IKULU: Rais Magufuli apokea taarifa ya ripoti ya Pili ya Mchanga. Waliosaini Mikataba Wakaangwa

Kauli ya kesema kuwa wastaafu 'watulie hakuna atakayewabugudhi' ndilo jibu la hizi kelele zote! Muda wa kuthibitisha haya ni mfupi sana na sote tutashuhudia.
 
Moja ya mapendekezo ya kamati ya Jaji Osolo ni mikataba ya madini irudishwe Bungeni ikapitiwe upya na bunge. Vile vile mikataba yote sasa ipitiwe na iridhiwe na Bunge.
Hilo siyo tatizo, ila tatizo ni aina ya wabunge na siasa za ndani ya bunge ndizo zinazonifanya nipate tabu. Wabunge tulionao sifa yao kubwa ni kujua kusoma na kuandika tu ili kuingia bungeni. Sasa watu wa aina hii wakikutana na misamiati migumu ya kimikataba wataweza kung'amua?
Lakini pia siasa za ndani ya bunge letu, ambazo kwa siku za hivi karibuni zimekuwa ni siasa za kukomoana na visasi ndani ya bunge. Je kwa pamoja yutalijenga taifa kwa kupeleka mikataba hii kwenye chombo cha namna hii?
Mawazo tu.
 
Kama bunge linalotarajiwa kujadili mambo hayo haliruhusiwi kuwa laivu,tuna nia njema?

Tunataka uwazi wa kisheria katika madini,lakini wanaojadili sheria hizo tumezuia wasiwe laivu!

Ni mwendelezo wa usiri katika mambo ya kitaifa!


Dhana ya nataka sitaki! Rais anataka uungwaji mkono, ni sahihi, basi awashirikishe wananchi kwa kuruhusu bunge live, wananchi wanalo la kuchangia katika vita hii vinginevyo asikasirike anapopingwa!
 
Kama bunge linalotarajiwa kujadili mambo hayo haliruhusiwi kuwa laivu,tuna nia njema?

Tunataka uwazi wa kisheria katika madini,lakini wanaojadili sheria hizo tumezuia wasiwe laivu!

Ni mwendelezo wa usiri katika mambo ya kitaifa!
Hata wabunge wa Ccm wenyewe wasiruhusiwe kujadili wote isipokuwa iwe wanasheria walio bobea wa vyama vyote na wawe nusu kwa nusu ili kutoa crime nzuri kwaajili ya Taifa letu.
 
Binafsi siwaelewi ccm. Mikataba ilipotakiwa na kina Zito na Mnyika bungeni walikuwa wa mwanzo kupinga. Eti leo after all the damages done ndo wanashangilia iletwe. Mungu alituumba tukiwa na vichwa na tumbo. Sasa njaa ikihamia kichwani na tukianza kufikiri kwa matumbo yetu ni hatari kwa ustawi wa taifa. Tatizo la Bunge letu ni nani aliyetoa hoja. Hoja hata iwe ya kipuuzi ikitoka ccm itaungwa mkono, hoja ikiwa ya maana ikitoka upinzani itapingwa kwa nguvu zote. Laiti wangefuata maombi ya kina Zito enzi zile pengine sasa tungekuwa watu tofauti kidogo.
 
Kama acacia wanadai wako sawa kutokana na mikataba je serekali wako sawa kutokana na mikataba angamizi?
Km mnapatana na mtu kukuvunia mazao shambani kwako mkataba unasema robo tatu ya mazao yote achukue mvunaji kosa ni la nani?
Lakini kwa akili ya kawaida ww mvunaji unaona ni busara kuchukua 3/4 ya mazao eti kisa mkataba? Ni wapi duniani iliwahi kutokea hivyo?
Cha msingi tumsuport rais kitendawili hichi kiteguliwe kwa sababu anatetea madini yetu kwa manufaa yetu.
 
"Jama ee tumuunge mkono kichaa wetu au viipi?"

Hii sentesi ilinifanya nijibaraguze kufunga gidamu za viatu vyangu ili niwasikilize hawa vijana wa kitaa (---)

Kwa kuwa sikupata nafasi na wala sitaipata ya kuyajua majina yao, isipokuwa mmoja (kidou) nawabatiza majina ili ujumbe niliousikia niwafikishie.

Walikuwa watano:-
A,
B,
C
D,
Kidou.

A: unadhani hii vita ni ya kitoto! Wazungu bila umoja lazima tukae!! (tukae = tushindwe)

B: halafu kichaa wetu ameonyesha nia njema saana, si unaona anavyowaumbua ccm wenzie? Hii hata mchonga hakuwahi kuifanya si unaona mchonga alivyokuwa anawalinda mpaka kina machela wanazeekea kwenye siasa.

Kidou: kwani malechela alikoseaga nini mpaka akabebwa?

A: achana nae huyo ana arosto!!

C: Sasa huyu kichaa wetu anataka tumuunge mkono, mbona yeye anatu dis kinoma noma?

B: anatudis vipi bwana? We bwiiga nini?

Kidou: anatudis kivipi!!

C: kwanza kabisa tumemwambia kuwa mteule wake bashite ana vinyago (vyeti) vya mchongo!!
Unaona bwana, yeye kauchuna kama hasikii vile mpaka bashite analeta soo kitaa, anawarukiarukia watu muhimu mpaka wengine wameamua kujitoa kwenye mambo ya kijamii kama mipira na mambo kibao tu. Ina maana hatuungi mkono kwenye michongo yetu au viiipi?

Halafu inshu ya Lugumi si mliifuatilia hadi bungeni masela!!!! Kiko wapi?
Kelele zooote tulizompigia yeye kanyuti!

Kuna hili swala la wafanyakazi hewa, hapa ndio kichaa wetu anapotutoa kwenye reli kabisaaaa.

Kidou: mi nnavyojua wafanyakazi hewa ni wafanyakazi ambao hawapo!! Au viiipi?
Ila kwenye matumizi inaonekana kuna fungu la hela linalipa wafanyakazi!!!

C: si unaona sasa alivyotusaliti mwishowe anakuja kutuonyesha wafanyakazi wenyewe kumbe wapo anawapa noma eti wana vinyago vya kuchonga,

A: sasa kuwa na vinyago vya kuchonga ndio kutokuwepo?

Kidou: kutokuwepo kivipi we fala!!

A: Fala mwenyewe!

HALI YA HEWA ILICHAFUKA KIDOGO.

A: ambao hawapo (hewa) hawawezi kuonekana!!! aliyekuwa anatafutwa ni yule aliyekuwa analipa watumishi ambao hawapo!!!
Hapo msela wetu katusaliti!!!
Na mapene tunayoyaokoa kwenye wafanyakazi hewa ilibidi tupatiemo mtelemko kwenye umeme!!! Eeehh! Ilipaswa bei ishuke au hata kwenye mwendo kasi inabidi ishuke iwe 300 tu lakini kichaa wetu kakomaa kichizi.

----- tunamuombea vipi wakati kila siku yuko na kina pengo, malasusa, niwemugizi, shehe mkuu, shehe wa daisalamu, mama rakatare!!
Anatuzeveza!!!
------

Kidou: mi naona ili tumuunge mkono inabidi aonyeshe uwezo wa kutusikiliza sisi wananchi taasisi na vyama vyoote!! Si vipo kiaheria bwana!!!

Halafu apeleke mswaada bungeni afute kinga ya rais kushtakiwa!!!
Kina kikwete na mkapa wameitumia vibaya kinga hiyo.
Tunaweza kujikuta tunamuunga mkono chatu mtoto, akishakua inakuwa bonge la sooo!!

A: kidou yule braza pale mnamnyaka!!?

Kidou: tujikatae usalama wengi kitaa wanalazimisha kuunga mkono mambo kichwa kichwa.
.
.
.
.
.
Nimeachwa peke yangu!!!!!!

My take!!
Kitaa kuna wasomi wengi saaana.
 
