Ikulu: Rais Magufuli awaapisha Mawaziri wawili na Balozi. Ahoji kuhusu upelelezi wa tukio la utekwaji wa Mo Dewji

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Katika hafla mbalmbali zinazofanyika, imekuwa ngumu mno kwa Raisi kushindwa kutoa sababu za kufanya maamzi fulani. Hata kama atajizuia ila mwishoni unashangaa ameshasema.

Tunatarajia kuwa ataeleza sababu za kutengua teuzi za Prof Kabudi na Mahiga na kuwapangia wizara mpya.

Pia tunatarajia kuwa ataeleza sababu za kutohamia Dodoma kabla ya mwaka 2018 kuisha kama alivyoahidi au kwa nini hakuhamia mapema January kama Waziri Mkuu alivyoutangazia umma.

========

Karibu!

Viongozi wanaoapishwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Augustine Mahiga. Pia anaapishwa Balozi Hassan Simba anayekwenda kuiwakilisha nchi nchini Malawi.

Pia IGP Sirroanawaapisna na kuwavisha vyeo vya ukamishna wateule wa Jeshi la Polisi.

-----
Hotuba ya Waziri Profesa Kabudi

Mimi ni kiumbe dhaifu nisiyestahili na mwenye mawaa mengi. Namshukuru Mungu kwa hili. Namshukuru Rais Magufuli kwa kuniona nafaa katika nafasi hii.

Nimefundishwa na Dr. Augustine Mahiga na nilijifunza mengi kwake na kiingereza kwakweli alikuwa anakimanya. Nitaitumikia nafasi hii kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na uwezo wangu wote.

Tanzania ndio nchi pekee ambayo 'Universal Declaration of Human Rights' ni sehemu ya Katiba yetu. Hakuna kitu cha kuongeza kwa sababu vitu vya kutusaidia kusonga mbele vipo.

Watanzania wote walio ndani na nje ya nchi tukome mara moja na kukaa kimya maana taifa halitawavumilia. Nchi hii ni ya kidemokrasia na kwa hiyo hatutaki kufundishwa na yeyote kwani tunajitambua.

Hotuba ya Waziri Dr. Mahiga

Namshukuru Rais kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri. Kazi uliyokuwa umenipa ilikuwa inafanana na kazi na uzoefu niliokuwa nao tangu 1983 hadi 2013.

Nchi yoyote lazima itafute nafasi katika Jumuiya ya Kimataifa. Kwa bahati nzuri, nafasi yetu ndani ya Jumuiya ya Kimataifa ipo vizuri na tuna marafiki wengi. Hatuna adui duniani

Katika Jumuiya ya Kimataifa vitu havikai bila ya kubadilika, hivyo unapoingia ubia lazima uwasiliane na Jumuiya za Kimataifa. Tulikuwa na kazi ya kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuhusu siasa yetu ya ndani lakini lazima tupambane na wapotoshaji

Tumekuwa na malumbano ya wazi na Mashirika ya Kimataifa, kwa juhudi za Wizara wamenza kutuelewa. Nilipata mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, aliniambia amenipa jukwaa la kueleza uhalisia. Ufaransa pia walinialika na niliwaeleza wakaelewa

Natoa shukrani za pekee kwa kunipa nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nitakuwa nafasi ya mbele kuwa karibu na Bunge, Wananchi na Serikali. Nitaitekeleza Katiba yetu kwa vitendo

Nimeshiriki kutengeneza katiba za mataifa matano na sasa nitapata muda wa kuingalia kwa karibu Katiba yetu.

Namshukuru Rais kwa kumrudisha nyumbani kwani sasa nitakuwa karibu zaidi ya bunge na wananchi.

