Ikulu yakanusha taarifa ya mali za taasisi ya WAMA inayoongozwa na mama Salma Kikwete kupigwa mnada

Huyu Rais wa CCM badala ya kushughulika na mambo makubwa kama ishu ya Dangote yeye ameamua kukimbilia kigodoro cha Mama Salma, dah!
 
Ya dangote tuliambiwa kafunga kwasababu ya garama za uzalishaji amepandishiwa baadae tukaambiwa sio hivyo ni mitambo inarekebishwa baadae ukwl ukasimama na hya kma in uzushi basi ushwindwe kma sio ukwl utasimama hatakama kwa hili lbda kwa lingine
 
Nakumbuka hii habari niliiona front page kwenye gazeti la raia mwema na Zanzibar Leo kwamba " Mali za Salma kikwete kuuzwa kwa mnada" .
Naomba magazeti haya yachukuliwe hatua stahiki kwa kumchafua Kikwete na familia yake.
 
Hii alipaswa kukanusha yeye au watu wa TRA? Ukiona TRA wako kimya ujue ni kweli na hapa ni kuua soo maana sio ajabu hata mzee wa Msoga anaelewa mchezo gani anachezewa. Nilishangaa hata pale alipo kwama Airport kisa visa ni Msigwa huyo huyo aliyeingilia kutoa tamko kwa nini?
Ofisi kweli inaenda kama alivyosema Mwinyi, motokaa mbovu
 
Magu nahisi anatumia muda mwingi mitandaoni na kwenye tv kuangalia nani kamkashifu
Ushauri ; Afanye kazi aliyoomba haya mengine amwachie Nape
 
Nakumbuka hii habari niliiona front page kwenye gazeti la raia mwema na Zanzibar Leo kwamba " Mali za Salma kikwete kuuzwa kwa mnada" .
Naomba magazeti haya yachukuliwe hatua stahiki kwa kumchafua Kikwete na familia yake.
inawezekana ni ukweli zilitaka kuuzwa lakini baada ya kugundua ni za mama wa taifa zika... by the way nimeona the gurdian jpm kakanusha kukomalia mambo ya kodi ya kikwete
 
Je WAMA wanalipaga kodi au hawalipi..?

Kama wanalipa, basi sawa..✔✔✔✔✔✔

Kama hawalipi, nani kawapa Exemption..? kwa maslahi ya nani..? kodi kama hawalipi ni kosa kubwa kisheria, na hapo ndio nitaona double standards..!!

Je wanalipa au hawalipi KODI..? Swali ni hilo
 
View attachment 442591


TAARIFA KWA VYONIBO VYA HABARI


Katika siku za karibtmi baadhi ya wombo wa habari na mitandao ya kijamii imechapisha taarifa zinazomhusisha Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Mama Salma Kikwete naa Taasisi anayoiongoza ya Wanawanke na Maendeleo (WAMA) kwamba

imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoiingiza nchini na hiwo kuwa hatarini kupigwa mnada.
Taarifa hizo zimemhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa anahusika kuzuia mizigo hjyo bandarini mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

Tunapenda kuutalifu umma kuwa taarifa hizo sio kweli na ni uzushi, na Rais Magufuli hajawahi kuzuia wala kuagiza kuzuiwa kwa mizigo ya Mama Salma Kikwete.


Rais Magufuli amesikitishwa sana na uzushi huo unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake na amewataka waandishi wa habari na wombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake wazingatie weledi na kufuata sheria.


“Nimesikitishwa sana na uzushi unaofanywa dhidi ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete tafadhali mnaotengeneza uzushi huu muache mara moja, muacheni Rais mstaafu Kikwete apumzike''.


“Rais Mstaafu Kikwete amefanya makubwa kulitumikia taifa hili, amestaafu anampumzika, narudia muacheni apumzike, serikali haiwezi kuendelea kuvumilia uzushi na uchonganishi unaofanywa kwa makusudi kuwachafua viongozi wastaafu'' Ameonya Rais Magufuli

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam
O4 Desemba, 2016
Mmesema wenyewe,
-Kuna madudu mengi yaliyofanyika awmu iliyopita
-Kuna uozo mwingi uliofanyika
-Kuna makaburi hamuwezi kuyafukua kwani kuyafukia itakuwa shida
-Ngojeni kwanza tuinyooshe (kwa maana ya kuwa ilipinda
Sasa inakuwaje tena jamani mnaturudia wakati mlituamisha ya kuwa awamu iliyopita ilikuwa ilifanya makosa.
Naomba tu kurugenzi yako isijibu kila hoja kwani mnakaribishwa maswali zaidi kuliko kuweka hali sawa.
Jumatatu njema Mkurugenzi
 
Back
Top Bottom