Ikulu vs Gazeti la Mwananchi: JK akana kuwasamehe waliomuua Lut Jen Kombe

Hawa masaburi kweli mmeacha kuwatoa Babu na wanae mmekuja ukuwatoa wauaji walio hukumia kifo kwa tuhuma nzito zenye fitna na usaliti mkubwa juu ya mkuu wao,yote coz Imran alikuwa na mchapa kazi mwenye msimamo,hakuna asiye mjua kwa misimamo ya haki mkuu yule,kila aliyesikia kuwa amefariki alisakitikaa,hawa jamaaa miaka 16 tu wametolewa daaaah serikali yetu nomaaa,iba kuku au gombana na jirani yk mwenye wadhifha wwt srknl utafungwa hadi kufa,walio uwa kwa makusudi watatolewa,tumesha wajua,kombe tulimpenda na tutaendea kumkumbuka daima.damu yk haita enda bure.
 
Naomba kuuliza kama sie yy aliyetoa msamaha na anaona sio sahihi kwa watuhumiwa kupunguziwa adhabu, akiwa kama Rais hawezi kutoa tamko la kuendeleza adhabu hiyo?
 
Sasa ndo naamini kulikuwa na mkono wa mtu kwenye mauwaji ya Kombe.Siku ccm ikiondolewa madarakani,basi tutajuwa mengi sana.Ukweli ni kwamba it will be chaotic to some extent watu wakijuwa how deeply bad these people are.

Hilo ndilo linasababisha hawa jamaa watumie nguvu hata ile ya mkiani kuhakikisha wanaendelea kuimiliki ikulu...Wataendelea kutumia nguvu hadi lini, hilo ndilo ambalo hawataki kulisikia hata baada ya kuangalia kinachoendelea huko kwingine (Misri, Libya, Tunisia n.k)!!
 
Hili tamko kiboko. Shida ya hili tamko ni kusafisha Kikwete basi hakuna lingine, kuwa mambo yote yalifanyika wakati yeye hajaingia madarakani.

Kweli kama ni hasara Tanzania ilipata basi ni kumchagua Kikwete kuwa Rais wa nchni hii kama si Kikwete kumchangua Salva kuwa MC wake yaani msema chochote wa kutokea Ikulu.

Kama Mkapa hafai ikuwaje Kikwete amuchie kampeni za Igunga?
 
Basi itapigwa dana dana mpaka watazamaji tusahau!

Natumaini mwandishi/mhariri wa Mwananchi hataiachia hii habari
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Mwananchi, matoleo ya jana, Jumatano, Oktoba 12 na leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.

Gazeti hili limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungo cha miaka miwili.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
13 Oktoba, 2011

Kama sio Kikwete aliye waachia huru ni nani mwingine?
 
Serikali ni ya nani? Kikwete kama binafsi? CCM? Haina uhakika na maamuzi yake mpaka inashindwa kusimamia hoja yake?
 
Ila pamoja na yote kuna maswali ya kujiuliza juu ya hili gazeti..,kwa ninavyofahamu mimi ni kuwa chombo chochote cha habari kinakuwa na dhumuni ama madhumuni juu ya kuundwa kwake..,ukiacha kule kufikisha habari kwake lakini muundaji wa chombo hicho huwa na dhumuni binafsi la msingi, hivi ndivyo ilivyo duniani kote..,SASA LABDA NIJIULIZE BINAFSI LENGO LA MWANANCHI NI LIPI KWA KUANDIKA HAYA..?

Lengo ni kutujuza umma juu ya mambo yanayoendelea nchini mwetu. Utawala wa ccm hauna ujasiri wa kusimamia sheria!
 
Naomba kuuliza kama sie yy aliyetoa msamaha na anaona sio sahihi kwa watuhumiwa kupunguziwa adhabu, akiwa kama Rais hawezi kutoa tamko la kuendeleza adhabu hiyo?
Yeye hajasema lolote kuhusu msamaha umetolewa au haujatolewa, wala hajasema lolote kuhusu anona au haoni ni sahihi, kasema, moja, yeye hajagusa issue ya hao wauaji, mbili, maamuzi yote (hukumu au chochote kile) yalitolewa kabla ya 2005 alipoingia madarakani.
 
so its true that these criminals are out? Mkapa na kikwete one day they shall answer to this criminal acts they are perpectuating. its unfortunately that our government has gone insane and wild killing innocent civillians and protect killers. One day yes.
 
Jk never fails to amuse me................................kama waliachiwa kabla ya yeye kuchaguliwa mwaka 2005............................inakuwaje wakae jela miaka yote hadi Mei 2011? Ni kitu gani kilizuia wasiachiwe mwaka 2005 au kabla ya hapo?

JK ndiye alidai maamuzi ya ujenzi wa hoteli za Kempinski yalifayika kabla hajaingia Ikulu ila utekelezaji wake ulifayika wakati wa kipindi chake................hivi jambo kama ni baya ukikaa kimya au kulishabikia unatofauti gani na wale waliofanya huo uhalifu?

