nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
* Hahusiki kesi ya Mahalu
Na Mwandishi wetu (Gazeti la Uhuru)
Thursday, 28 April 2011
IKULU imekanusha habari kwamba imekuwa ikihaha kumsafisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Reyemamu, alisema jana kuwa Ikulu haiwezi kufanya hivyo, kwani Mkapa hahusiki na kesi hiyo. Alisema habari hizo ni za uongo zinazolenga kumhukumu mtu bila hatia.
Rweyemamu alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kufuatia gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ikisema: 'Mkapa kutinga kortini' na kwamba 'Ikulu yahaha kumuokoa Kikwete'.
Gazeti hilo toleo namba 239 la Aprili 27 hadi Mei 4, mwaka huu, lilichapisha habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari kisomekacho ‘Mkapa kutinga kortini'.
"Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. "Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Rweyemamu alisisitiza Rais mstaafu Mkapa hahusiki katika kesi hiyo na kwamba badala yake anayehusika ni Profesa Mahalu, hivyo kuleta mijadala au kuingiza nje ya mahakama ni kuingilia mwendelezo wa kesi, jambo ambalo si busara.
Aidha, Rweyemamu amewataka waandishi wa habari kuwa makini na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoingilia masuala ambayo yako mahakamani.
Habari hiyo, ilidai katika hati ya kiapo cha Machi 31, mwaka 2011 chini ya sheria ya usajili wa nyaraka, Mkapa alitoa utetezi kuwa kila kitu kilichofanywa na Profesa Mahalu kilikuwa sahihi.