Ikulu kuwe nyumbani

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
458
170
Nawajulisha bungeni, na ninyi wa humu ndani
Kinyag'nyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani
Ninazunguka nchini, mijini na vijijini
Na mimi nimo kwa ndani, kinyang'anyiro nchini

Na mimi nimo njiani, Ikulu kuwe nyumbani
Nishaanza kampeni, nawajulisha juweni
Tena sifanyi utani, dhamira ipo moyoni
Kinyang'anyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani

Ikulu kuwe nyumbani, nasema nipo njiani
Napita makanisani, na pia misikitini
Kabila sina juweni, na wala huo udini
Kinyang'anyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani

Kura zenu naombeni, na debe langu pigeni
Ndugu zenu julisheni, ya kuwa mimi makini
Tukikutana njiani,mapesa nitawapeni
Kinyang'anyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani

Nimefika kituoni, ingawa siyo mwishoni
Mwenyewe nipo makini, nahonga huko bungeni
Ikulu kuwe nyumbani,tena sinao utani
Kinyang'anyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani!

Raisi Mtarajiwa
 
we ni pinda ....? wasira.........? membe.........? january............? au lowasa
 
Ikulu siyo nyumbani;

Namtafuta tabibu, mwenye kupiga ramli

Awezaye kunitibu, na kunijibu maswali

Anipe pia sababu, zenye uzito kamili

Namtafuta tabibu, anayejua ramli

Mganga au tabibu, na pia mnyenye tunguli

Nijuwe yalo nisibu, nikashindwa mara mbili

Nikaupata ububu, kuvurugikwa akili

Namtafuta tabibu, anayejua ramli

Nayatafuta majibu, nishakosa mara mbili

Nizihisia sababu, sijui kama za kweli

Nazeeka kuwa babu, mara ya tatu muhali

Namtafuta tabibu, anayejua ramli

Namtafuta tabibu, ikulu kweli ni mbali

Anipatiye majibu, kushindwa kura awali

Zilinishinda hesabu, kinyang’anyiro cha pili

Namtafuta tabibu, anayejua ramli

Tano yangu hesabu, beti zilizo kamili

Nimezitoa sababu, za kupigiwa ramli

Pia na huyo tabibu, nasema asiwe mbali

Namtafuta tabibu, anayejua ramli

Choveki.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom