Ikulu: Rais Magufuli apokea ujumbe kutoka kwa Kagame. Akubali kupeleka Rwanda walimu wa Kiswahili

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Rais Magufuli leo amepokea ugeni kutoka kwa Rais Kagame wa Rwanda na kuzungumza nao Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.

Pamoja na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.

C92xMyDXUAAeer2.jpg:large.jpeg
 
Rwanda kwa sasa wanatuzidi kimaendeleo.

Ni lazima tujifunze kutoka kwao. Pongezi kwa Mh. Rais.
watu wengine bhana kazi kusifia tu wengine. nchi ndogo jirani hata haijai mkono kulinganisha na nchi yetu unakuta mtu analinganisha. hivi rwanda si kama kilimanjaro tu. nimefika rwanda naweza sema mkoa huo umeendelea sana kuliko rwanda. ukitaka bisha.
 
Aibu Sana nchi ya Julius Nyerere kugeuza kanchi kadogo kama wilaya moja ya Mahenge kuwa ndio role models wetu. Hawana madini, hawana gas, hawana Serengeti, hawana Manyara, hawana Ngorongoro crater, hawana chochote leo hii ndio role models wetu. Hii yote inasababishwa na elimu mbovu ya chuo kikuu cha Dar. Imagine mtu amesoma degree zote tatu chuo kikuu cha Dar ataelewa kweli upande mwingine wa dunia. Tutaishia kuona Rwanda ndio mfano wa maendeleo wakati vijijini Rwanda wananchi wanakunya vichakani hawana vyoo kama sisi
 
Back
Top Bottom