IKULU: Rais Magufuli awapongeza Taifa Stars na bondia Hassan Mwakinyo. Awapatia viwanja Dodoma

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,786
114,189
Wanabodi,

Declaration of interest
Mwaliko huu hauna uhusiano na bandiko hili
Trend Reading, Taifa Stars Kualikwa Ikulu Kupongezwa. Ushindi Huu Ni Dalili Njema Kwa Rais Magufuli. Please Don't Politicise!. - JamiiForums

Kufuatia ushindi wa jana wa Taifa Stars, leo Rais Magufuli, amewakaribisha Ikulu kuwapongeza kwa lunch ya nguvu. Mwaliko huo pia umehusisha Kamati ya Uhamasishaji.

Live itaanza saa 4:00 kamili asubuhi hii.
Karibuni.
P.
Update
Muda huu Rais anaongea na wachezaji wa Timu ya Taifa! ameeleza alivyochukizwa na Timu yetu ilipofungwa na Leshoto. Amesema wazi kuwa alikuwa hapokei wala kujibu sms za Waziri wake Makyembe kutokana na kuchukizwa .Ameanza kupokea simu zake leo asubuhi baada ya Taifa Stars kufuzu AFCON!
AIdha amebainisha kuwa Waziri Mkuu na Makamu wamekuwa wakimpigia simu kumuomba fedha za Mashindano ya Vijana Under 17 yanayofanyika nchini Mwezi ujao na amekuwa akiwakatalia kwa kuwa anajenga Reli.
Hata hivyo kutokana na ushindi wa jana...amekubali kutoa fedha hizo!
Tunasafari Ndefu!
Lakini mwishoni amepiga tafu Peter Tino Sh.5,000,000.00 zikamsaidie kwenye Biashara zake!
P
 
Kwakweli tuweke siasa pembeni,tunaipongeza sana timu ya uhamasishaji iliyofanywa na Makonda kwa kweli imezaa matunda.Nadhani zile Milioni kumi walizoahidiwa wachezaji washaingiziwa kwenye account zao.Everybody say yeaaaaaah.
 
Wanabodi,

Declaration of interest
Mwaliko huu hauna uhusiano na bandiko hili
Trend Reading, Taifa Stars Kualikwa Ikulu Kupongezwa. Ushindi Huu Ni Dalili Njema Kwa Rais Magufuli. Please Don't Politicise!. - JamiiForums

Kufuatia ushindi wa jana wa Taifa Stars, leo Rais Magufuli, amewakaribisha Ikulu kuwapongeza kwa lunch ya nguvu. Mwaliko huo pia umehusisha Kamati ya Uhamasishaji.

Live itaanza saa 4:00 kamili asubuhi hii.
Karibuni.
P.
Mayalla, unatukaribisha ikulu?
Mbona unanitia mashaka! Tukifika kuna utaratibu gani jinsi ya kuingia.
Ninatanguliza shukurani zangu.
 
Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi wa chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?

Asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo

Asante kasi ya Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom