Ikulu: Rais Magufuli awaapisha Mawaziri wawili na Balozi. Ahoji kuhusu upelelezi wa tukio la utekwaji wa Mo Dewji

Mwenye clip ya dr.mahiga akiwa davos atuwekee kasema alikomaa nao sana mabeberu pale davos hadi wakamwelewa. Na amesema waziri wa madiba ndio aliemtonya kuwa ishue haijakaa poa awahi kusawazisha.
 
Mr president untaka kutwambia nini Baba, kwammba Mamboleo allikuwa anatuzuga?? kwa nini umeamu kuongea leo wakati ambao tumeshasahau?? Mr president lakini si na wewe ulituhumiwa kutekwa kwa Mo???

Au tuseme mr president unatak wa release Movie yako mpya?? imekammilika?? una uhakika itabamba?
Hii muvi anawauzia watasha huko abroad. Ili washushe misaada na madolari. They can buy this..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wote walio ndani na nje ya nchi tukome mara moja na kukaa kimya maana taifa halitawavumilia. Nchi hii ni ya kidemokrasia na kwa hiyo hatutaki kufundishwa na yeyote kwani tunajitambua.
Huyu ni mlevi? Pumbavu kabisa!
Nchi ya kidemokrasia maana yake ni 'kukaa kimya'?

Huyu ni mgonjwa. Siyo mzima kichwani huyu!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, leo Machi 04, anawaapisha Balozi Dk. Augustine Phillip Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Prof. Palamagamba John Mwaluko Aidan Kabudi kuwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hao ni wakongwe, shati kufanya Suruali tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu!

Viongozi wanaoapishwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Augustine Mahiga. Pia anaapishwa Balozi Hassan Simba anayekwenda kuiwakilisha nchi nchini Malawi.

Pia IGP Sirroanawaapisna na kuwavisha vyeo vya ukamishna wateule wa Jeshi la Polisi.

-----
Hotuba ya Waziri Profesa Kabudi

Mimi ni kiumbe dhaifu nisiyestahili na mwenye mawaa mengi. Namshukuru Mungu kwa hili. Namshukuru Rais Magufuli kwa kuniona nafaa katika nafasi hii.

Nimefundishwa na Dr. Augustine Mahiga na nilijifunza mengi kwake na kiingereza kwakweli alikuwa anakimanya. Nitaitumikia nafasi hii kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na uwezo wangu wote.

Tanzania ndio nchi pekee ambayo 'Universal Declaration of Human Rights' ni sehemu ya Katiba yetu. Hakuna kitu cha kuongeza kwa sababu vitu vya kutusaidia kusonga mbele vipo.

Watanzania wote walio ndani na nje ya nchi tukome mara moja na kukaa kimya maana taifa halitawavumilia. Nchi hii ni ya kidemokrasia na kwa hiyo hatutaki kufundishwa na yeyote kwani tunajitambua.

Hotuba ya Waziri Dr. Mahiga

Namshukuru Rais kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri. Kazi uliyokuwa umenipa ilikuwa inafanana na kazi na uzoefu niliokuwa nao tangu 1983 hadi 2013.

Nchi yoyote lazima itafute nafasi katika Jumuiya ya Kimataifa. Kwa bahati nzuri, nafasi yetu ndani ya Jumuiya ya Kimataifa ipo vizuri na tuna marafiki wengi. Hatuna adui duniani

Katika Jumuiya ya Kimataifa vitu havikai bila ya kubadilika, hivyo unapoingia ubia lazima uwasiliane na Jumuiya za Kimataifa. Tulikuwa na kazi ya kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuhusu siasa yetu ya ndani lakini lazima tupambane na wapotoshaji

Tumekuwa na malumbano ya wazi na Mashirika ya Kimataifa, kwa juhudi za Wizara wamenza kutuelewa. Nilipata mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, aliniambia amenipa jukwaa la kueleza uhalisia. Ufaransa pia walinialika na niliwaeleza wakaelewa

Natoa shukrani za pekee kwa kunipa nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nitakuwa nafasi ya mbele kuwa karibu na Bunge, Wananchi na Serikali. Nitaitekeleza Katiba yetu kwa vitendo

Nimeshiriki kutengeneza katiba za mataifa matano na sasa nitapata muda wa kuingalia kwa karibu Katiba yetu.

Namshukuru Rais kwa kumrudisha nyumbani kwani sasa nitakuwa karibu zaidi ya bunge na wananchi.

Hotuba ya Jaji Mkuu, Profesa Juma

Tulizoea likitajwa jina la Prof. Kabudi ilikuwa ni Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Mahiga ili kuwa ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Sasa tutatakiwa kuzoea upya, tunamshukuru Prof. Kabudi kwa kufanya kazi kubwa sana

Prof. Kabudi ametusaidia sana kwenye kurahisisha kazi ya utoaji haki mfano ni umuhimu wa 'Mobile Court'. Pia matumizi ya TEHAMA ambayo ndio uelekeo mpya wa mfumo wa Mahakama, tunaamini Dkt. Mahiga utatusaidia pia katika hili

Hotuba ya Spika Jobu Ndugai

Spika Ndugai: Dkt. Mahiga kwenye vitabu vya watoro sasa unaondoka na inawezekana Prof. Kabudi akachukua nafasi, lakini tunaelewa majukumu yenu. Kuna kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, itakusaidia sana Prof. Kabudi katika kufanya kazi

Kuna katabia kameibuka kwa watu kuisema vibaya nchi yao wakiwa nje na ndio maana tumekuwa wakali sana Tukuombe Waziri umshawishi Rais kuhusu nchi zinazotaka kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, baadhi ya majirani bado hawako vizuri

Viongozi wengi wa Taifa hili wametoka katika familia duni na masikini hivyo taifa hili halina mwenye kulimiliki hivyo kila mtu afanye kazi.

Hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Nawapongeza mawaziri walioteuliwa na kusema kutokana na umahili na uzoefu wao ana uhakika watafanya vizuri.

Balozi umeapa unaweza kufanya kazi ni muhimu kusimamia mahusiano mazuri maana nchi yetu ipo katika mkakati mzuri wa kuinua uchumi kwahiyo jukumu lako kubwa ni kutuunganisha na wafanyabiashara wakubwa

Juzi nilipokuwa na wafanyabiashara wadogo na wakati maeneo waliyolalamikia ni baadhi ya watumishi wa polisi na tumewaahidi tutalifanyia kazi suala hilo hivyo mhakikishe mnatimiza yale mnayotakiwa kuyafanya

Hotuba ya Rais Magufuli

Rais Magufuli: Nawapongeza wote kwa ajili ya majukumu yenu mapya. Nina hakika mtazingatia maneno yaliyopo katika maadili

Mengi yamezungumzwa, na Mimi niungane na wengine kuwapongeza wote mlioapishwa. Nimefanya mabadiliko haya kwa sababu za kawaida, ukiwa kocha unaweza kubadilisha wachezaji wako. Wako wanaosema huyu sio Mwanasheria, kwani anakwenda kufundisha Sheria?

Wizara ya Sheria imejaa wanasheria, sasa unaweza kumpeleka Mwanadiplomasia ili akaweke mambo sawa. Naamini Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje watampa ushirikiano

Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, nako kunahitaji mtu kama Prof. Kabudi ili aende akawasukume. Ukichanganya Sheria na Diplomasia mambo yanakuwa mazuri. Prof. Kabudi ni muwazi sana

Kazi ya kuteua Makamishna wa Jeshi la Polisi haikuwa ndogo, nilimuita Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu wa Wizara. Huwezi kuwa Kamanda wa Oparesheni kisha Askari wako wanauawa. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri ukiacha kasoro ndogo

Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi

Lazima tujenge taswira ya Jeshi la Polisi kama lilivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Kama kuna maafisa wa Jeshi la Polisi wanaofanya vibaya leta taarifa ili hata nyota zao zipunguzwe na wanaoshindwa wasipelekwe Makao Makuu

Wale Askari wadogo wanaofanya kazi vizuri msiwakatishe tamaa, anamkamata Mtu mnamwambia amwachie. Msisite kuleta mapendekezo kwa wale wanaofanya vizuri. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri kama majeshi mengine lakini hizi dosari lazima zirekebishwe.

Nawashukuru sana viongozi wa dini kwa kuliombea taifa, kuzidisha ushirikiano na kudumisha amani.
LEO NDIYO ANAFAHAMU KUWA POLISI WANAFANYA MICHEZO YA KITOTO....? AU ANATAKA KUJIVUA LAWAMA.....HAKUJUA KUWA MO DEWJI ALIKUWA IKULU KABLA YA KUPATIKANA?
 
Mwenye clip ya dr.mahiga akiwa davos atuwekee kasema alikomaa nao sana mabeberu pale davos hadi wakamwelewa. Na amesema waziri wa madiba ndio aliemtonya kuwa ishue haijakaa poa awahi kusawazisha.
anasema aliitwa Finland na ufaransa, kisema kwmaba alisawazisha mambo ni kijifariji tu.
 
SITUNAAMBIWA KUWA HUYU KABUDI NDIYO MWANASHERIA NGULI WA NCHI HII, INAKUWAJE ANAONDOLEWA HAPO ALIPOKUWA NA NDIYO FANI YAKE ALIYOSOMEA?
 
Watanzania wote walio ndani na nje
ya nchi tukome mara moja na kukaa
kimya maana taifa halitawavumilia.
Nchi hii ni ya kidemokrasia na kwa
hiyo hatutaki kufundishwa na yeyote
kwani tunajitambua. Hii kauli....?
Mkuu cha msingi mlo uingie tumboni tu, watu watafanya kila kitu wamfurahishe bwana yule.
 
Nipo jirani kabisa na Mambosasa. Naona kabisa hayupo vizuri. Nafikiri mapigo ya moyo yamebadilika, Anahema kwa shida kidogo. Sitanii nipo naye jirani kabisa kabisa.
mwambie ameiona AK 47 hiyo inavyomuelekea....akae mkao mzuri...
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, leo Machi 04, anawaapisha Balozi Dk. Augustine Phillip Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Prof. Palamagamba John Mwaluko Aidan Kabudi kuwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Nilifikiri huyu Palamagamba ni aina ya samaki :p:p
 
Nimeshangaa sana kusikia Mzee Baba JPM(a.k.a Jiwe) kuwa hajui kabisa Mo alikuwa wapi kwa siku 9. Hahahahaa just haaaaa. Hii kwa kweli inafurahisha na kusikitisha sana. Akiwa na uso mkavu kabisa mbele ya Camera na TV kuwa hajui Mo alikuwa wapi. Je hili liwe ajabu lingine la dunia?

Haya mambo haya hahaaaa .

# Eti maendeleo hayana chama??
 
Back
Top Bottom