IKULU yaagiza uchunguzi watendaji wizarani, taasisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IKULU yaagiza uchunguzi watendaji wizarani, taasisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  FidelisButahe IKULU imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kuwachunguza watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndio chanzo cha mawaziri wao kuwajibishwa.

  Hii ni kauli ya kwanza ya Ikulu, tangu Rais Jakaya Kikwete afanye mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri kwa kuwaondoa mawaziri sita ambao wizara zao zilitajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabiliwa na kashfa ya ufisadi na matumizi mabaya yafedha za umma.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue juzi aliliambia Mwananchi kuwa tuhuma zote ambazo zilibainishwa katika ripoti ya CAG katika maeneo mbalimbali sasa zitachunguzwa na Takukuru pamoja na DCI. "Tuhuma zote zitapitiwa na vyombo husika (Takukuru na DCI), kitakachofanyika ni kuzipitia tuhuma zote ili kuwatambua wahusika sahihi," alisema Balozi Sefue. Alifafanua kwamba uchunguzi huo unafanyika ili kuhakikisha kuwa uamuzi utakaotolewa haumuonei mtendaji yoyote. "Tutachunguza na watakaobainika watakachukuliwa hatua za kinidhamu au kufikishwa mahakamani,"alisema Sefue na kuongeza:

  "Baada ya Takukuru na DCI kumaliza kazi yao taarifa watakazozitoa zitakwenda kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka), ili kuona kama jambo lililobainika linaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kupelekwa mahakamani." Balozi Sefue alisisitiza kwamba inafanyika hivyo ili, kuhakikisha hakuna mtendaji yoyote atakayeonewa na pia hawataki mwenye makosa aponyoke. Aliwataka watumishi na watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma kufanya kazi kwa kukumbuka mambo mawili, ambayo ni kutambua kuwa wameajiriwa kwa ajili ya Watanzania na kuzingatia maadili ya kazi.

  "Wakitekeleza hayo mawili mambo yanakuwa mazuri zaidi…, mtumishi anatakiwa kutambua kuwa kaajiriwa na wananchi hivyo anatakiwa kujituma na kuzingatia maadili ya kazi," alisisitiza Balozi Sefue. Hata hivyo, imewatoa hofu watendaji wote nchini kwa kuwataka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kukumbuka kuwa wapo kazini kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania na si vinginevyo.

  Asifia uwazi Balozi Sefue alisema sio kweli kuwa hivi sasa vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma vimeongezeka bali hali hiyo inaonekana zaidi kwa sasa kwa kuwa Serikali imekuwa ikifanya mambo yake kwa uwazi mkubwa. "Hivi sasa ripoti mbalimbali zinawekwa wazi bungeni na wabunge wanachangia, ripoti haziwekwi tena kabatini na hiyo ndio sababu, sio kweli kuwa matukio ya ubadhirifu yameongezeka kwa sasa," alifafanua Balozi Sefue. Kauli ya balozi Sefue inakuja wakati tayari CAG , Ludovick Utouh amewaonya mawaziri wapya na watendaji serikalini kwamba ripoti zake hivi sasa zina nguvu za kusimamia uwajibikaji hivyo, wanapaswa kusimamia vema wizara zao kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.

  Utouh alisema mawaziri wanapaswa kufahamu kuanzia sasa hadi mwaka 2015 zitatoka ripoti nyingine tatu, hivyo ni vyema wakachukua tahadhari kama wasimamizi wakuu wa shughuli za wizara.

  Utouh alisema kilichotokea bungeni na hadi kufikia mawaziri kuwajibishwa, imethibitisha kuwa sasa kutakuwa na uwajibikaji mkubwa utakaosababishwa na ripoti zake kama watendaji wasipofuata taratibu za Serikali. Wakati akitangaza mabadiliko ya mawziri, Rais Kikwete alisema baada ya mawaziri kuwajibika kisiasa, wanaofuta ni watendaji katika wizara na taasisi nyingine za umma ambao ndiyo chanzo cha mawaziri hao kujiuzulu.

  Alisema mawaziri wamekuwa wakijiuzulu hata kwa makosa ambayo si yao na kwamba hivi sasa Serikali itaanza kuchukua hatua kwa watendaji wakiwamo makatibu wakuu, wakurugenzi wa wizara, watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma pamoja na bodi za mashirika husika.

  Mawaziri waliowajibishwa kutokana na matokeo ya ripoti ya CAG ni William Ngeleja (Nishati na Madini), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Omar Nundu (Uchukuzi), Mustafa Mkulo (Fedha), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara). Naibu Mawaziri waliokubwa pia na panga hilo ni Dk Lucy Nkya, (Afya) na Athuman Mfutakamba (Uchukuzi).


