Ikulu: Rais Magufuli awataka watendaji kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao. Awaasa kuridhika na nafasi walizo nazo, siyo kukimbilia Ubunge

Jambo kubwa Sana kwa serikali hii ya JPM ni kutoa nafasi kwa sisi vijana tuoneshe uwezo wetu wa kuwatumikia watanzania Viva MAGUFULI 2020-2025
Mnapewa nafasi bila kufundishwa kuwa viongozi na ndio maana mnachemsha mapema
 
Tunasubiri tuone atasema nini Rais Mzalendo Magufuli



------ UPDATE----

Rais Magufuli leo amemwapisha Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo baada ya kutenguliwa Juni 19, 2020.


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI (KWA UFUPI)

Nami niungane Kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mpya Wa Arusha na Wakuu wa Wilaya waliochaguliwa na Wakurugenzi Wawili.

Nawapongeza sababu mumepata Majukumu Mapya. Niseme kwa Ufupi sana, nendeni mkazingatie viapo vyenu. Inanisikitisha pale ninapowateua na hawafuati viapo vyao.

Utakumbuka hivi karibuni Arusha ilibidi nitengue uteuzi wa wote niliokuwa nimewateua kuanzia RC, Mkurugenzi pamoja na DC. Ni kwa sababu katika kipindi karibu miaka miwili walikuwa wanagombana tu, kila mmoja ni boss, kila mmoja anatengeneza mizengwe ya mwenzake. waliniudhi

Mimi saa nyingine nasikitika sana unapoona watu uliowaapisha na kuwateua na kuwaamini kwa niaba ya Watanzania, wanapoenda kule hawafanyi kadri ya viapo vyao

RPC pamona na mkuu wa TAKUKURU wa Arusha nilikuwa niwaondoe. Nimewasemehe lakini sijawasemehe moja kwa moja. Wakifanya kosa lolote nawatoa. Wafanye kazi niliyowatuma sio wajitume.

RC Arusha wafikishie ujumbe wafanye kazi niliyowatuma kulingana na Mamlaka yao. Wasimamie Sheria.

Pale Monduli kuna Migogoro inatengenezwa kwa makusudu. Mfano Mgogoro wa Kanisa na Shule. Wataka Jiji likalipe Milioni 400 ili wajenge Shule.

Kulikuwa na Mgogoro kwenye Msikiti, kuna kiongozi alikuwa anawahubiri Waislam, Mkurugenzi alipokataa akaonekana mbaya. Mwinyi, Mkapa na Kikwete walikataa, Na Kikwete alijibu kwa Maandishi kukataa. Kwa hiyo msimamo ni ule ule. Ila panapotokea shughuli kama Maulid, ile open space inatimika bure. Tatizo lile limeletelezwa na mkuu wa mkoa. Kila mmoja anatoa ahadi, tusitoe ahadi ambayo haiwezekani. Nalizungumza hili ili mkuu wa mkoa, Wilaya na DC Msiingilie.

Kenani wewe ulikuwa Mwenyekiti wa UVCCM na ulikimbiza mwenge mwaka jana, umezunguka nchi nzima na Tanzania unaifahamu. Nina imani hauwezi kushindwa kazi Arusha

Wito wangu muende mkafanye kazi na mridhike, mkumbuke tu miaka bado mingi mnayo. Kwa sababu tatizo lingine la vijana unapompa nafasi wana tendency ya kutoridhika na hizo nafasi wanashindwa kuelewa miaka bado ipo mingi sana. Sasa mkaridhike na kazi mliyonayo mkawatumie Watanzania. Haiwezekani watu wanatumwa kwenda kufanya kazi za serikali, wao wanafanya kazi zao binafsi, kazi zao walizokuwa wanafanya wengine mnazifahamu, watu wanapaswa kufanya kazi walizotumwa.

Nitashangaa sana siku moja IGP akagombee ubunge Bunda kwa kuwa anatoka Bunda akitegemea akichaguliwa huenda nitamteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati hata hana uhakika atashinda kura za maoni, lakini tujifunze kuridhika

Nafahmau Pima ulikuwa kwenye mawazo ya kwenda kumtoa Msukuma kule. Nikaona ngoja nikuteue, kama ukitaka kwenda nenda. Siwazuii kugombea lakini kama umeaminika tumikia nafasi yako. Kila mmoja anaweza mahali popote.

Ntakushangaa mkuu wa mkoa wa Morogoro uende kugombea ubunge, lakini ndio demokrasia.

Mkurugenzi jiji la Arusha nakuagiza ile stendi sasa ukaimalize, tunataka watu wa Arusha wapate stendi bora kama walivyopata watu wa mikoa mingine. Viongozi walitaka stendi ikajengwe kwenye kiwanja cha CCM hii haiwezekani, japo mimi ni CCM lakini hili hapana.

RPC, IGP mkawaonye watendaji wenu walioko Arusha, wakafanye kazi nilizowatumwa, wasifanye kazi ambazo sikuwatuma, nao leo ilikuwa niwatoe. RPC pamoja na mkuu wa TAKUKURU wa Arusha lakini nimeona niwaonye hapa hapa, nimeamua kuwasamehe lakini sijawasamehe moja kwa moja.

Nendeni mkachape kazi, kamalize kero za Wananchi. Mkamtangulize pia Mungu.


WAZIRI WA TAMISEMI, SELEMAN JAFO

RC Arusha umepata fursa nenda kaishi vizuri na Ma-DC wako, niwaombe Ma-DC hasa ambao wapo Makao Makuu na Ma-RC wenu nendeni mkafanye kazi kwa upendo na ushirikiano, lakini Wakuu wa Mikoa msiwabemendee wakuu wenu wa Wilaya

Nyie mmepewa dhamana, Mh Rais amewaamini sana, ushauri wangu nendeni mkafanye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana, kila mtu amuheshimu mwenzake tukiwa na hali hiyo tutafanya vizuri sana na tutapata mafanikio makubwa

RC Arusha umepata fursa nenda kaishi vizuri na Ma-DC wako, niwaombe Ma-DC hasa ambao wapo Makao Makuu na Ma-RC wenu nendeni mkafanye kazi kwa upendo na ushirikiano

Wakuu wa Mikoa Nchi nzima nawaomba msiwabemende Wakuu wenu wa Wilaya msiwafanye Wakuu wa Wilaya wasifanye lolote, wasaidieni msiwabemende, na Wakuu wa Wilaya waheshimuni Wakuu wa Mikoa, tukifanya hivi tutakuwa tumemsaidia Rais

View attachment 1485758
Viongozi wateule wakila Kiapo cha Uadilifu baada ya kuapishwa​

Rais Magufuli

Mheshimwa Waziri wa tamisemi, Mheshimiwa Katibu Mkuu Utumishi Dr. Ndumbalu, Wakuu wa Mikoa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu, Watendaji wengine.. Habari za asubuhi?

Nami niungane Kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mpya Wa Arusha na Wakuu wa Wilaya waliochaguliwa na Wakurugenzi Wawili.

Nawapongeza sababu mumepata Majukumu Mapya.

Niseme kwa Ufupi sana, nendeni Mkazingatie Viwapo vyenu.

Inanisikitisha pale ninapo wateua na hawafuati Viapo vyao.

Mtakumbuka Arusha nmewatengua Wote sababu kwa miaka miwili walikiwa wanagombana tu. Walifanya kazi zao lakini waliniuzi kwa kutokushirikiana kufanya yale ambayo nliwaagiza. Naomba ninyi msifanye hivyo.

Kwahiyo ninachowaomba kafanyeni kazi na ikiwezekana karidhike na ulicho nacho. Vijana wana atendence ya kutolidhika na nafasi zao. Ninawaamin Vijana, wazee na Wakina Mama. Kafanye kazi mlizopangwa.

Mkawaonye watendaji wenu walio Arusha. Wakafanye kazi nlizowatuma.

Rpc pamona na mkuu wa takukuru wa Arusha nlikuwa niwaondoe. Nmewasemehe lakini sijawasemehe moja kwa moja. Wakifanya kosa lolote nawatoa. Wafanye kazi nliyowatuma sio wajitume.

RC Arusha wafikishie ujumbe wafsnye kazi nliyowatuma kulingana na Mamlaka yao. Wasimamie Sheria.

Pale Monduli kuna Migogoro inatengenezwa kwa makusudu. Mfano Mgogoro wa Kanisa na Shule. Wataka Jiji likalipe Milioni 400 ili wajenge Shule.

Kulikuwa na Mgogoro kwenye Msikiti, kuna kiongozi alikuwa anawahubiri Waislam, Mkurugenzi alipokataa akaonekana mbaya. Mwinyi, Mkapa na Kikwete walikataa. Na Kikwete alijibu kwa Maandishi kukataa. Kwahiyo msimamo ni ule ule. Ila panapotokea shughuli kama Maulid, ile open space inatimika bure. Tatizo lile limeletelezwa na mkuu wa mkoa. Kila mmoja anatoa ahadi, tusitoe ahadi ambayo haiwezekani. Nalizungumza hili ili mkuu wa mkoa, Wilaya na DC Msiingilie.

Nataka ishu ya Stand iishe. Kila siku mnataka Stand ya Arushwa ijengwe karibu na CCM, ile ni Stand ya Wananchi..

Wamecheleweshea wananchi Maendeleo. Hawa watu wakabishanie nje uraiani.

Na hii iwe fundisho, jengeni element ya kuvumiliana.

Kwahiyo ni matumaini yangu ninyi mlioteuliwa manaenda kutimiza wajibu wenu. Mkashirikiane na kila mtu.

Arusha tumepeleka Miradi Mingi mno, na wananch wanajua. Kasimamie hilo.

Viongozi ninao wateua walidhike na Vyeo walivyo navyo.

Nashangaa Sirro aende kugombea Bunda eti akishinda nitampa UWAZIRI. Kama ningetaka si ningemteua tu mapema?

Unaweza ukagombea hujui kama utashinda au kama tutakuteua. Ndumbalu kula za maoni alikuwa wanne lakini wengine tukawakata tukamchagua yeye.

Lidhika na vyeo vyenu. Kama una uhakika ukienda utashinda, nenda tena kwa speed.

Nafahmau Pima ulikuwa kwenye mawazo ya kwenda kumtoa Msukuma kule. Nikaona ngoja nikuteue, kama ukitaka kwenda nenda. Siwazuii kugombea lakini kama umeaminika tumikia nafasi yako. Kila mmoja anaweza mahali popote.

Ntakushangaa mkuu wa mkoa wa Morogoro uende kugombea ubunge.. Lakini ndio demokrasia.

Nlikuwa nachomekea tu. Lakini nawapongeza sana. Nendeni achape kazi. Kamalize kero za Wananchi. Mkamtangulize pia Mungu. Mungu a Wabariki sana.
Asante sana.

Vizuri, Gambo sasa aende kugombana na mkewe. Amefuata nyayo za Magessa Mulongo, ndoto zake za kisiasa ndio zimefia hapo.
 
Maendeleo ya vitu versus maendeleo ya watu. Impact analysis
Kitu kikubwa ni uwekezaji kwenye miundombinu ambayo inamgusa kila mtanzania kwaio kwa Kasi ile ile 2020-2025 mark words unakwenda kushuhudia Tanzania yenye miundombinu Bora na maisha Bora kwa raia wake ni swala la muda tu miaka 5 haitoshi kufanya kila kitu mkuu tumuongeze mh Rais muda
 
Maendeleo ya vitu versus maendeleo ya watu. Impact analysis
Unajua tofauti yake au umekaririshwa na wasaka tonge kupitia siasa? Ni hao hao wakipanda jukwaani wanatoa ahadi za maendeleo ya vitu. Ni hao hao Serikali ikiwekeza kwenye maendeleo ya vitu wanadai ni fedha ya kodi za wananchi. Upumbavu na ulofa wa kisiasa
 
Ila nyie wanalumumba mna mambo.
Kipindi Gambo hajapigwa chini mlikuwa mnamsifu hapa sasa katimuliwa mumemgeuka.
 
Rais wa Tanzania John Magufuli amewaasa viongozi anaowateua kuridhika na nafasi wanazopatiwa akisema kuwa haiwezekani ukapata kila kitu.

Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akiwaapisha Bw. Idd Hassan Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuapa kwa viongozi wengine walioteuliwa wa Mkoa wa Arusha, Kamishna wa polisi Edward Jotham Balele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Bw.Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

''Niendelee kutoa wito kwa viongozi ninaowateua wajifunze pia kuridhika na nafasi walizonazo, nitashangaa sana kama IGP ataondoka hapa aende akagombee Bunda, kwa sababu anatoka Bunda, akawa anaomba ubunge akitegemea nitamteua kuwa waziri, kwanza hana uhakika kama atashinda katika kura za maoni na anawezekana akashinda na bado nikamfuta.'' Alieleza Rais Magufuli

''Ni kuridhika lakini hauwezi kuwa na kila kitu, lakini Demokrasia iko huru kama una uhakika kabisa kuwa ukienda kule utashinda tu, basi nenda tu, nenda tena nenda kwa spidi kubwa, lakini mimi ninafikiri saa nyingine ni kuridhika, kila mahali unaweza kufanya maajabu katika position yako, vinginevyo huwezi kuwa na kila kitu, inawezekana huwezi ukawa na kila kitu.'' Alisema.

