Ikulu leo: Pinda awa kivutio kwa wasomi wa vyuo vikuu, wagombea kupiga nae picha

Kolimba Jr

Member
Nov 24, 2014
83
68
Katika hafla ya maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru Ikulu leo, wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwemo viongozi wa serikali za wanafunzi wamewapa taabu kubwa walinzi wa waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kumgombania wamsalimie na kupiga nae picha. Wanavyuo hao walimzunguka waziri mkuu na kumuweka katikati huku walinzi wake wakihaha kuweka mambo sawa. Pinda aliwasalimia wote na kuomba viandaliwe viti mahali pazuri ili wapige picha kwa awamu. Kutokana na wingi wao waziri mkuu aliwaomba wasomi hao wapige picha kwa makundi ili kuzuia vurugu iliyoonekana kujitokeza kila mtu akitaka akae mbele ya mwenzie.
Waziri mkuu alimaliza zoezi hilo huku kijasho chembamba kikimtoka.
 
Nimeiona mahala. Naamini huyu Mzee anakonga nyoyo za watu. Ni wakati sasa watu kujitahidi kulinda na kuishi ktk maadili ili kuwa kivutio na kioo cha umma.

Watu wanapenda kukaribia mtu aliye msafi ili walau kuonja na kuishi harufu ya usafi.
 
Katika hafla ya maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru Ikulu leo, wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwemo viongozi wa serikali za wanafunzi wamewapa taabu kubwa walinzi wa waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kumgombania wamsalimie na kupiga nae picha. Wanavyuo hao walimzunguka waziri mkuu na kumuweka katikati huku walinzi wake wakihaha kuweka mambo sawa. Pinda aliwasalimia wote na kuomba viandaliwe viti mahali pazuri ili wapige picha kwa awamu. Kutokana na wingi wao waziri mkuu aliwaomba wasomi hao wapige picha kwa makundi ili kuzuia vurugu iliyoonekana kujitokeza kila mtu akitaka akae mbele ya mwenzie.
Waziri mkuu alimaliza zoezi hilo huku kijasho chembamba kikimtoka.

Mwenye hili jina hakuwa mjinga kama wewe
 
Kampeni zishaanza.

Pinda kama alikuwa kajifunika funika utupu wake, escrow imemvua nguo.

Pinda astaafu tu na kila pensheni, urais ndoto kubwa sana kwake.
 
Nyota ya Pinda inazidi kung'aa, tunajifunza jambo hapa. Kuwa ukilitumikia taifa kwa uadilifu na kuwa karibu na unaowaongoza daima utasonga mbele. Siasa ni watu, hivyo kwa hili Pinda umepiga hatua kubwa kisiasa.
 
Usikute amewaandaa hao watu, maana hata lindi watu wameandamana hadi ofisi ya mkoa kupeleka ujumbe kwa JK kuwa Prof Muhongo ni msafi.
 
Hizi mbio za urais CCM kila kundi linakuja hapa jf kumpamba mgombea wao. Ngoja acer aje nayeye kuleta za Mwigulu kuwa kivutio
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha MPE pole kwa shughuli nzito ya kupiga picha mpaka anatokwa na kijasho chembamba.....
 
Rock Spider, kama umewahi kupitia angalau sekondari basi huwezi katu kupuuza ukweli kuwa marais wa vyuo na vijana wengine wa vyuo viongozi kwa ujumla wao wanawakilisha kundi la watu wachache walioaminiwa na wenzao kuwaongoza vyuoni. Huwezi kupuuza ukatuletea habari ya asilimia. Mbona hukuuliza matokeo ya TWAWEZA yalihoji asilimia ngapi? Ukiuliza swali hilo nitakuona hujui maana ya utafiti.
 
Back
Top Bottom