Hotuba ya Jaji Mkuu, Profesa Juma

Tulizoea likitajwa jina la Prof. Kabudi ilikuwa ni Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Mahiga ili kuwa ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Sasa tutatakiwa kuzoea upya, tunamshukuru Prof. Kabudi kwa kufanya kazi kubwa sana

Prof. Kabudi ametusaidia sana kwenye kurahisisha kazi ya utoaji haki mfano ni umuhimu wa 'Mobile Court'. Pia matumizi ya TEHAMA ambayo ndio uelekeo mpya wa mfumo wa Mahakama, tunaamini Dkt. Mahiga utatusaidia pia katika hili

Hotuba ya Spika Jobu Ndugai

Spika Ndugai: Dkt. Mahiga kwenye vitabu vya watoro sasa unaondoka na inawezekana Prof. Kabudi akachukua nafasi, lakini tunaelewa majukumu yenu. Kuna kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, itakusaidia sana Prof. Kabudi katika kufanya kazi

Kuna katabia kameibuka kwa watu kuisema vibaya nchi yao wakiwa nje na ndio maana tumekuwa wakali sana Tukuombe Waziri umshawishi Rais kuhusu nchi zinazotaka kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, baadhi ya majirani bado hawako vizuri

Viongozi wengi wa Taifa hili wametoka katika familia duni na masikini hivyo taifa hili halina mwenye kulimiliki hivyo kila mtu afanye kazi.

Hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Nawapongeza mawaziri walioteuliwa na kusema kutokana na umahili na uzoefu wao ana uhakika watafanya vizuri.

Balozi umeapa unaweza kufanya kazi ni muhimu kusimamia mahusiano mazuri maana nchi yetu ipo katika mkakati mzuri wa kuinua uchumi kwahiyo jukumu lako kubwa ni kutuunganisha na wafanyabiashara wakubwa

Juzi nilipokuwa na wafanyabiashara wadogo na wakati maeneo waliyolalamikia ni baadhi ya watumishi wa polisi na tumewaahidi tutalifanyia kazi suala hilo hivyo mhakikishe mnatimiza yale mnayotakiwa kuyafanya

Hotuba ya Rais Magufuli

Rais Magufuli: Nawapongeza wote kwa ajili ya majukumu yenu mapya. Nina hakika mtazingatia maneno yaliyopo katika maadili

Mengi yamezungumzwa, na Mimi niungane na wengine kuwapongeza wote mlioapishwa. Nimefanya mabadiliko haya kwa sababu za kawaida, ukiwa kocha unaweza kubadilisha wachezaji wako. Wako wanaosema huyu sio Mwanasheria, kwani anakwenda kufundisha Sheria?

Wizara ya Sheria imejaa wanasheria, sasa unaweza kumpeleka Mwanadiplomasia ili akaweke mambo sawa. Naamini Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje watampa ushirikiano

Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, nako kunahitaji mtu kama Prof. Kabudi ili aende akawasukume. Ukichanganya Sheria na Diplomasia mambo yanakuwa mazuri. Prof. Kabudi ni muwazi sana

Kazi ya kuteua Makamishna wa Jeshi la Polisi haikuwa ndogo, nilimuita Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu wa Wizara. Huwezi kuwa Kamanda wa Oparesheni kisha Askari wako wanauawa. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri ukiacha kasoro ndogo

Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi

Lazima tujenge taswira ya Jeshi la Polisi kama lilivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Kama kuna maafisa wa Jeshi la Polisi wanaofanya vibaya leta taarifa ili hata nyota zao zipunguzwe na wanaoshindwa wasipelekwe Makao Makuu

Wale Askari wadogo wanaofanya kazi vizuri msiwakatishe tamaa, anamkamata Mtu mnamwambia amwachie. Msisite kuleta mapendekezo kwa wale wanaofanya vizuri. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri kama majeshi mengine lakini hizi dosari lazima zirekebishwe.

Nawashukuru sana viongozi wa dini kwa kuliombea taifa, kuzidisha ushirikiano na kudumisha amani.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Hajaongea siku nyingi.. leo tunategemea kusikia mengi. Halafu akijuaga tunasubiri anakula kona.. ila kwa hili mmmmh hawezi kukepwa😊
 
Katika hafla mbalmbali zinazofanyika, imekuwa ngumu mno kwa Raisi kushindwa kutoa sababu za kufanya maamzi fulani. Hata kama atajizuia ila mwishoni unashangaa ameshasema.

Tunatarajia kuwa ataeleza sababu za kutengua teuzi za Prof Kabudi na Mahiga na kuwapangia wizara mpya.

Pia tunatarajia kuwa ataeleza sababu za kutohamia Dodoma kabla ya mwaka 2018 kuisha kama alivyoahidi au kwa nini hakuhamia mapema January kama Waziri Mkuu alivyoutangazia umma.

Manunuzi na malipo ya KOROSHO yanaendeleaje?

Nani kakwambia KATENGEUA UTEZI WAO? unajua maana ya KUTENGUA? Hivi haya maneno mnaandikaga mkitumia akili za hawa wanyama wa serengeti🐃🐃🐃🐃🐃🐃

Cha msingi kuwa na subira, tuone Mh. Rais ataongea nini, acha kumuwekea maneno yako mdomoni mwake, huruhusiwi, kuwa na adabu
 
Karibu!

Viongozi wanaoapishwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Augustine Mahiga. Pia anaapishwa Balozi Hassan Simba anayekwenda kuiwakilisha nchi nchini Malawi.

Pia IGP Sirroanawaapisna na kuwavisha vyeo vya ukamishna wateule wa Jeshi la Polisi.

-----
Hotuba ya Waziri Profesa Kabudi

Mimi ni kiumbe dhaifu nisiyestahili na mwenye mawaa mengi. Namshukuru Mungu kwa hili. Namshukuru Rais Magufuli kwa kuniona nafaa katika nafasi hii.

Nimefundishwa na Dr. Augustine Mahiga na nilijifunza mengi kwake na kiingereza kwakweli alikuwa anakimanya. Nitaitumikia nafasi hii kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na uwezo wangu wote.

Tanzania ndio nchi pekee ambayo 'Universal Declaration of Human Rights' ni sehemu ya Katiba yetu. Hakuna kitu cha kuongeza kwa sababu vitu vya kutusaidia kusonga mbele vipo.

Watanzania wote walio ndani na nje ya nchi tukome mara moja na kukaa kimya maana taifa halitawavumilia. Nchi hii ni ya kidemokrasia na kwa hiyo hatutaki kufundishwa na yeyote kwani tunajitambua.

Hotuba ya Waziri Dr. Mahiga

Namshukuru Rais kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri. Kazi uliyokuwa umenipa ilikuwa inafanana na kazi na uzoefu niliokuwa nao tangu 1983 hadi 2013.

Nchi yoyote lazima itafute nafasi katika Jumuiya ya Kimataifa. Kwa bahati nzuri, nafasi yetu ndani ya Jumuiya ya Kimataifa ipo vizuri na tuna marafiki wengi. Hatuna adui duniani

Katika Jumuiya ya Kimataifa vitu havikai bila ya kubadilika, hivyo unapoingia ubia lazima uwasiliane na Jumuiya za Kimataifa. Tulikuwa na kazi ya kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuhusu siasa yetu ya ndani lakini lazima tupambane na wapotoshaji

Tumekuwa na malumbano ya wazi na Mashirika ya Kimataifa, kwa juhudi za Wizara wamenza kutuelewa. Nilipata mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, aliniambia amenipa jukwaa la kueleza uhalisia. Ufaransa pia walinialika na niliwaeleza wakaelewa

Natoa shukrani za pekee kwa kunipa nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nitakuwa nafasi ya mbele kuwa karibu na Bunge, Wananchi na Serikali. Nitaitekeleza Katiba yetu kwa vitendo

Nimeshiriki kutengeneza katiba za mataifa matano na sasa nitapata muda wa kuingalia kwa karibu Katiba yetu.

Namshukuru Rais kwa kumrudisha nyumbani kwani sasa nitakuwa karibu zaidi ya bunge na wananchi.

Hotuba ya Jaji Mkuu, Profesa Juma

Tulizoea likitajwa jina la Prof. Kabudi ilikuwa ni Wizara ya Katiba na Sheria na Dkt. Mahiga ili kuwa ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Sasa tutatakiwa kuzoea upya, tunamshukuru Prof. Kabudi kwa kufanya kazi kubwa sana

Prof. Kabudi ametusaidia sana kwenye kurahisisha kazi ya utoaji haki mfano ni umuhimu wa 'Mobile Court'. Pia matumizi ya TEHAMA ambayo ndio uelekeo mpya wa mfumo wa Mahakama, tunaamini Dkt. Mahiga utatusaidia pia katika hili

Hotuba ya Spika Jobu Ndugai

Spika Ndugai: Dkt. Mahiga kwenye vitabu vya watoro sasa unaondoka na inawezekana Prof. Kabudi akachukua nafasi, lakini tunaelewa majukumu yenu. Kuna kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, itakusaidia sana Prof. Kabudi katika kufanya kazi

Kuna katabia kameibuka kwa watu kuisema vibaya nchi yao wakiwa nje na ndio maana tumekuwa wakali sana Tukuombe Waziri umshawishi Rais kuhusu nchi zinazotaka kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, baadhi ya majirani bado hawako vizuri

Viongozi wengi wa Taifa hili wametoka katika familia duni na masikini hivyo taifa hili halina mwenye kulimiliki hivyo kila mtu afanye kazi.

Hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Nawapongeza mawaziri walioteuliwa na kusema kutokana na umahili na uzoefu wao ana uhakika watafanya vizuri.

Balozi umeapa unaweza kufanya kazi ni muhimu kusimamia mahusiano mazuri maana nchi yetu ipo katika mkakati mzuri wa kuinua uchumi kwahiyo jukumu lako kubwa ni kutuunganisha na wafanyabiashara wakubwa

Juzi nilipokuwa na wafanyabiashara wadogo na wakati maeneo waliyolalamikia ni baadhi ya watumishi wa polisi na tumewaahidi tutalifanyia kazi suala hilo hivyo mhakikishe mnatimiza yale mnayotakiwa kuyafanya

Hotuba ya Rais Magufuli

Rais Magufuli: Nawapongeza wote kwa ajili ya majukumu yenu mapya. Nina hakika mtazingatia maneno yaliyopo katika maadili

Mengi yamezungumzwa, na Mimi niungane na wengine kuwapongeza wote mlioapishwa. Nimefanya mabadiliko haya kwa sababu za kawaida, ukiwa kocha unaweza kubadilisha wachezaji wako. Wako wanaosema huyu sio Mwanasheria, kwani anakwenda kufundisha Sheria?

Wizara ya Sheria imejaa wanasheria, sasa unaweza kumpeleka Mwanadiplomasia ili akaweke mambo sawa. Naamini Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje watampa ushirikiano

Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, nako kunahitaji mtu kama Prof. Kabudi ili aende akawasukume. Ukichanganya Sheria na Diplomasia mambo yanakuwa mazuri. Prof. Kabudi ni muwazi sana

Kazi ya kuteua Makamishna wa Jeshi la Polisi haikuwa ndogo, nilimuita Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu wa Wizara. Huwezi kuwa Kamanda wa Oparesheni kisha Askari wako wanauawa. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri ukiacha kasoro ndogo

Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi

Lazima tujenge taswira ya Jeshi la Polisi kama lilivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Kama kuna maafisa wa Jeshi la Polisi wanaofanya vibaya leta taarifa ili hata nyota zao zipunguzwe na wanaoshindwa wasipelekwe Makao Makuu

Wale Askari wadogo wanaofanya kazi vizuri msiwakatishe tamaa, anamkamata Mtu mnamwambia amwachie. Msisite kuleta mapendekezo kwa wale wanaofanya vizuri. Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri kama majeshi mengine lakini hizi dosari lazima zirekebishwe.

Nawashukuru sana viongozi wa dini kwa kuliombea taifa, kuzidisha ushirikiano na kudumisha amani.
 
IMG_1443.JPG

Hafla ya kuapishwa kwa mawaziri wawili Profesa Pamagamba kabudi aliyeteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje na Afrika Mashariki pamoja na Mahiga waziri wa katiba na Sheria.Viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo Naibu na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wanasiasa na mawaziri wameshafika kushuhudia tukio hilo.
 
Karibu!

Up dates;
Viongozi mbalimbali wameshawasili wakiwemo Waziri mkuu mh Majaliwa, Spika Ndugai na Jaji mkuu Prof Juma.

Pia wakuu wa vyombo vya usalama wameshawasili akiwepo CDF Mabeho na IGP Sirro.

Kwa kweli ukumbi umesheheni wageni wa kutosha namuona pia Kamishna wa Uhamiaji, Mkuu wa Takukuru hali kadhalika Naibu Spika Dr Tulia.

Mbona hapo katika Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuna Mmoja ambaye nadhani ndiyo muhimu kwakuwa nchi yote ipo ' Kiganjani ' mwake 24/7 na hao Wawili uliowataja hapo juu humtegemea Yeye na hata Ufanisi Wao humtegemea mno Yeye na kama haitoshi hata ' Uteuzi ' Wao ulithibitishwa na Idara / Taasisi yake ambayo anaiongoza? Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Back
Top Bottom