IKULU-JF Ville-Uamuzi wangu wa Kwanza.

Sura-ya-Kwanza

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
566
10
Baada ya sherehe za kuapishwa kwa awamu ya pili na kutangaza baraza jipya la mawaziri, siku mbili baada ya hapo na mikutano kedekede niliendelea kupitia kabrasha kutoka kwa wakuu wa usalama, nimeona kuna umuhimu wa kushughulikia ndoondoo zilizoambatanishwa...kwa mda mrefu nimekuwa nazongwa na marafiki zangu hapa ofisini-niwatatulie maswala yao!

Sasa nawaona wengine wamehusishwa na mlolongo mrefu wa ufisadi! wamo kwenye kabrasha!

Kha..nimechoka mie na huko nje sasa hivi nasikia kuna mabango ya kunitaka nijiuzulu!...

Nimeamua kuitisha mkutano wa faragha, nimeomba baraza langu la mawaziri mara moja hapa kwenye magogo niliyokaa...



Niliwauliza swali moja tu 'kwanini nisiwafukuze kazi?" na kuwaamuru waende njurundoto siku mbili na waje na jibu!:D
 
Hiyo ni sura ya Kwanza, je wakirudi toka Ngurdoto utakuwa na Sura ya Pili, na jeuri ya kuwafukuza?

You have that Audacity?...Tangu lini?

Acha kuchekesha watu JK!
 
...siku mbili baadae nilipata ugeni kutoka kwa mke wa mmoja wa mawaziri walioko njurundoto, huku akiwa na soni nimlia jiwe la bati:D Alinieleza jinsi mumewe anavyoweweseka huko na kuwa alikuwa na barua ya kutoka kwa mumewe.

Bila kuhamaki nilimweleza kuwa yumo ofisini kwa Raisi na sio kwa baba tindi(tindi ni mwanangu wa tisa):rolleyes: kwa mke wa mwisho- nitakuwa ni Raisi wa kwanza kuwa madarakani bila mke hapa nchini JFVillania- Niliendelea kumwelezea kuna njia za kunifikishia barua kama hiyo kwangu, na hivyo kumtaka aondoke na barua yake hiyo.
Nimepata simu kutoka kwa Waziri wa Mitandao Na Tekelinalokujia Mh. SHY aalinieleza kuna vijana huko ughaibuni na mtandao wao wa forum inayoitwa "Tunaongea Tunachotaka" wakiongozwa na Mwanambilimbi-pilipili, wakidai kwanini niwapeleke Mawaziri wangu Njurundoto kwa siku mbili!

Nilinyanyua simu nyingine na kumpigia Waziri wa Fedha na Mpuputiko wa Uchumi Mh. Blu-Layoni....


 
...nilimwelekeza Mh Layoni atayarishe fungu kwa ajili ya kuwango'a mtandaoni hawa wajamaa...I quipped ..."whatever it takes...no trace back to this office..tafuta njia na uhakikishe Mh SHY anapata" nilikata simu na kumweleza Mh .SHY ategemee hilo fungu...
 
...kurugenzi ya usambazaji wa habari iliweza kunipatia mchoro wa ajabu tu-nasema wa ajabu kwa kuwa ametumia tarakishi kuweka maneno ukutani! ukutani?, ukuta mweupe? Asitakeukutawalahi:D

Bado nikiwa na wimbi la mshangao... mshauri wangu wa karibu(sio rafiki)aliniuliza "...kwanini?"

...kuelekeza azma yangu, nilimuuliza kwanini na yeye hakuwa na tiketi ya kuwa njurundoto?

Maswala ya kitaifa yalinikumba kama kumbakumba-ni mlolongo mrefu wananchi wanaweza kuimba-nilitaka kupata mwongozo, nilisali, na kumtaka msaidizi wa karibu amlete mama tatu(aliyewahi kuwa mke wa nane) Ikulu kwa maoengezi zaidi!
Nilienda kulala huku nikiwa na wazo moja tu!

...nitawafukuza tu...! mama tatu aliniliwaza!
 
Asubuhi ya leo nitaitisha mkutano wa Chama Chetu Cha Maendeleo

Nimepata taarifa kuwa nyara za serikali sasa zinatumiwa...
oops simu inalia!...
 
Asubuhi ya leo nitaitisha mkutano wa Chama Chetu Cha Maendeleo

Nimepata taarifa kuwa nyara za serikali sasa zinatumiwa...
oops simu inalia!...


hahaha bado unasema wakemewe viongozi wanaochocheza fujo na majungu ndani ya chama
endelea kwani unaongea na simu siku nzima??
 
hahaha bado unasema wakemewe viongozi wanaochocheza fujo na majungu ndani ya chama
endelea kwani unaongea na simu siku nzima??


Wattuuuuuuuuu piiiiiiiiiipooooooooooo mwambie Amenisahau mimi Mh. Mashallah mbona anitaji na ujela jela wangu na kuwalinda wotte mafisadi?????????
 
Baada ya sherehe za kuapishwa kwa awamu ya pili na kutangaza baraza jipya la mawaziri, siku mbili baada ya hapo na mikutano kedekede niliendelea kupitia kabrasha kutoka kwa wakuu wa usalama, nimeona kuna umuhimu wa kushughulikia ndoondoo zilizoambatanishwa...kwa mda mrefu nimekuwa nazongwa na marafiki zangu hapa ofisini-niwatatulie maswala yao!

Sasa nawaona wengine wamehusishwa na mlolongo mrefu wa ufisadi! wamo kwenye kabrasha!

Kha..nimechoka mie na huko nje sasa hivi nasikia kuna mabango ya kunitaka nijiuzulu!...

