Habari waungwana,
Kama tujuavyo, waziri mkuu wa Ethiopia anaendelea na ziara nchini na baada ya kuwasili uwanja wa ndege ameelekea Ikulu. Anatarajia kuweka saini kwenye mikataba mitatu ya ushirikiano ikiwemo mkataba wa kamisheni ya kudumu, hati ya makubaliano ushirikiano sekta ya utalii.
=======
Anaenda kwa sasa ni Rais Jamuhiri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli na anaongelea suala la umeme ambapo Ethiopia wanajenga mabwawa ya kufua umeme na anasema waziri mkuu wa nchi hiyo amekubali kuleta wataalam wanayojenga mabwawa hayo.
Anasema Ethiopia wamekubali kufungua ubalozi nchini Tanzania na tayari amewapa eneo la kujenga ubalozi na makazi ya balozi bure.
Rais Magufuli pia ameongelea utalii na anasema Ethiopia haijawahi kunyanyaswa wala kutawaliwa na anaelezea vita mbalimbali zilizopiganwa na nchi hiyo.
Magufuli: Historia inatueleza kuna kabila lilitoka Ethiopia, waziri mkuu huwezi kumtofautisha na wambulu. Ndege zitakuwa zinakuja na watalii, wataenda kwenye vivutio vya utalii. Ethiopia wameendelea sana kwenye masuala ya Telecomunication. Wana shirika moja kubwa sana ambayo pesa zake ndizo zilizotumika kujenga reli(Standard gauge).
Waziri mkuu akirudi nyumbani, amesema atachagua chuo kimoja kianze kufundisha Kiswahili, Adiss ndio makao makuu ya AU, nilimuomba chuo kikuu kimoja kifundishe Kiswahili na amekubali. Tumekubaliana kwenye viwanda, mining na ametoa ofa ya training katika riadha.
Pia ushirikiano katika majeshi, tunataka kutengeneza Tanzania mpya na Ethiopia mpya. Bahati mbaya umekuja kwa siku mbili, ungeweza kukaa hata kwa wiki mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam