Ikulu yaandaa habari kuchafua wabunge wa CHADEMA

Tunawangoja mtaani kwa wananchi, tena waliopigika ambao wakisikia mbunge anatafuna mihela yote hiyo na hajawahi kupata panadol dispensary, ndo wataeleza vizuri
 
Wewe wa news room hebu tupe heading kwenye gazeti lako bana, au kama vipi weka taarifa nzima ilivyoandikwa
 
Chadema na wabunge wote ebu tumieni akili::

Kwanza watu wamesigm kuwa wamehudhuria bunge, sasa utawalaumu vipi, wakati taratibu ndio hizo. Halafu Chadema wanataka sheria ibadilishwe, ili POSHO ZIFUTWE?? WHAT IS SO WRONG WITH THAT??

Kwa sababu posho ziko tied up na mahudhurio, kila mbunge achukue posho, na baada ya kiako cha bunge posho yote Sitting allowance itolewe kama msaada kwenye majimbo yanayoongozwa na yenye wabunge wa chadema.

Chadema, waeleze umma kuwa wanachopinga sio tu SITTING ALLOWANCE KWA WABUNGE, BALI SITTING ALLOWANCE ZOTE NCHINI PERIOD.

Sasa hivi mafisadi wa serikali kuanzia IKULU, wizarani na kila mahali wanaogopa kwani hapa ndipo wanakopata hela za bure kwa vikao vya kipuuzi.
 
Leo majira ya mchana tukiwa News room kuna taarifa ambayo imeandikwa na imesambazwa kwa wahariri ikiwa na lengo la kuwachafua wabunge wa CHADEMA kesho kuhusiana na posho.Taarifa hiyo imetolewa baada ya Ikulu kulitaka Bunge liwapelekee mahudhurio ya wabunge wote waliosaini kwenye orodha ya mahudhurio na imetumika hiyo kwa kuangalia ni wabunge gani wa CHADEMA waliweza kushiriki kwenye vikao na hivyo kusema kuwa ni orodha ya kupokea posho.
posho.png
Habari hiyo itakuwa ndiyo front page kwenye magazeti mbalimbali kesho na lengo ni kuhakikisha kuwa walau wanapumua ili suala la posho wananchi waone kuwa limekigawa CHADEMA kati ya wabunge wake.Naomba kuishia hapo kwa sasa kwani ndio tunakimbizana na deadline, ntarejea baadae kuwajuza na nikiweza nitaiscan taarifa hiyo na kuiweka hapa jamvini.
.Ina maana bunge la Makinda limeshapoteza hadhi kiasi cha serikali(ikulu) kulisimamia kwa kuliagiza?Mama achia ngazi haraka, kwa sababu sasa imedhihirika hujui mamlaka ya bunge, wala wajibu wako.Kama bunge limefikia mahali ambapo linaagizwa na serikali, basi mimi sina tena sababu ya kujizuia kujitundika kwa kamba ya katani. Nnayo ndani tayari, ila nasubiri kuona agizo likitekelezwa..
 
Utawala wa muda mrefu uwe wa mtu mmoja, ukoo, kabila au chama unapofikia kikomo unatapatapa. Siku zote watala wa muda mrefu hulewa utawala na madaraka. CCM wamelewa, hii imetokana na kukaa madarakani muda mrefu kupindukia. mwisho wao umefika hawana jinsi,hawana namna tena.
 
Najua vle vjingazet mshezi vtafanya hvyo ila c mwananchi na tanzania daima.
 
mwenye mbinu za kijinga kama hizi nadhani si wingine bali ni yule mzee mwenye sura ya ny...... PR wa magogoni.

Hii ni mbinu ya kitoto, magazeti kuleni hizo hela za wajinga ndo waliwao.

Mzingo wa miwa wa mjinga huishia mabegani.
 
kama wamekataa kuzipeleka palipotakiwa na wabunge kama KDI sasa wabunge watazipeleka kwa mikono yao, hatuwezi kuwaachia NGURUWE shamba kamwe.
 
Sasa lengo ni kuwaaminisha wananchi CDM ni wanafiki au ni vipi?.....kwa sababu kwa mujibu wa spika hiyo ni orodha ya mahudhurio ambayo kila mbunge anapaswa kuisaini.....kweli Magamba maji yamewafika shingoni.
 
Ndiyo maana mimi nawashangaa na nitaendelea kuwashangaa wote wale wanaoendelea kuweka matumaini yao kwa hiki chama, CCM. Jamani Watanzania hata kama ni upofu wa kutoona mbali lakini hii hali sasa inatisha, serikali hii si ya wananchi tena na taifa limetekwa nyara na genge la wahuni. Samahani ndugu zangu lakini hakuna namna ya kuweza kuuita huu utawala chini ya Kikwete zaidi ya utawala haramu unaodumu kiujanjaujanja bila kujali sheria wala kutoa haki kwa raia.

Kinachonisikitisha kuliko yote ni kuwa kama hata humu kwenye jamvi la JF wanapatikana watu wanaoishabikia, sasa hali ikoje huko kwingineko ambako habari hazifiki - kweli mtaji wa CCM ni ujinga, umasikini na maradhi ya wananchi ! Hii ndio sababu kwa sasa serikali ya CCM iko tayari kupiga na hata kuua mradi wanabaki madarakani hata kama taifa linateketea. Hata hivyo imekula kwao kwani mbinu wanazozitumia zinawasaliti kwa sababu kama ilivyotegemewa, zinapangwa kijinga.

Siku zote huwa naichukia CCM lakini hii imezidisha machungu yangu. I cannot wait kesho asubuhi nikiikuta habari hii kwenye front page, kwa kweli itaniuma sana. Mkuu nakubaliana na wewe asilimia 200. Mtaji wa CCM ni ujinga wetu na zaidi ni Umasikini wa Watanzania, ndo maana hawawezi kupambana kutoa umasikini. Wanapata kura kwa kugawa kofia, fulana na kanga. Mungu tusaidie hii ni kali.
 
CCM are the gates of hell, but they shall never prevail, wameipa nchi umasikini wa kuitosha hawana aibu, ni wezi tena wasio na haya. Wana ukosefu wa kinga rohoni ndio maana nchi imekuwa vulnerable.
 
All right, tunasubiri hiyo taarifa itakayoandikwa kwenye Magazeti ya Uhuru na Mzalendo kesho!
 
Haya ndiyo madhara ya watu kuwa madarakani bila kustahili. Ikulu ya aina hii ni aibu kwa watanzania wote. Wengine tunafarijika tu kuwa hatukushiriki kuwaweka madarakani, lakini tunaathiriwa na kila uchafu wanaoufanya. Kwa trend hii, itafika wakati wetu watatusulubu kwa masahibu tuliyowaachia!
 
nionavyo miaka hii mitano tanzania hatutakuwa na maendeleo maana wanasiasa wa upinzani na chama tawala kazi ni kurumbana, na kutafutiana visa. hii ni hatari kwa maendeleo yetu, kweli wana siasa ndiyo nguzo ya kurudisha nyuma maendeleo
 
Back
Top Bottom