mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
Hivi mtu kugeuzwa mradi inakuwaje?ninachofahamu mimi ni kwamba kama kweli alishiriki basi aligeuzwa mradi maana waandaji walikuwa wanamtafuta mtu ambaye kuwepo kwake kungeongeza watu, hivyo rais aligeuzwa mradi kwa namna hiyo,We jiulize je umewahi kuona matamasha/sherehe anaalikwa mtu hohe hahe? ni laazima aalikwe mtu atayefanya tamasha lifane, hivyo hawa jamaa wa zinduka waliona raisi ndio anafaa hivyo wakamualika na kwa kupitia yeye tamasha likaongezwa uzito.Kwa hiyo hata wafadhili kwa kitendo cha kumualika rais laazima walitikisa vichwa wakaongeza imani kwenye mradi huo.sasa ikulu inakataa nini?.
Mheshimiwa Rais hajageuzwa mradi na mtu yoyote, na kwa kweli ni ukosefu wa heshima kudai kuwa Mheshimiwa Rais amegeuzwa mradi, na wala hakuna mchezo wowote mchafu uliokuwapo katika ushiriki wa Mheshimiwa Rais katika uzinduzi huu.
Mheshimiwa Rais alishiriki kama mgeni rasmi tu katika shughuli hiyo. Siyo yeye Mheshimiwa Rais ama Ikulu ilishiriki katika maandalizi ya uzinduzi huo kwa namna yoyote ile.