete.


Rais Magufuli amesikitishwa sana na uzushi huo unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake na amewataka waandishi wa habari na wombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake wazingatie weledi na kufuata sheria.


“Nimesikitishwa sana na uzushi unaofanywa dhidi ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete tafadhali mnaotengeneza uzushi huu muache mara moja, muacheni Rais mstaafu Kikwete apumzike''.


“Rais Mstaafu Kikwete amefanya makubwa kulitumikia taifa hili, amestaafu anampumzika, narudia muacheni apumzike, serikali haiwezi kuendelea kuvumilia uzushi na uchonganishi unaofanywa kwa makusudi kuwachafua viongozi wastaafu'' Ameonya Rais Magufuli

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam
O4 Desemba, 2016
 
sasa hawa wanaotunga hizi habari wawe wanafikiria kidogo, Magufuli alitamka hadharani kabisa kuwa atamlinda Kikwete leo aje apige mnada mali za taasisi ya mkewe? Watanzania bana..
 
Taarifa ya kukanusha uzushi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii zinazomhusisha Rais Dkt Magufuli kuzuia mizigo ya aliekuwa mke wa Rais wa Awamu Ya Nne Mama Salma Kikwete
1480846666310.jpg
 
Kwani anausafi gani hata achafuliwe?

Tunakumbukizi ya nyumba za serikali zilizogawiwa kwa kwaa kwaaa kwaa!!!

Nina kigugumizi.
Nitarejea baadae
 
Msigwa inabidi na wewe ubadilike.. Huu uandishi wa karne ya saba achana nao.. Sasa ofisi yako inabidi ielewe nafasi kubwa ya mitandao ya kijamii.. Barua zako inabidi zianze kusomeka hivi, "Taarifa kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii"...
 
Eti wamekanusha hivi Ikulu siku hizi ndio TRA?.......

Ikulu siku hizi ndio bandari?.............

Yaani jambo dogo kama hili eti serikali inakanusha kutokea ikulu.........

Kwahiyo watu wanaouziwa mahoteli,Nyumba ,na Mali zao maagizo yote yanatoka Ikulu kwa Magufuki ili wafanyiwe hivyo?.......

Kweli tumeingia chaka awamu hii.......
 
Hawa wanajaribu kuonyesha ubaya wa mitandao ya kijamii ili waseme imejaa uzushi na tunaifungia...alafu malaika wa mtandao anashuka
 
Kama ni uzushi, tcra watafute chanzo kisha wakichukulie hatua za kisheria na watujuze, vinginevyo mimi nitaona imekanushwa kiutu uzima!
 
Eti wamekanusha hivi Ikulu siku hizi ndio TRA?.......

Ikulu siku hizi ndio bandari?.............

Yaani jambo dogo kama hili eti serikali inakanusha kutokea ikulu.........

Kwahiyo watu wanaouziwa mahoteli,Nyumba ,na Mali zao maagizo yote yanatoka Ikulu kwa Magufuki ili wafanyiwe hivyo?.......

Kweli tumeingia chaka awamu hii.......
Na mlivyosema yeye amezuia hamkuliona hilo au bado mnaweweseka na kipigo cha octoba 2015??
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom