Ikulu yachachamaa habari ya Jk kugeuzwa mradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yachachamaa habari ya Jk kugeuzwa mradi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukwangule, Mar 11, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumesoma kwa mshangao na masikitiko makubwa habari iliyochapishwa jana, Jumatano, Machi 10, 2010, katika ukurasa wa kwanza wa Gazeti la Tanzania Daima chini ya kichwa cha habari “JK ageuzwa mradi”.

  Habari hiyo inahusu uzinduzi wa mpango kabambe wa kupambana na kutokomeza ugonjwa hatari wa malaria nchini, mpango unaoendeshwa chini ya kauli mbiu ya Zinduka – Malaria Haikubaliki.

  Kwenye habari hiyo, imedaiwa kuwa “watoto wa vigogo” wamemponza Rais kwa kujinufaisha binafsi kwenye mchakato wa maandalizi ya uzinduzi huo, na kwamba “mchezo mchafu” huo wa kujinufaisha ulianzia Ikulu wakati wa kumtafuta Mheshimiwa Rais Kikwete, ili ashiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye tamasha lililofanyika kwenye Viwanja vya Leader’s Club, Dar es Salaam, Februari 13, mwaka huu, 2010.

  Ikulu inapenda kusema kuwa habari hii ni ya uongo na uzushi wenye nia mbaya ya kuingiza jina la Mheshimiwa Rais na Ikulu ya wananchi katika jambo ambalo halikuwapo.

  Mheshimiwa Rais hajageuzwa mradi na mtu yoyote, na kwa kweli ni ukosefu wa heshima kudai kuwa Mheshimiwa Rais amegeuzwa mradi, na wala hakuna mchezo wowote mchafu uliokuwapo katika ushiriki wa Mheshimiwa Rais katika uzinduzi huu.

  Mheshimiwa Rais alishiriki kama mgeni rasmi tu katika shughuli hiyo. Siyo yeye Mheshimiwa Rais ama Ikulu ilishiriki katika maandalizi ya uzinduzi huo kwa namna yoyote ile.

  Tunapenda kufahamu kwamba mwaliko kwa Mheshimiwa Rais kushiriki kwenye shughuli ile ulikuwa ni wa Kiserikali, uliratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ndiyo iliyosimamia maandalizi yote ya shughuli hii, kwa kushirikiana na wabia wengine katika kampeni ya Zinduka – Malaria Haikubaliki.

  Mheshimiwa Rais alishiriki katika uzinduzi huu ikiwa ni sehemu ya Sera Muhimu ya Serikali yake ya kutaka kutokomeza ugonjwa wa malaria, ugonjwa unaoua Watanzania wengi kuliko ugonjwa mwingine wowote. Huu ni ugonjwa unaoua wastani wa Watanzania 291 kwa mwaka, sawa na wastani wa watu 10 kila saa moja, wengi wakiwa ni watoto na ndiyo maana Mheshimiwa Rais aliutangaza ugonjwa huo kuwa ni janga kubwa la taifa letu la Tanzania.

  Ni jambo la kusikitisha sana kwamba kampeni muhimu ya kupambana na muuaji mkubwa wa wananchi wa Tanzania, sasa imegeuzwa na watu wachache kuwa chanzo cha kutumbukiza jina la Mheshimiwa Rais na Ikulu katika madai yasiyokuwa na tija kwa wananchi wanaoendelea kusumbuliwa na kuuawa na ugonjwa huu.

  Ikulu inasikitishwa na vitendo vilivyoanza kujitokeza kwa baadhi ya watu kutumia jina la Rais na Ikulu kunogesha hoja zao, hata pale ambapo Mheshimiwa Rais wala Ikulu haihusiki. Watu hawa wachache ni lazima waache kufanya mchezo na nafasi ya Rais.

  Kama yupo mtu anayo maslahi yake katika mpango huu na uzinduzi wake basi asimhusishe Rais wa Jamhuri ya Tanzania au Ofisi ya Rais, Ikulu. Aidha, kama yapo matatizo ya mikataba baina ya wahusika katika uzinduzi wa kampeni hiyo, au kama kuna watu wanadaiana, wayamalize matatizo yao wenyewe bila kumhusisha Mheshimiwa Rais, Ikulu wala maofisa wa Ikulu.

  Ikulu pia inapenda kusisitiza kuwa maofisa wote wa Ikulu walioshiriki katika maandalizi ya uzinduzi huo, na kwenye uzinduzi wenyewe, walifanya hivyo kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kufanikisha shughuli hiyo, na wala si kwa kujinufaisha binafsi.
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  11 Machi, 2010
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kumbe maoni yetu yamewafikia walengwa,safi sana.
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kumbe ilikuwa ni tamasha na ilifanyika kwenye club!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Takwimu hazipo sahihi hizi!
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mkuu una makengeza nini,vaa miwani basiii

  ....ili ashiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye tamasha lililofanyika kwenye Viwanja vya Leader’s Club, Dar es Salaam, ..
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  kama kawaida naona wameanza 'kujikanyaga'!
   
 8. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  "Ikulu pia inapenda kusisitiza kuwa maofisa wote wa Ikulu walioshiriki katika maandalizi ya uzinduzi huo, na kwenye uzinduzi wenyewe, walifanya hivyo kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kufanikisha shughuli hiyo, na wala si kwa kujinufaisha binafsi"


  January hapo keshasafishika tena!
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Akina Ruge si walisema wanatafuta walinzi wa kumlinda rais???!!!! mbona watu waliskia hizi statement......
  Ikulu inabidi wawe wakali kuhusu haya mambo na sio kukurupuka ina maana tabia hii itaendelea.

  Swala la JK kuwa mradi hiyo kawaida sana, akienda mikoani vitenda vya hapa na pale kwenye ujio wake mbona watu wanatengeneza pesa.Ikulu, do some critical investigations

  Kama JK ni deal na anauzika, hamuoni nyie wengine mnaweza mkawa mashelves,mizani, ambazo zinatumika kutunza na ku-quantify bidhaa! hamna uwezo wa kusema lolote, nyie jiteteeni tu.

  Maumivu ya kichwa yanaanza taratibu......
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  basi.. next time mkae chini kusoma mnavyoandika. Kwa ufupi ni kuwa Ikulu na Rais Kikwete walihusika katika maandalizi hayo na kwa vile shughuli nzima ilikuwa ina viingilio kuna mtu ametengeneza fedha kwenye huo Mradi na uwepo wa Rais bila ya shaka ulichangia watu wengi kwenda (more money)..

  So.. Rais aligeuzwa mradi. Au mnataka tuwakumbushe na ya Arusha nako. Next time.. fikirieni vizuri mnapomhusisha Rais kwenye mambo mbalimbali.. wekeni principles ambazo zitafuatwa na kila shughuli inayotaka kutumia jina la Rais au Ikulu.

  One.. kama ni public basi hakuna kiingilio (mnaweza kuandaa utaratibu wa tiketi za bure tu ili kumudu watu watakaoingia ndani, kama ni ndani)
  Two.. Shughuli yoyote yenye lengo la kuchangisha fedha au faida ni lazima ijulikane wazi mapema na Ikulu na faida hiyo ijulikane mapema na inakwenda wapi!
  Three.. mkiboronga ombeni msamaha msijifanye kama mnaongoza Ufalme wa Jakaya Kikwete I
  Two...
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nashangaa ni kwanini wanajitetea na kulialia.lol.
   
 12. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Sawa, lakini huyo mtu (JYM?) keshavuta zake safi tu, kwa hiyo kwa huyo mtu JK ni mradi. Uzushi au uongo uko wapi? Ignorance is bliss!

  Kama Ikulu hawajui au wameingizwa mkenge, haina maana huo ni uongo au uzushi. Watu wametengeneza hela safi sana, na zingine bado zinakuja....kalaghabaho
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Inachekesha sana yaani kila uchwao utasikia Ikulu imechachamaa, JK amekasirika haijawahi tokea, Ikulu wanasema wote walioshiriki katika jambo hili hatua kali zitachukuliwa etc etc. Ngonjera tu Jakaya Kikwete na mwandishi wake banyamulenge sijui ni mtusi yule au Muhutu hawana agenda yoyote kwa Tanzania bali ni kwa manufaa yao binafsi. Ye akae pale asubiri siku zake kazi yake kubwa ni kukenua meno kama loafer flani hivi kazi ya uongozi haiwezi.

  Tunasubiri taarifa ya safari yake ijayo ughaibuni.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi hiyo hafla ilifanikiwa kiasi gani?
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  At least we know kwamba ikulu kuna jambo wanweza... nalo ni kuchachamalia ushabiki!! Pia tunajua wapi wanshindwa, ni kushughulikia shida za watz

  Hate it when they release matamko ya udaku wanaacha watu wa kigoma hawana reli na wateja wa NBC bila huduma
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  Naona unatafuta ugomvi mwingine!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  yeah.. maana wameandika kwa kireeeefu lakini wameshindwa kusema kama hafla hiyo ilifanikiwa au vipi.. halafu mbona sijasikia zinduka nyingine.. au ndio ukishazinduka unaruhusiwa kuzimia tena?
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimesoma tamko la Januari Makamba kupitia mwamvuli wa IKULU (kabla gazeti halijaenda mitamboni) akikanusha kumzunguka SUGU. sasa naamini JYM ni mwanafunzi aliyefaulu vyema wa RA.

  Hii ni dalili ya wazi kwamba muungwana amechoka na anasaka cheap promo bonanza kupitia eventz zilizo chini sana ya protokali ya ofisi yake.

  wamewalipisha viingilio watu pale leader's club lakini bado akina mama kule amana wanajifungua na kurudi home bila hata ya uwezo wa kununua net iliyolipiwa na hati punguzo..... Naona EL ana wanafunzi mafisadi wengi kweli
   
 19. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hii ni aibu sana!!!
  inasemekana wale waliotoa kiingilio (walalahoi), hawakuambulia hata hiyo net, na wale ambao waliitwa VIPs wakapewa net bure, japo ni surplus to requirements kama kweli wanatumia..
  Hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo!!
   
 20. T

  Tuntufye New Member

  #20
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Each one of us, and, indeed, all those who aspire to national leadership must bring their own visions, views and styles to the business of reforming Tanzania, and the search for solutions."


   
Loading...