IKULU: Rais Magufuli amwapisha Dr. Wilbrod Slaa kuwa Balozi Sweden na Muhidin Mboweto kwenda Nigeria

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,478
20,390
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Februari, 2018 saa 3:00 asubuhi atawaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa watakaoapishwa ni Mhe. Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana tarehe 15 Februari, 2018.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

16 Februari, 2018.

Habari zaidi zinafuata.

======

slaa.jpg


d9a376830a8f74a670227224b0eb39b6.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
371d593cc62877ad20f4fcdd2920f460.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16,
b0ee482f69fe9889c48cfc0a9912c99f.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiashuhudia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kula kiapo kuwa mabalozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
6e5a9534d076f467be2901859e79ef9b.jpg

iku.jpg
 
Suala la umri vipi?

Ndiyo hivyo tena wazee wanapeana na kugawiana viti vya kusinzilia baada ya kunywa uji wa ulezi! Sijui ccm haina vijana wasomi kwa nafasi za ubalozi? But it's true hawana kwani wasingewaajiri kina mabashite, nyeti na gambo na kuwaazima kina mkumbo, slaa na mgwira kusaidia!

Vipi kina makinikia msando na yule aliyeitwa tumbili hawajapewa ukuu wa wilaya na ukurugenzi?
 
Back
Top Bottom