Ikulu kutumika kuendeshea kikao cha Kamati ya Taifa ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu kutumika kuendeshea kikao cha Kamati ya Taifa ni sahihi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndachuwa, Jan 22, 2011.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  "...............Lakini jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio mbalimbali ya kikao hicho kilichoketi juzi Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, John Chiligati alisema suala la Dowans limeamuliwa na mahakama ya kimataifa hivyo utekelezaji uliopo ni kuilipa kampuni hiyo" Quote.

  Source: Mwananchi
  Ikulu na samani zake zote ni mali ya umma. Ikulu kutumika kuendeshea vikao vya chama kimoja ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi na haina tofauti na magari ya serikali kutumika kwenye kampeni kwani linanufaisha kundi dogo katika umma wa watanzania.

  Vyama vingine navyo vikitaka kutumia mfano kumbi za halmashauri kuendeshea vikao vyao vitaruhusiwa?.

  Kwa zama hizi za vyama vingi ni muhimu viongozi wetu wakatofautisha mali za wananchi wote za zile za vyama vyao.
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa anachanganyikiwa sasa, maana anashindwa kutofautisha vikao vya chama na vikao vya serikali. Mbona ofisi za chama zipo tu Lumumba?????????
  Hicho ndio chanzo cha matumizi mabaya ya mali za uma. Namna hii haifai!!!!!!!!
  :nono:
   
 3. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Naungana na wajumbe waliotangulia maana kwa sasa taaifa letu ni la mfumo wa vyama vingi kwa hiyo kuondoa dhuluma na lawama ambazo hazina msingi wowote serikali ijaribu kutenganisha kati ya shughuli za kichama na za serikali ili wananchi wasiwe wanalalamika kila mara
   
 4. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  haya mambo ni ya kustaabisha sana inafikia hatua chama tawala kinatumia mali za serikali kukinufaisha chama!
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  CCM wamelewa madaraka. Kwanini watumie mali za umma kwa manufaa ya watu wachache wasiofika hata milioni 5 kati ya 42 milioni???????? Rais anatakiwa kujibu kwa kutumia vibaya Ofisi.
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Je atasingizia usalama wa Lumumba kwa sasa ni mdogo?
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  NDio kwanini iwe hivyo mimi nilidhani walikuwa Lumumba ....tunataka wafuate taratibu inakuwaje aliejitangaza Rais anakuwa mvunjifu wa sheria za nchi.
   
 8. G

  GEOMO Senior Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ukisikia ulevi wa madaraka ndio huu na hili ndilo mojawapo ya matatizo ya mwenyekiti wa taifa wa chama kuwa raisi hususani hawa viongozi mchwara wasijua kutofautisha chama na serikali.
   
 9. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajua walichowafanyia wanafunzi wa UDOM so hawawezi kwenda Dodoma, wanafunzi wa UDOM watawamaliza. Wanahasira sana na Serikali yao, haswa huyo JK. Ndio maana siku hizi wanaanza kuhamishia vikao IKULU.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwani CCM waliwafanyia nini wanafunzi wa UDOM?
   
Loading...