Aliye karibu na JK amshauri asome 2 John 1: 10-11 "If anyone comes to you and does not bring this doctrine, do not receive him into your house nor greet him,"

"For he who greets him shares in his evil deeds."


tatizo kubwa la msamaha huu ni kuwa umebariki -extra-judicial killings carried under gratuitous use of force..............na hawa wauaji hawakukaa hata miaka kumi jela ili kuonyesha ya kuwa wamejutia walichokifanya........................msamaha huu unanuka harufu kali ya kuwa ni serikali ya ccm ndiyo iliyomwuua Gen. Kombe na kosa lake lilikuwa anaombeleza na Chadema....................wabaya wake waliona ya kuwa wamtoe roho.......kama walivyomkolimba Sokoine na Kolimba among other of TZ former luminaries..........
 
kama msamaha ulitolewa wakati wa utawala wa mkapa si tayari wangekua wameshatoka? mkapa kastaafu 2005 iweje wakae mpaka leo?
hakuna kudangnanyana, kikwete ndio kawasamehe, kama sio yeye mkurugenzi alishitaki gazeti la Mwananchi tuone...
 
sasa kweli kuna mambo hapao! maamuzi yalifanyika kabla JK hajaingia ikulu, lakini kwa mujibu wa Mwananchi walitoka May 2011! hapo sasa habari gongana hapa
 
Tuwekeeni mapungufu yote ya ben hapa, vinginevyo litatokea gazeti lingine na tutarudia hayahaya! Just thinking...
 
hao jamaa wameachiwa kuja kufanya kazi maalumu!! watch out.
Kumbuka taarifa iliyokwisha tolewa humu jamvini kuhusu njama za kuuwawa watu muhimu ambao wanaonekana ni tishio kwa CCM. Hapa kuna jambo yawezekana kabisa watakuwa mitaani on mission wakimaliza kazi yao wanarudi nyumbani kwao. Makamanda wa Chadema kuweni makini, tuko pamoja katika kuleta mapinduzi ya kweli Tanzania.
 
Mwananchi hii watuambie vizuri hii habari waliipata: wanashindwa kuandika za msingi kama ''Mauaji ya Igunga'' wanatuletea habari zilizochakachuliwa: lakini pia hao waliokamusha inabidi watuambie wenyewe kama wenyewe nafasi yao ni hipi ktk hii skendo!
 
tunajua kuwa serikali ya tanzania imua kombe kwa makusudi kwa sababu za kisiasa. Sasa kikwete anataka kuonyesha kuwa hakuhusika na mipango ya mauaji hayo bali mkapa ndiye alihusika.
 
KIKWETE AJIBU KWENYE TWITTER NA FB sehemu ambayo ndo ameifanya ya kuwasiliana na wananchi utadhani kila mtu anamiliki kompyuta.Mambo anayoandika huko huwa hayana mantiki zaidi ya kujionyesha kuwa ni mjanja kumbe Big Zero!!!
 
Wakati fulani nilikuwa natamani kupata kazi kazi katika Kurugenzi ya habari ya Ikulu lakini kwa mwendelezo wa matamko yanayo yatoa kila kukicha mimi hamu sina tena. Nadhani hata wale jamaa wanaosomea uwanahabari pale Times kwa miezi 3 au 6 wanauwezo mkubwa wa kujibu hoja kuliko kundi hili la Rweyemamu na maamuma wenzake. Kwa kweli hiki kikundi cha kiduku ni kiboko katika kujibu hoja. Taarifa haina kichwa wala miguu yaani kama majibizano ya wambea mitaani. Kama ni kusema Kikwete hausiki basi mtajeni ni nani aliyehusika na huo msamaha. Kama hao jamaa walisamehewa mwaka 2005 Disemba kwanini waachiwe agosti 2011 (miaka 6 baadae?). Kwanini wale walioachiwa waseme wanamshukuru Mh. Rais Kikwete kwa msamaha wakati waliachiwa na Mkapa? wazee wa kiduku kuweni makini na majibu yasiyo na kichwa wala miguu. Pia suala la Rais kutoa msamaha lipo kisheria na lipo kwenye Katiba yetu kwahiyo kusaini mtu kunyongwa au kupunguza adhabu siyo kituambacho kinapingana na majukumu ya Rais. Na rais husaini baada ya kushauriwa na jopo la wataalam kufanya hivyo au lah. Maelezo yenu yanamfanya rais aonekane kama vile amevunja Katiba wakati ni suala la kawaida kabisa. Kama kazi imewashinda bora mkae kimya tu kuliko kutufanya wooote tuliosomea taaluma hii kuonekana vilaza. Nimeanza kuingiwa na mashaka kuhusu uwezo wenu kama wanahabari. Nawakilisha
 
Back
Top Bottom