Mikataba hiyo si iliandikwa na mawakili wasomi PhDs ,

Wengine walisomea Harvard

Hii nchi imeliwa na kingizwa hasara na the so called wasomi

Msiwasingizie wasiojua kusoma

Sheria zote za kijinga zimesababishwa na the so called wasomi

Bakhresa hana elimu lakini kwenye kampuni yake hawezi kuingia mikataba ya kifedhuli
 
Basi at least Wabunge wote wawe angalau na 1st degree maana HUKU kujua (a e i o u ) (kusoma,kuandika) tu, kwa Dunia ya sasa hapana tubadili sheria ili ndioooooooo ziwe ndio zisizokua na Shaka.
 
Mimi nashauri Baraza lote la mawaziri liwajibike kwa makosa yao,Bunge na Marais wote waliohusika akiwepo Mkapa na Kijwete. Mawaziri wakuu wasiachwe hata chama cha ccm kiwajibishwe maana ilani yao mbovu ndio imetufikisha hapa. Natamani sana wakina ndioo wawajibishwe kwa hizo ndio zao. Pia asipone hata waziri mmoja alikuwepo wakati wa upitishwaji wa sheria hizo mbovu pamoja na mikataba hio mibovu hapo tutakuwa tumenyoosha nchi.
 
Sina maneno mengi ila nipende kuutambua mchango wa hoja nzito zitokazo kwa mh. Tundu Lissu, awapo nje na ndani ya bunge.

Nitatofautiana na watu wengi hasa wanaccm wenzangu ambao kwao bora ccm iishi ila Tanzania(Tanganyika) ife. Ila kwangu licha ya kuendelea kuona ccm ni chama bora ukilinganisha na vyama tulivyonavyo nchini, na kinaweza kuwa chama kibovu na cha hovyo kabisa ukikiweka kwenye mizania ya kimataifa.

Niwe wazi kwa mh. MWENYEKITI WANGU NA RAIS WANGU John Pombe Joseph Magufuri huu ni ushauri usio na chembe ya UNAFIKI ebu mchukue Mh. Lissu asaidie taifa weka usiasa pembeni Tanzania ni ya Watanzania wala siyo ya CCM au Chadema ama Cuf. Jishushe muite mh. Lissu umuombe awe kwenye jopo la wanasheria wa kupitia(reviews) za SHERIA YA MADINI NA GESI huyu mtu hakika anazijua sheria za hii nchi kuliko majaji na maprofessor wa sheria wa nchi hii.

Naomba nikushauri mh. RAIS huu mwanya wa hawa BARRICK kutaka kuwepo negotiation tuutumie kufumua mikataba hii ya madini hasa maana naona tunakomalia sheria vipi mikataba iliyofungwa kwa sheria za hovyo na kinyonyaji utambue sheria mpya haiwezi kuukumu kosa la zamani.

Mwisho ninayo mambo mawili ya kukumbusha KATIBA MPYA hasa isiyo na mlengo wa mavyama kama unavyoyaita ni mhimu kuliko kitu kingine ata hizo sheria tutakazofanyia marekebisho. Cha mwisho nakumbusha NYERERE tulikuwa naye alifanya makubwa akafariki Tanzania ikabaki na leo ni kipimo cha UADILIFU, UCHAPA KAZI NA UTU NA UTANGAMANO WA TAIFA, alifanikiwa kufanya haya maana alikuwa na falsafa UJAMAA(udugu) na KUJITEGEMEA(uchapa kazi) haya mambo yalimfanya akafanikiwa maana ndiyo yalikuwa dira na imani yake. Sasa hivi taifa(TANZANIA) halina FALSAFA (imani) ambazo zinaweza kuwaongoza watanzania. What if unamaliza miaka 5 anaingia mwingine nini kitamfanya afuate nyayo zako ata kama ni nzuri.???

Somo la UZALENDO LIANZISHWE mara moja mashuleni na kila raia atafutiwe namna ya kuonesha na kuishi uzalendo kwa nchi yake.
Ni hayo tu kwa leo.
MUNGU IBARIKA TANZANIA.
 
Back
Top Bottom