  CHANZO: IKULU yaagiza uchunguzi watendaji wizarani, taasisi
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna haja gani ya kufanya uchunguzi wakati ripoti ya CAG ilishamaliza wanataka kutafuna hela yetu ya kodi tu yamenenepeana yameisha kuwa Kama kiti moto bado yanatukamua tu 2015-2012=3 mtakoma
   
 3. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MziziMkavu

  Tangu JK ahamie Magogoni umefanyika uchunguzi feki (Cosmetics) na hakuna hata kunguni aliyekufa pamoja na hizo tume kutafuna billions of money. Juzi tu Jairo ambaye ni master mind of the Jakaya Project alilewa akakwapua millions na Bunge lisilokuwa na meno likatingisha kiberiti likakuta kimejaa na Hadi Leo David Kitundu Jairo bado yuko kwenye Payroll ya Rostam na ya Serikali ya Kikwete thubutu mtu amguse hakuna cha Hosea, Feleshi, Mwema, Manumba hata Sefue anayeweza kutenganisha Jakaya na mwanadani wake Jairo.

  What ever you wish it's just a day dream. Hao wakuchunguzwa aliwateua mwenyewe JK of course kwa maagizo ya Rostam Aziz. "If wishes were horses even the poor could ride one "

  Kila mkurugenzi wa taasisi unayemwona aliwekwa hapo alipo na mfumo mbovu uliokuwepo wa Serikali ya CCM of course the system ilimchambua hata Kama Rais alipewa mapungufu Yao lakini ndiye aliyeamua wapewe madaraka kwa hiyo the same level haiwezi kuagiza wachunguzwe.

  Kama hakuwachunguza akina Mkulo watao pesa how comes wachunguzwe hawa? What is so special just fuata mziki dawa ni kuwaondoa tuanzie hapo after all nobody is indispensable. Kwa kauli ya Kikwete hakuna mtu aliyezaliwa kuwa Waziri/Mkurugenzi au Katibu Mkuu.

  Think loudly if one dies what happens. Kuagiza uchunguzi ni kupoteza muda but pia ni kuwapa nafasi ya kuwahonga wachunguzi. Akina Mwema na Mnyika walichunguza EPA and today they are more rich just do your homework! Hadi Leo ripoti ya uchunguzi hajawahi kusomwa hadharani and it's a closed subject...Remember Richmond> Dowans> Symbion and now the Baby Aggreko > sheria ya Madini> Meremetas etc,etc,etc....... You can go up to what in calculus they call infinity!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hawa watu wana matatizo; hadi Ikulu iagize?
   
 5. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sijaona kauli ya mtu kusimamishwa kazi, watachunguzwa wakiwa ofisini kwao!! What a fair investigation!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Kauli hii inamaanisha mamalaka zote za kupambana na uhalifu zimefumbatwa mkononi mwa JK pale Magogoni kwa lengo la kupunguza mgongano wa maslahi hasa kutokana na ukweli kuwa wateule wengi wa JK wamepewa pia kazi ya kutunisha mfuko binafsi wa JK kwa kutumia nyadhifa zao. Uthibitisho ni wale mawaziri walioboronga kukataa kujiuzulu.

  Naam walijua ikulu ndo mambo yote. Eloi eloi lamasabaktan!!!!!
   
 7. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ina maana Takukuru, Polisi hawana nguvu ya kufanya kazi mpaka iagize ikulu?

  what a ****!! Huyu kibaka Hosea na Said Mwema kazi yao ni nini haswa, Je ikiwa ikulu kuna mtuhumiwa anahitajika kwenda lupango hii inaonyesha ikulu ikigoma asichukuliwe hata chukuliwa sasa.

  Hii nchi haijakaa sawa kabisa Chadema hebu chukueni nchi tufute miaka 50 tuanze ukombozi na uhuru upya kabisa.
   
 8. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umeonaeeeeh! Ni njia ya kuwasafisha
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kila siku wanasubiri waagizwe na hata wakiagizwa wanakuja na taarifa za kubumba - kumbuka taarifa ya Takukuru juu ya Richmond - Hivi kuna haja ya kuwa nao?
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzee Mwanakijiji hawako huru.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Precise pangolin report ya CAG haiwezi kuwa conclusive kuwashitaki watu mahakamani. DCI na PCCB ndio wana dhima ya kufanya uchunguzi wa kipelelezi ili kukusanya ushahidi wa kuweza kuwafikisha mahakamani watuhumiwa. Report ya CAG inaweza kuwa sehemu ya ushahidi. Mkuu pia ukisoma report za ukaguzi utagundua kwamba huwa hazisemi directly kwamba kuna wizi bali huwa zinatilia mashaka mashaka; hivyo ni vyema uchunguzi wa kiupelelezi ukafanyika.

