Ikulu yaahirisha Press Conference

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
612
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tarehe 01 Julai, 2008 siku ya Jumanne tunatoa taarifa ya kuahirisha Press Conference
mpaka hapo mtakapo taarifiwa vinginevyo. Upatapo ujumbe huu naomba utoe taarifa kwa
yeyote anayehusika.

Ahsante na Kazi Njema.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
ikulu,
DAR ES SALAAM.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tarehe 01 Julai, 2008 siku ya Jumanne tunatoa taarifa ya kuahirisha Press Conference
mpaka hapo mtakapo taarifiwa vinginevyo. Upatapo ujumbe huu naomba utoe taarifa kwa
yeyote anayehusika.

Ahsante na Kazi Njema.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
ikulu,
DAR ES SALAAM.
Hivi utaratibu wa Rais Kuzungumza kila Mwisho wa Mwezi umeishia wapi?Au Salva naye yuko Misri
 
Hii ni kurugenzi ya propoganda tu na hakuna lolote la maana hata wakitaka kuzungumza nanyi waandishi watataka kutumia propoganda zao tu kuonyesha mambo ni shwari wakati nchi iko katika msukosuko wa ufisadi.
 
Mambo ya aibu sana!! Hamna tamko rasmi lolote linalotoka Ikulu...utafikiri wako likizo! Hii inaonyesha nchi tunaweza kuiendesha wananchi wenyewe...huku JF tuendelezr mapambano by the time they get back, watakuta mpaka ofisi zao tumeshazikalia wenye uchungu na nchi!!
 
Acha tu waendelee kuahirisha matatizo,iposiku hayo matatizo yataibuka yenyewe mitaani
 
Thanks for this information, at least we know hakuna press
 
Jamani tuna akhirisha hiyo Press Conference bila ya kutuwa ni kwa sababu gani imeakhirishwa. Kwa hivyo Mkurugenzi huyo wa IKULU hana jambo lolote la kusema. Haya ndiyo mambo ya Tanzania na serikali yetu hii. Kila kitu ni siri na siri inapofichuka basi inakuwa ni mzozo wa Richmond,BOT au EPA.

Kwa nini Mkurugenzi huyu hakuweza kusema ukweli na ndio kitu ambacho kinatakiwa kutoka IKULU.

Ni kweli rais J.Kikwete yuko kwenye mkutano Egypt. Basi yale mazungumzo yake ya kila mwisho wa mwezi yangeliweza kutolewa na makamo wa rais kwa niaba yake.

Huu ni upotovu wa good governance and administration.
Dr.khamis
 
Nafikiri hawana la kuongea maana rais yupo likizo mpaka tuhuma za ufisadi zififie
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom