IKULU: Rais akutana na Asasi za Kiraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IKULU: Rais akutana na Asasi za Kiraia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Feb 3, 2012.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wakuu, naomba kuwasilisha...

  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Website: www.mawasilianoikulu.go.tz


  Fax: 255-22-2113425

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Asasi Zisizokuwa za Kiserikali (AZISE) wamekutana leo, Ijumaa, Februari 3, 2012, Ikulu, Dar Es Salaam, kuzungumzia mapendekezo ya Asasi hizo kuhusu jinsi ya kuboresha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Nambari 8 ya Mwaka 2011.

  Ujumbe huo wa watu 17 na ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la AZISE, Bwana Humphrey Polepole umefanya mazungumzo ya kiasi cha saa tatu na Mheshimiwa Rais Kikwete na kutoa mapendekezo yake juu ya kuboresha Sheria hiyo na mchakato nzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya.

  Mbali na Bwana Polepole, ujumbe huo ulishirikisha pia wajumbe wengine saba wa Baraza hilo, na wajumbe kutoka taasisi za Tanzania Youth Coalition (TYC), mjumbe kutoka The Leadership Forum/Jukwaa la Katiba, SHIVYAWATA, FEM ACT, mjumbe kutoka Legal and Human Rights Centre/Jukwaa la Katiba, SAHRINGON, na Youth of United Nations (YUNA).

  Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na ujumbe huo yamefanyika katika mazingira ya maelewano na miongoni mwa mambo mengine pande hizo mbili zimekubaliana kama ifuatavyo:

  1. Ujumbe wa wataalam wa ASIZE kukutana mara moja na ujumbe wa watalaam wa Serikali kuona namna gani ya kushirikisha mawazo ya Asazi hizo katika mchakato unaoendelea wa Marekebisho ya Sheria na ule mpana zaidi wa Katiba yenyewe
  2. Kwamba Katiba inayotafutwa ni Katiba ya Watanzania wote na ya nchi ya Tanzania, na wala siyo ya chama kimoja cha siasa, ama ya kabila moja ama ya kikundi kimoja cha dini. Hivyo, Katiba hiyo itafutwe kwa kujali na kutilia maanani kulinda Umoja na mustakabali wa Taifa.
  3. Kwamba kila mwananchi awe na uhuru kamili kushiriki katika Mchakato wa Kutunga Katiba Mpya lakini uhuru huo utumike kusaidia kufanikisha mchakato na wala siyo kuvuruga nchi.
  Ujumbe huo pia umempongeza Mheshimiwa Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kuanzisha mchakato wa Kutafuta Katiba Mpya kwa namna ambayo haijapata kufanyika tokea kupatikana kwa Uhuru miaka 50 iliyopita na kufanikiwa kwa Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

  Rais Kikwete mwenyewe amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kukutana naye kujadili suala muhimu kwa maslahi ya nchi na kusema kuwa utashi wake ni kuona Tanzania inapata Katiba nzuri na inayotelekezeka na kwa wakati uliokubaliwa.

  Hili ni kundi la nne kukutana na Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusiana na mchakato huo. Kabla ya hapo, Rais Kikwete amekutana na kufanya majadiliano na uongozi wa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Raia,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  03 Februari, 2012
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Wapi picha?!
   
 3. k

  kuzou JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  raisi anajipa kazi si yake ya kupokea maoni ya katiba,ni kama anafanya kazi ya ukarani,RAISI TUNAMATATIZO MENGI TU YA WEWE KUFANYA ,MADAKTARI WAMEGOMA UPO TU,YAANI DUachana na katiba teua tume wape kazi hiyo wataaalam
   
 4. S

  SOBIBOR Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 5. O

  OLEWAO Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Salva ni msanii sana usikute ni propaganda baada ya kusikia tetesi kuwa mabunge ya ccm yanajipanga kukwamisha marekebisho, mbona hakukuwa hata na taarifa kwa umma juu ya mkutano huo? Wakuu kama Salva siyo msanii atutupie picha hapa JF tujadili.
   
 6. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  rais wetu ni msikivu sana akishauriwa kuhusu mambo ya maana anaelewa
   
 7. O

  OLEWAO Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hawa jamaa kwenye picha simfahamu hata mmoja. Kama ni kweli ni wawakilishi wa asasi za kiraia basi TUNAMSHUKURU JK KWA KUTUNOLEA JAMBIA(KATIBA) ILI TUICHINJE CCM 2015! HEKO JK.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  The strength of any leader comes from serving his own people. JK needs Tanzanians now than ever before in his office tunure. He should learn to listen to them and lead with wisdom! His journey is still long and draining emotionally, physically and spiritually!
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Frankly speaking JK anapoteza muda tu hapo mapendekezo mengi wanaomba wapewe nafasi katika kamati
  Chadema wameomba hayo hayo, CUF wameomba hayo hayo, NCCR the same na sasa hawa..nothing new..
   
Loading...