  Lakini mkuu pia usije kushangaa wanatakaswa kwa kukosekana ushahidi wa moja kwa moja wa kuwatia hatiani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. J

  JIS Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Ningekuwa CAG ningeachia ngazi. Wewe unafanya kazi nzuri halafu aje mtu mwingine kuchunguza nini? Nimeamini hakuna mtendaji yeyote atakayewajibishwa, labda kuhamishiwa sehemu nyingine. Au yawezekana yale madudu yalifanywa na mawaziri waliowajibishwa, watendaji walifanya kwa shinikizo lao!!! Tusiseme sana, tungoje uchunguzi ufanyike tuone matokeo yake.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Ukisikiaga maagizo utumbo ndiyo haya!. Kama ripoti ya CAG ilipotoka tuu ilishaonyesha madudu yote, hao Takukuru na DCI walikuwa wanasubiri nini kutimiza wajibu wao?. Ukisikia incompetence at higher level ndio hii na JK anasubiri kama wabunge watawaka ndipo achukue hatua!.

  Ningekuwa ndio mimi JK ningewaita Hosea na Mwema na kuwauliza tangu ripoti imetoka mmefanya nini?. Wakisema walikuwa wanasubiri maagizo!, just fire them on the spot!. Wanasubiri maagizo kutekeleza majukumu yao!.

  I'm sick!.
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wamepewa hizo nafasi kama fadhila hivyo hata kwenye utendaji ni lazima wasubiri maelekezo ya aliyewafadhili
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo la nchi yetu ni uchunguzi. Cag ameshatoa ripoti lakini tunatakiwa kuchunguza tena. Sasa sijui wanachunguza ripoti ya cag au wanaanza upya. Na sijui huo uchunguzi utakamilika lini maana kila mahali uchunguzi haujakamilika. Polisi, Mahakamani, kwenye halmashauri, kila mahali uchunguzi haujakamilika.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hukumbuki wikileaks walishasema kuwa Dr Oseah anashindwa kuwagusa watu flan koz ya mamlaka kuu,,,pamoja na na hayo inaonekana IKULU imeumia sana baada ya mawazir kutemwa,mbona alipoondoka Lowasa,Karamagi na ;msabaha ikulu haikuagiza UCHUNGUZI
   
 17. MAWAZO UJENZI

  MAWAZO UJENZI JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 1,727
  Likes Received: 622
  Trophy Points: 280
  Kuna mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Magu Mwanza anaitwa Colnel Ngudungi ametafuna Bilion 17,had kamati ya bunge hesabu za selikari za mitaa inayoongozwa na Mrema ilikataa hesabu zake but had leo hii anakula bata ofisini,kwa nini asipandishwe kwa pilato?
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wangekuwa mbuzi ama ng'ombe pasaka ya juzi tushamaliza habari yao na matatizo kama haya yasingelikuwepo tena sasa
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wakuu wakati tunachangia hii thread pia naomba muwe mnapitia hapa http://www.nao.go.tz/files/Central%20Government-General%20Audit%20report.pdf ili kupata hizo report za CAG na kuzisoma na kuzitafakari. Manake nimeshituka kusiakia naibu waziri mmoja akisema watendaji ambao mashirika/idara zao zimepata hati chafu ama yenye mashaka wachukuliwe hatua za kisheria!

  Wakuu tukubaliane kwamba kuwa na hati chafu hakumaaninishi kwamba kwa uhakika kabisa kuna UBADHIRIFU ama WIZI kwenye idara yako vivyo hivyo kuwa na hati Safi hakumaanishi kwamba kwa uhakika kabisa hakuna UBADHIRIFU ama wizi kwenye idara yako! Mtapiga kelele lakini ndivyo ilivyo.

  Au http://www.nao.go.tz/reports.php?start=0
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Zote ulizotaja hapo ni sifa za viongozi wa Tz na nyinginezo nyingi they conduct research without coming with answers or solution so why conduct the research? Wabongo wanakuambia ni kupigwa changa lama macho haya bwana jk umefanikiwa kutupiga changa la macho kwa mambo zaidi ya 10 ambayo yanamkandamiza na kumwibia Mtz na sasa tunachokingojea ni aibu yako/ uumbuke kwa haya mabaya yote uliyotutendea watanzani! Namini siku zote mwisho wa ubaya ni aibu na sasa ndicho kinakungoja
   
Loading...