Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
TAARIFA

Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 20 Oktoba, 2019 atawaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Balozi.

Hafla ya uapisho huo itafanyika Ikulu Jijini DSM kuanzia saa 9:30 alasiri hii. Itarushwa mubashara kupitia Redio, Televisheni na Mitandao.

====

UPDATES: 1600hrs

Rais John Magufuli amewaapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi na Ali Sakila kuwa Balozi leo Oktoba 20 Ikulu jijini Dar

Rais Magufuli: Niwapongeze sana viongozi niliowaapisha leo hii, nendeni mkafanye kazi, katimizeni majukumu yenu kwa weledi”

Rais Magufuli: Muende mkawatumikie Watanzania bila kumuonea mtu kwa kadri Mungu wenu atakavyowaongoza. Kabunduguru wewe umefanya kazi sehemu nyingi, Utumishi na TAMISEMI naamini kwenye Mahakama utatusaidia sana

Rais Magufuli: Kaendeleze mazuri yanayofanywa na Mahakama. Mahakama inafanya kazi nzuri na imekuwa kimbilio la Wananchi wengi - Balozi Ally kaendelee na kazi zako. Kwa ufupi mkafanye kazi zenu vizuri kwa kwenda kuwatumikia watu

Rais Magufuli: Brigedia Jenerali wa TAKUKURU anafanya kazi vizuri. Kwenye Vyama vya Ushirika huku wakulima walikuwa wanadhulumiwa - Viongozi 99 wamekamatwa na Tsh. Bilioni 1.2 zilikuwa kwa viongozi wa AMCOS. Brigedia ameniambia lakini hadi sasa zimerejeshwa Milioni 255

Rais Magufuli: Kazi ya uongozi ni kusimamamia Haki, kufuata Sheria bila kumuonea mtu yeyote. Unaweza kusemwa vibaya ila wewe endelea na kazi - Si wote watakupenda ila tufanye kazi. Kwa ujumla nawashukuru wote, Mama Samia na kila mtu katika Utumishi wenu

7(1).jpg

8jpg.jpg

12.jpg

11..jpg



 
Duh! Ila kuna kitu mkuu inabidi ajifunze hapa!

Kuzushiwa kifo na watu walivyokuwa wakishangilia unadhani tuna Taifa moja tena?

Wengi waliokuwa wakifurahia kwamba amekufa, walitoa sababu za wale mashabiki wake kufurahia mateso ya Lissu na walofurahia kupotezwa na inasemekana kuuwawa kwa Ben Saanane!

Hamkani mambo siyo shwari tusidanganyane!
 
Back
Top Bottom