Nambarione
Member
- Sep 3, 2013
- 63
- 60
Inaelekea Prof. Mruma na timu yake walikuwa na lao jambo hata katika uandishi wa mapendekezo yao. Kwa nini hawakusema chochote kuhusu mwizi Acacia zaidi ya kusema yale makontena 277 yaendelee kubakia bandarini? Nilitegemea pendekezo la kwanza liwe Acacia kutakiwa kulipa fedha za umma alizokwepa kulipa, mgodi wake utaifishwe, nk. lakini wakajikita kuwapiga virungu baadhi ya watendaji wa serikali ,tena kwa kubagua. Ni wakati kwa Prof. Mruma na wenzake kutubu kwa mola. Angalia mwenyewe kilichofanyika, mgodi ulioanza mwaka 1998 mawaziri waliopita pale Wizarani ni wengi sana lakini wakachukuliwa watatu tu wa kuchunguzwa, wengine wakaachwa huru wakati wote walifanya kitu kilekile kuhusu usimamizi wa makinikia. Upande wa wanasheria akaguswa mtemi Chenge akaachwa Kalemani ambaye ndiye alikuwa mpishi mkuu wa sheria na mikataba yote ya madini inayopigiwa kelele leo. Upande wa makamishna wa madini wakachukuliwa watatu tu tena baadhi yao wametumika kwa muda mfupi sana kwenye nafasi hiyo, wala hawakuhusika na kusainiwa kwa mikataba ya Barrick/Acacia, wakaachwa waliokaa kwenye nafasi hiyo kwa miaka mingi (Mwakalukwa, Chambo, nk) tena ndio wahusika wakuu waliofungua migodi hiyo ya Acacia (hususan Mzee Mwakalukwa) na kuelekeza namna ya kushughulikia usafirishaji wa makinikia. Ubaguzi huu lengo lake nini hasa? kwani wao (waliotajwa kwenye taarifa hizo) hawana familia? hawana kadi za CCM? Ni kigezo gani kilichowatofautisha wao na wale walioachwa huru? Kama ni uchunguzi walitakiwa kuchunguzwa wote bila ubaguzi, maana uchunguzi ndio ungetoa jibu nani yuko safi nani hayuko safi. Binafsi nachukia sana watu wanaofanya mambo kwa hila kuumiza wenzao. Hapo Kamati ilikosea sana. Mungu anachukia kiongozi anayefanya kazi zake kwa hila, ubaguzi na kuonea watu wasio na hatia. Prof. Mruma & Co. tubuni kwa mola.