Nimeamua kuitisha mkutano wa faragha, nimeomba baraza langu la mawaziri mara moja hapa kwenye magogo niliyokaa...



Niliwauliza swali moja tu 'kwanini nisiwafukuze kazi?" na kuwaamuru waende njurundoto siku mbili na waje na jibu!:D
this font size is too small to read!
 
.....:mad:

...haikuwa taarifa nzuri!! Nimekata simu:mad:

...Baraza langu limerudi toka njuruddoto, na wote wametoa maelezo yao ya kwanini nisiwafukuze kazi-Hii ni moja ya barua niliopata......

Your Xyylensi,

Nimetumikia umma kwa muda, bado natumikia umma sasa na bado nataka niendelee kutumikia umma.

...Kama unavyonielewa Your Xyylensi, wananchi wamo kwenye umasikini, ili kufanikisha azma yangu ya kutumikia umma ningependa kuongezewa posho ya kwenda kuwaona, vile vile VX ya kikazi sasa inahitajika kubadilishwa-kwani nikienda nayo hivi wataona mie naye enda kuwasaidia sina uwezo huo kwa vile limechakaa kama daladala-hawataniamini...

...Njurundoto ilikuwa kawa! Nimetafakari matakwa yako- siwezi kujiuzulu kwa vile napenda kazi, napenda wananchi, bila wao siezi kula-naweweseka nikijiuzulu wao watakula wapi?

...Kwa mchakato huo Your Xyylensi, nimeamua kufanya biashara yangu binafsi ili nisifanye ufisadi-nasikia hili ndilo linalolalamikiwa, hivo basi naomba kutumia lile VX lazamani au ikibidi mkopo bei poa ili niweze hata kwenda kwenye shamba langu la minazi....

...Nahitimisha kwa kusema niko nawe njia nzima...kama utakubali tulindane...
mafisadi wasitushinde.

wako mtiifu,

UpoleWaMtungi.




......Kwa vile barua hii nimeisoma kiunagaubaga na kuwasilisha kwenu, kwa kweli sikufurahishwa na huyu Waziri wa Michakato na mambo yasiyokuwa ya lazima.
Nilimuamuru aondoke mara moja na kurudi Njurundoto kwani barua yake haitoshelezi-arudi baada ya siku kumi.

Mama tatu sasa ananieleza chakula tayari-niliwafukuza Mawaziri waliobaki na kuanza kukata matonge "sasa wasiniseme" ati nakula peke yangu ebo!


Tulienda kupumzika huku nimejawa na mawazo wa Mkutano wa kuharakisha wa Chama Chetu cha Maendeleo- Taarifa nilizo nazo ni kuwa kuna Chama Cha Kujaribisha umma...;)Mama Tatu aliniomba nisiweweseke sana kwani hao ni waganga keki tu ya Taifa.:eek::eek:

"Gudnaity my waif":p
...na hao wengine nao pia my waif"
Tulicheka na kulala...mhhh....;)
 
....'Unatoka kitandaniii?' aliuliza mama tatu. 'Unaonekana kama una mawazo, chai teyari!' alimaka!

Mama tatu ananijua kwa undani, utundu wangu, ukorofi wangu, na mengi tu. Ni rafiki yangu wangu wa karibu kupita Wamuya, na Lendute. wakorofi hawa ni shopping tu! haya yakiwa mawazoni nilimwangalia mama tatu akiondoka na mikogo(kama kawaida yake) mhhh "kaumbika" chura hawafai. ...Kuelekea jikoni nasikia harufu ya vitumbua na viazi vitamu!.

Tulioga na kunywa chai pamoja....mezani, mawazo yangu yalkuwa pale pale. "nitawafukuza tu"

Niliingia kwenye gari, vingora mwee mwee, Nimewaomba wana usalama kuzima na twende na trafiki(hawapendi hili) kiundani nasema "hata wanune" Leo kitaeleweka.



 
Baada ya kukutana na baraza langu, niliwaambia wote kuwa ..."uamuzi huu sikufikia kirahisi" Nilimwomba Mkurugenzi wa mawaziri atayarishe bunge la dharura.

"leo hii kazi hamna, sina konfidensi nanyi!

Nikiondoka kuelekea ofisini mwangu, mhariri wa magazeti ya mke wangu(Front Anger) Lendute, amenieleza kuwa mkwe wangu ameandika kuhusu nani anirithi, ni mwaka wangu wa nne na sing'oki, haswa baada ya kugundua kuwa chumvi ya baharini mpakani mwetu inaweza kutumiwa kupikia, hivyo hela nyingi za kigeni! Hata hivyo, mkwe wangu ana watoto wawili na mwanangu wa kike, anaitwa Maniyowu. Nilimwambia mhariri amuache tu.

Nililetewa habari kuwa Raisi wa Tumbepile anaapishwa mwezi ujao. Tumbepile ni Nchi moja kubwa tu bara la Smurmaj. Wanawekeza, ni wawekezaji ndio wanaohitaji chumvi, nilimwelekeza Waziri wangu wa wawekezaji na mambo ya ofisi zangu kutayarisha safari hii, kwani na mimi nimo humo!


Siku haikuishia hapo, kuna chakula cha nchana na mabalozi wote nchini, niliweza kutumia mda huo kuwapasha kuhusu kuwatimua Mawaziri wahujumu. na kuwaondolea wasi wasi wa serikali yangu kuyumba. Balozi wa Tumbepile Seettibye Mromqe, ambaye pia ni rafiki wangu wa siku nyingi aliniomba kuondoka mapema kwani anadai anasumbuliwa tumbo! Kha Mawazoni nasema "amebanwa tu huyu"

Luninga iliwashwa.... Breaking News....
 
Back
Top Bottom