ikulu yakanusha kuhusika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ikulu yakanusha kuhusika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jan 10, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ofisi ya rais ikulu imetoa ufafanuzi na kueleza ukweli uliopo na kukanusha uongo ulioandikwa kwenye gazeti moja la hapa nchini.
  Ikulu imeeleza kuwa haihusiki katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji na haitahusika kwa namna yoyote ile.
  imeviasa vyombo vya habari kuandika habari za ukweli badala ya kuandika habari za chuki na zinazopotosha jamii.

  Source.habari Tbc saa 2 na saa 4 usiku.
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ikulu haiwezi kukwepa lawama ya kutousika na uhalifu uliofanywa na viongozi ambao wako chini ya Rais na kitendo chake cha kukaa
  kimya na kutowachukulia hatua na kuwafumbia macho wahusika waliojigawia vitalu hivyo huku wakiwa na ushahidi wote ni msaada tosha toka ikulu hawaitaji msaada mwingine wowote kutoka ikulu. hii ni sawa na polisi kushuudia uhalifu ukifanywa mahala na yeye kukaa bila kuchukua hatua yeyote halafu baadaye anaulizwa kuhusu tukio hilo naye anajibu sikuhusika kwa kuwa tu hakumkaba yule mtu lakini kwa kitendo chake cha kutokuchukua hatua naye pia ameusika kwenye uhalifu kwa kuruhusu uhalifu kutokea huku akiwa na uwezo wa kuzuia.
   
Loading...