Rais Magufuli ameeleza sababu za kutengua uteuzi wa viongozi watatu wa Mkoa wa Arusha kuwa ni kutokana na viongozi hao kutoelewana na kugombana bila sababu za msingi licha ya kuonywa mara kadhaa, na ametaka vitendo hivyo visijirudie kwa wateule wapya na viongozi wengine nchini.

''Mimi saa nyingine huwa nasikitika sana unapowaona watu uliowateua na kuwaapisha na kuwaamini kwa niaba ya watanzania wanapokwenda kule hawafanyi kadiri ya viapo walivyonavyo.''

''Mtakumbuka hivi karibuni Arusha ilibidi nitengue uteuzi wa wote niliokuwa nimewateua kuanzia RC, Mkurugenzi wa mji pamoja na DC ni kwasababu katika kipindi cha miaka karibu miwili walikuwa wanagombana tu, kila mmoja ni bosi kila mmoja anatengeneza mizengwe dhidi ya mwenzake... Sikufurahishwa''.''Walifanya kazi zao lakini waliniudhi wao kutokushirikiana kufanya yale ambayo nimewaagiza,

''Sasa nimewateua ninyi sitaki yajitokeze hayo, kafanyeni kazi na mkaridhike na mlicho nacho kwasababu ...tatizo jingine la vijana unapompa nafasi wana tabia ya kutoridhika na hizo nafasi wanashindwa kujua kuwa miaka bado ipo mingi sana, sasa mkaridhike na kazi mliyonayo mkawatumikie watanzania''.

Kuhusu migogoro inayoabili Arusha , Magufuli amewataka viongozi kusimamia sheria na kuzingatia viapo vya maadili ya kazi wakati wa utekelezaji wa majukumu mbali mbali.

''Kwa sababu RPC yupo hapa, IGP yupo hapa yule wa TAKUKURU yuko hapa, mkawaonye watendaji wenu walioko Arusha.. wakafanye kazi nilizowatuma wasifanye kazi ambazo sikuwatuma,nao leo nilikuwa niwatoe RPC pamoja na mkuu wa TAKUKURU wa Arusha lakini nimeona niwaonye hapahapa, nimeamua kuwasamehe lakini sijawasemehe moja kwa moja, wakifanya kosa lolote wataondoka nataka wakafanye kazi nilizowatuma sio kazi wanazojituma wao.''

''Nimejitahidi sana kuwasamehe kwa sababu haiwezekani ukawa umewatuma watu kwenda kufanya kazi za serikali wanakwenda kufanya shughuli zao, nyinyi mnafahamu shughuli walizokuwa wanazifanya hasa katika kipindi hiki kifupi. Kwa hiyo kawafikishie ujumbe.'' Alisema Magufuli

Rais Magufuli amemtaka mkuu mpya wa mkoa kusimamia migogoro mkoani Arusha ambayo amedai kuwa mingine ilikuwa ikitengenezwa kwa makusudi kama vile mgogoro wa kanisa na shule. Mgogoro ambao ulishamalizwa zamani kuwa kama shule inahitaji eneo zaidi ijenge ghorofa katika shule yao.

''Palikuwa na mgogoro kwa waislamu , eneo la msikiti ni mita za mraba 10495 na eneo la wazi ni mita 4165, kuna kiongozi mmoja alikuwa akihubiri kwa ndugu zetu waislamu, ombeni na hii open space, Mkurugenzi alipokataa, ikawa Mkurugenzi amekataa kutoa eneo, ni kuchonganisha uongozi wa mkurugenzi na ndugu zetu waislamu''.

Lakini tatizo lile limesababishwa na Mkuu wa Mkoa, anazungumza hivi huku, na huku anazungumza hivi huku, lengo ni kuonekana kwamba yeye ni mzuri sana, kila mmoja anatoa ahadi, tusitoe ahadi ambazo haziwezekani ni lazima tusimamie sheria.''

''Na hili liwe fundisho kwa viongozi ninaowateua, lazima mkajenge element za kuvumiliana, lazima tujifunze kuzingatia sheria na maadili na viapo vyetu tunavyoviapa.'' Alieleza Rais Magufuli.

hqdefault.jpg
 
Back
Top Bottom