Ikulu imetumia sh bilioni 53 toka mwaka 2003 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu imetumia sh bilioni 53 toka mwaka 2003

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jun 5, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  04 June 2011
  Claud Mshana

  SERIKALI inatazamia kutumia Sh10.257 bilioni katika bajeti yake ya 2011/2012 kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu.

  Bajeti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo, imeongezeka kwa Sh3 bilioni ikilinganishwa na makadirio mwaka jana kwa kazi hiyo. Katika bajeti ya mwaka 2010/2011 Ikulu ilitengewa Sh7.257 bilioni.

  Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka huu inayotarajiwa kusomwa bungeni wiki ijayo, fedha hizo ni kati ya Sh66.769 bilioni za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya Ofisi ya rais na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, huku matumizi ya kawaida kwa Ikulu yakipangwa Sh8.52 bilioni.

  Kiasi hicho cha ukarabati wa Ikulu kimeongezeka kutoka Sh7.257 bilioni mwaka jana, huku fedha za matumizi ya kawaida kwa mwaka unaoisha wiki ijayo zikiwa ni Sh8.8 bn.

  Katika vitabu vya makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2011/12 ambavyo Mwananchi Jumapili imefanikiwa kuviona, fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi na miradi ya maendeleo kwa baadhi ya wizara na idara zake, zimeongezeka huku wizara nyingine zikipigwa panga ikilinganishwa na mwaka wa fedha unaoisha.

  Kwa mujibu wa vitabu hivyo, Ofisi ya Makamu wa Rais imetengewa Sh40.4 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida badala ya Sh41.5 bilioni za mwaka jana, huku fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo zikiwa ni Sh12.41 bilioni badala ya Sh23.57 bilioni za mwaka unaoisha.

  Ofisi ya Waziri Mkuu, fedha zilizokadiriwa kutumika katika ujenzi wa ofisi hiyo kwa mwaka 2011/12 ni Sh4bilioni, huku fedha kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Dodoma zikiongezeka na kufikia Sh1.8 bilioni kutoka Sh1.6bilioni zilizotengwa mwaka jana.

  Kitengo cha kukabiliana na majanga kilichopo chini ya Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu, kimeongezewa fedha kutoka kwa wafadhili hadi kufikia Sh729 milioni kutoka Sh378 milioni zilizotengwa mwaka jana.

  Fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya bunge kwa mwaka ujao wa fedha ni Sh77.798 bilioni kutoka Sh52.58 mwaka jana huku fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Bunge zikifikia Sh2.04 bilioni.

  Ujenzi wa nyumba ya Spika unakadiriwa kugharimu Sh953.6 milioni ikilinganishwa na Sh1.31 bilioni zilizotengwa mwaka wa fedha 2010/2011.Miradi ya maendeleo ya Bunge ambayo imetengewa Sh3 bilioni, itakabiliwa na msukosuko baada ya wafadhili kutochangia mwaka huu. Mwaka jana wafadhili walichangia Sh500 milioni katika miradi hiyo.

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imefikiriwa kupewa Sh19.45 bilioni zikiwamo Sh96 milioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Fedha zote hizo za maendeleo zimetolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), zinaelezwa kuwa zimetengwa kutekeleza programu ya kuimarisha demokrasia.

  Fedha za miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Afya kwa mwaka ujao ni Sh364.79 bilioni, kati ya fedha hizo Sh22.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mpango wa kupunguza vifo vya watoto wachanga, huku Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi), ikipangiwa Sh800 milioni.

  Mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi yametengewa Sh90.36 bilioni, vita dhidi ya Kifua Kikuu (TB) na Ukoma Sh15.6 bilioni. Fedha zote hizo zimetoka kwa wafadhili.

  Katika makadirio ya mwaka ujao, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imetengewa Sh105.9 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeeo. Mwaka jana wizara hiyo ilitengewa Sh103.9 bilioni katika eneo hilo.

  Wizara hiyo pia imepunguziwa fedha kwa ajili ya programu ya kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo, mwaka ujao imetengewa Sh1.5 bilioni na Sh2.67 bilioni mwaka uliopita.

  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetengewa Sh135 bilioni katika miradi ya maendeleo badala ya Sh139 bilioni mwaka uliopita.Kwa mujibu wa makadirio hayo yanayotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo, Chuo Kikuu cha Dodoma kimetengewa Sh200 milioni.
  source:mwananchi
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  wakumbuke pia kuhifandhi mazingira kando ya ikulu ufukweni mwa bahari kuna mmomonyoko mkubwa sana wa ardhi katika barabara ya ocean.............. ila ingependeza zaidi kama wangetumia fedha hizo kuimarisha mpango wa serikali kuhamia dodoma...................
   
 3. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  he kumbe ikulu kila mwaka inakarabatiwa?? so in two years we can spend 17 billion, duh
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  sidhani kwamba watalkumbuka kwani kila mwaka bajeti ya ikulu ipo sea inaliwa na ha o hao wenyewe
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  wewe hujiulizi why riz1 anaendeha benz then anasema anaishi kiujanja ujanja? ndio ujanja wenyewe huu ati
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  SERIKALI inatazamia kutumia Sh10.257 bilioni katika bajeti yake ya 2011/2012 kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu.
  Bajeti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo, imeongezeka kwa Sh3 bilioni ikilinganishwa na makadirio mwaka jana kwa kazi hiyo. Katika bajeti ya mwaka 2010/2011 Ikulu ilitengewa Sh7.257 bilioni.

  Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka huu inayotarajiwa kusomwa bungeni wiki ijayo, fedha hizo ni kati ya Sh66.769 bilioni za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa ajili ya Ofisi ya rais na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, huku matumizi ya kawaida kwa Ikulu yakipangwa Sh8.52 bilioni.

  Kiasi hicho cha ukarabati wa Ikulu kimeongezeka kutoka Sh7.257 bilioni mwaka jana, huku fedha za matumizi ya kawaida kwa mwaka unaoisha wiki ijayo zikiwa ni Sh8.8 bn.

  Katika vitabu vya makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2011/12 ambavyo Mwananchi Jumapili imefanikiwa kuviona, fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi na miradi ya maendeleo kwa baadhi ya wizara na idara zake, zimeongezeka huku wizara nyingine zikipigwa panga ikilinganishwa na mwaka wa fedha unaoisha.

  Kwa mujibu wa vitabu hivyo, Ofisi ya Makamu wa Rais imetengewa Sh40.4 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida badala ya Sh41.5 bilioni za mwaka jana, huku fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo zikiwa ni Sh12.41 bilioni badala ya Sh23.57 bilioni za mwaka unaoisha.
  Ofisi ya Waziri Mkuu, fedha zilizokadiriwa kutumika katika ujenzi wa ofisi hiyo kwa mwaka 2011/12 ni Sh4bilioni, huku fedha kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Dodoma zikiongezeka na kufikia Sh1.8 bilioni kutoka Sh1.6bilioni zilizotengwa mwaka jana.
  Kitengo cha kukabiliana na majanga kilichopo chini ya Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu, kimeongezewa fedha kutoka kwa wafadhili hadi kufikia Sh729 milioni kutoka Sh378 milioni zilizotengwa mwaka jana.

  Fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya bunge kwa mwaka ujao wa fedha ni Sh77.798 bilioni kutoka Sh52.58 mwaka jana huku fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Bunge zikifikia Sh2.04 bilioni.

  Ujenzi wa nyumba ya Spika unakadiriwa kugharimu Sh953.6 milioni ikilinganishwa na Sh1.31 bilioni zilizotengwa mwaka wa fedha 2010/2011.Miradi ya maendeleo ya Bunge ambayo imetengewa Sh3 bilioni, itakabiliwa na msukosuko baada ya wafadhili kutochangia mwaka huu. Mwaka jana wafadhili walichangia Sh500 milioni katika miradi hiyo.

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imefikiriwa kupewa Sh19.45 bilioni zikiwamo Sh96 milioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Fedha zote hizo za maendeleo zimetolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), zinaelezwa kuwa zimetengwa kutekeleza programu ya kuimarisha demokrasia.

  Fedha za miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Afya kwa mwaka ujao ni Sh364.79 bilioni, kati ya fedha hizo Sh22.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mpango wa kupunguza vifo vya watoto wachanga, huku Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi), ikipangiwa Sh800 milioni.

  Mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi yametengewa Sh90.36 bilioni, vita dhidi ya Kifua Kikuu (TB) na Ukoma Sh15.6 bilioni. Fedha zote hizo zimetoka kwa wafadhili.

  Katika makadirio ya mwaka ujao, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imetengewa Sh105.9 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeeo. Mwaka jana wizara hiyo ilitengewa Sh103.9 bilioni katika eneo hilo.Wizara hiyo pia imepunguziwa fedha kwa ajili ya programu ya kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo, mwaka ujao imetengewa Sh1.5 bilioni na Sh2.67 bilioni mwaka uliopita.

  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetengewa Sh135 bilioni katika miradi ya maendeleo badala ya Sh139 bilioni mwaka uliopita.Kwa mujibu wa makadirio hayo yanayotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo, Chuo Kikuu cha Dodoma kimetengewa Sh200 milioni. Programu
   
 7. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kupika rangi na c langi
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  naomba maana ya neno langi
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Jf nisaidieni kwa hili. Kwani ghalama za kujenga ikulu mpya ni kama sh ngapi?
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna mtu anaweza kupata details White House wanatumia kiasi gani kwa mwaka kwa ajili ya ukarabati?
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  title yako na maelezo vyatofautiana sana.
  hata kama una nia ya kupotosha huko ulikofikia ni ngazi ya uendawazimu.
  tangu lini ukarabati unahusu kupaka rangi tu?
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Someni habari muilewe acheni kuwa petty and bitches. Hatupo shule ya imla.
   
 13. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 524
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Nawewe kupika rangi ndio nini au wanatengeneza mikeka..
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  comparison eeh?

  [​IMG]
   
 15. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 524
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  bil. 26
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  HTML:
   
  Kupanga langi ukulu sh 10.257 milioni 
  Kupika rangi na c langi 
  
  mwaongea lugha gani wananchi
   
 17. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Du inauma sana hivi haya majengo ya wakubwa kila siku yanakarabatiwa tuu. Mbona kila mwaka kukarabati ikulu, ofisi ya waziri mkuu, etc. Mwaka jana ikulu ilikarabatiwa, nyumba ya spika ikajengwa, na blabla zingine. Huu si uwizi wakati wengine hata maji ya kuoga achilia mbali kula hatupati. EE MUNGU tusaidie waja wako tunateseka duniani hapa wakati wengine wanakula vizuri na kulala vizuri.
   
 18. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wakuu, kwani kuna Tsunami imepiga Magogoni?
  Hizo 10bn ni kwa ajili ya ukarabati gani? kupaka rangi au Kununua furniture?
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  kupaka rangi,kutaka majani, kuzoa majani,kusafisha mavi ya ndege ndege wale na wadudu,kusafisha ma swiming pool etc.mimi naona hii bajeti haitoshi
   
 20. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmh!!
   
Loading...