Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,836
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu Bw. Salva Rweyemamu ameviasa vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kushabikia uchawi kwani vinaweza kutishia wafadhili ambao wanaweza kuwa na wasiwasi na "usalama wa nchi".
Bw. Rweyemamu amesema kuwa Idara yake imepokea malalamiko ya watu wengi ambao wametaka vyombo hivyo vichukuliwe hatua ya kisheria kwa kushabikia mambo ya kichawi kinyume na sheria.
Mausia hayo ya Bw. Rweyemamu yanakuja siku chacha baada ya Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge kudaiwa kuwanga katika ukumbi wa Bunge na kufanya mambo ya kishirikina. Hata hivyo haijajulikana kama serikali ina mpango wa kutumia sheria ya mambo ya uchawi dhidi ya waandishi.
KLHN itaendelea kuandika habari zozote zenye maslahi kwa Watanzania bila kuogopa, kupendelea au kuona aibu. KLHN inatoa usia kwa Ikulu na viongozi wanaoshabikia uchawi kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji kuacha kufanya hivyo ili wasije kuandikwa. Usia huo wa Ikulu unawahusu watu wa nyumbani mwao na waandishi wao.
M. M.