Ikulu yakanusha kuhusu rais Kikwete kuongezewa muda wa utawala

Ikulu imekanusha mara ngap taarifa ambazo ni za kweli??!!
Bg dl lipumba athibitishe taarifa zake!

wewe ulitaka wafanye nini wakubaliane na lipumba kuwa kasema kweli ndipo ufulahi?,basi fanya hivi lipumba yuko sawa na ikulu haijasema kitu ili ulizike unavyotaka wewe.
 
Sasa lipumba aliongea na ikulu nao wameongea sasa tatizo liko wapi hivi watanzania mbona wa ajabu hivi wewe ukiongea sawa mwingine akiongea inakuwa nongwa hii jamii vipi hawa watu vipi.
 


5:38 PM
Ikulu


Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani”.

Katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa madarakani hadi mwaka 2017” kwa sababu kuna“wasiwasi kuwa mchakato wa sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof. Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi. Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango hiyo.

Taarifa hiyo imedokeza kuwa itakuwa ni vyema kwa Mheshimiwa Lipumba kuisaidia jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane.

Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.

Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu.
KUKANUSHA SI KUPO KWENYE LUGHA, Mimi sioni haja ya kukubaliana au kukataa hili swala maana lisemwalo lipo kama halipo linakuja. Let's wait and seee buddies!!
 
kp15052013.jpg

.....Mkuu dongo la ukweli hilo kwa jk.
Cc: Ritz
 
Ikulu wamejibu vizuri tu nadhani lipumba atakuwa ameridhika na hayo majibu au kama atakuwa kastaarabika zaidi anaweza kuweka sawa tamshi lake.
 
Siku mtu akikurupuka kwenye media na kusema rais kashikwa na tumbo la kuha.risha kwenye msafara ikamlazimu kuchepuka kichakani kujisitiri basi kurugenz ya habar watakuja na bonge la tamko la kukanusha.
 
Yaani akitaka ajue hawamtaki watu aitishw kura ya maoni lama hajapata kura 6
 
Sasa lipumba aliongea na ikulu nao wameongea sasa tatizo liko wapi hivi watanzania mbona wa ajabu hivi wewe ukiongea sawa mwingine akiongea inakuwa nongwa hii jamii vipi hawa watu vipi.

......silence is a weapon like other weapons.
 
Kwa wale vijana wa zamani (kizazi cha analojia) watakuwa wanakumbuka yale ya KOMANDOO lile la Zenj!!! Wale wapambe zake kutokana na kujawa hofu juu ya ulaji wao baada ya kumaliza muda wake, basi wakaanza ku-test public opinion kwa kupenyeza 'uzushi' ama 'udaku' kuwa hapakuwepo na mtu mwingine anayefaa kuhandle situation ya Zenj kuliko yeye kwa wakati ule, hivyo aongezewe muhula!! Duh kilichotokea baada ya hiyo test ni chapter katika historia ya politics za bongzenj. Kwa kifupi, 'udaku' ni njia mojawapo ya ku-test public opinion/response. Mshanifahamu?
 
Lipumba ana akili nyingi zaidi ya hao walioko huko magogoni, amewatega kwa ulimbo na wamenasa kwa kujitetea kwa tetesi tu!!!Kama sio kweli baba MwanaAsha amenogewa na anataka kuongeza ufalme wake kwanini waweweseke?
 
huyu lipumba sasa anakotupeleka siko na mtu mzima anapokuwa muongo ni hatali sana,aje akanushe basi

Sio kazi yake kukanusha, Aliyeshutumiwa ndiye anayetakiwa kukanusha kuwa kinachosemwa juu yake sio kweli. Ye ashamaliza kazi yake.
 
ina maana wakati mmemtuma akaseme hayo hamkumuandalia na ushaidi kabisa,

hii inaweza kuwa imefanyika kwa makubaliano ya Lipumba na JK ili kupima upepo si unajua tena wanategemea CHADEMA ife kabla ya uchaguzi, sasa wanaona mziki hata mafua hauna, na 2015 imefika, so wanahitaji muda zaidi ili waibomoe CHADEMA, so yanagonga yanarudi , teh teh tehh
 
kwanini Ikulu wanakimbilia kukanusha mapema?
bora wangekaa kimya kwanza wakajiridhisha
ikiwemo kumuita msemaji na kumtaka akanushe alichokisema mwenyewe
kwenye media kama ikigundulika hana ushahidi au kapotosha.
hii itajenga imani zaidi kuliko kuwahi kutoa makanusho.
 
Back
Top Bottom