#COVID19 Ikulu, imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,155
2,000
Tatizo la siku hizi kila mtu aki google something anajiona amekuwa mtalaamu wa hicho alicho google na kuwaona wale watalaam halisi ya hicho kitu amewazidi na anaanza kuwasahihisha. Yaani mtu aliyegoogle kitu kwa dakika tano anajiona anakijua hiko kitu kuliko hao waliokisomea chuoni kitu hicho kwa miaka isiopungua mitano ya chuo kikuu. Hata wakieleweshwa hawataki kukubali kwani wanaamini walichokiona kwa mr google.

Hilo la uvaaji glovu nimesha kutoa elimu yake ya kisayansi. Ninairudia tena hapa kama ulikuwa hujaisoma huko juu:

Sababu kubwa ya watoa huduma ya afya kuvaa gloves ni kujikinga kuambukizwa virusi vya hiv na vya hepatitis ikitokea wakashika au kugusa damu ya mtu ambaye ana virusi hivyo. Kabla ya ujio wa virusi vya ukimwi mwaka 1984 walikuwa hawavyai gloves isipokuwa wakati wa operesheni huko theatre ambako walivaa surgical sterile gloves kwa ajili ya kutompandikizia bacteria au fungus mgonjwa wanayemfanyia upasuaji (surgical site infection prevention), kitu ambacho ni hatari sana kwa maisha ya mgonjwa anayefanyiwa surgery. Surgical gloves hizo ziliwakinga wanaofanya operesheni pia wasiambukizwe na virusi vya hepatitis virus kutoka kwenye damu ya mgonjwa wanayempasua. Hata kwenye kuzalisha huko labour ward (delivery rooms) walikuwa hawavyai gloves. Manesi na madaktari walikuwa wanawazalisha mama wajawazito bila kuvaa gloves. Walivyaa surgical gloves tu pale ilipobidi kuongeza njia ya uzazi (vagina) kwa kuichana kwa mkasi (episiotomy) na baadaye kuishona.

Gloves zilizokuwapo ni surgical sterile gloves kwa ajili ya operesheni na non sterilr examination gloves kwa ajili ya examination kwenye maeneo maalum ya mgonjwa mgonjwa kama (i)per rectal examination ambapo daktari anaingiza kidole chake kimoja (index finger) ndani ya mkundu wa mgonjwa na (ii) per vaginal examination ambapo daktari au muuguzi anaingiza vidole viwili kwa pamoja ndani ya uke wa mgonjwa. Gloves hizo zinamkinga daktari au muuguzi vidole vyake kushika mavi au uchafu ulioko ukeni. Lakini kwenye hali ya emergency na gloves kutokuwepo bado daktari au muuguzi atashika huo uchafu mikononi mwake kuokoa maisha ya mgonjwa, atanawa mikono yake kwa maji na sabuni kufanya disinfection.aka sanitization ya mikono yake.

Examination zingine za mgonjwa au utoaji wa huduma kama kuchoma sindano na kufunga kidonda hakukuhitaji kuvaa gloves ila mtoa huduma hunawa mikono kwa sabuni au antiseptics (hizi antiseptic ndiyo leo mnaziita sanitaizer) kabla na baada ya kumuhudumia/ kumgusa mgonjwa ili kuzuia kusambaza (transmission) ya vidudu hatarishi kama vya bacteria, virus na fungus (pathogenic microorganism) -- nasocomial infections aka hospital infections. Mbinu nyingine anayotumia mtoa huduma bila kuvaa glovu inaitwa non-touch technique - ambayo mtoa huduma anahakikisha hagusi damu au uchafu mwingine kutoka kwa mteja/ mgonjwa wake. Kwa mfano akishakudunga hiyo sindano ya chanjo, anaweka kipamba (swab) kwenye hiyo sehemu na mgonjwa mwenyewe ndiye anaigandamiza hiyo pamba kwa kidole chake mwenyewe hadi damu itakapoacha kutoka. Hivyo mtoa chanjo hagusi damu ya huyo mteja wake bali mteja ndiye anashika damu yake na baada ya hapo anapewa sehemu ya kuitupa.

Huu uvaaji holela wa gloves zisizo sterile na wala si examination gloves kwa kila mtu ni kwa sababu la kujikinga na janga la ukimwi ingawa pia vinasaidia kukinga kupata virusi vya viral hepatitis.
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,236
2,000
Na wewe iga Mkuu , maana hata hiyo statement "Unaiga kuandika yanayozunguka mitandaoni!" na yenyewe umeiga hakuna kitu kipya ambacho kizazi cha leo kitazungumza ambacho hakijawai kuandikwa.

Gwajima aka Mkono wa Baunsa ni TAPELI ,Chanjo zilizokuwa approved na WHO ndio zinatumika kwahiyo kuna option JJ ,Pfizer ,Astazenica etc kwahiyo kama Majaliwa kachanjwa JJ na mimi pfizer ni kweli tofauti.
chanjo ya ESTA ndo naitaka inapatikana wapi
 

katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,070
2,000
Au sisi wengine ni washamba jamani?
View attachment 1871735

View attachment 1871734

---
View attachment 1871367
Rais wa USA, Joe Biden akichomwa chanjo

===

Wizara ya Afya watoa ufafanuzi kuhusu hoja hii, soma hapa chini:
-
LABDA watu wa idara ya afya watatupa ufafanuzi.
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
2,087
2,000
Au sisi wengine ni washamba jamani?
View attachment 1871735

View attachment 1871734

---
View attachment 1871367
Rais wa USA, Joe Biden akichomwa chanjo

===

Wizara ya Afya watoa ufafanuzi kuhusu hoja hii, soma hapa chini:
-
Masuala ya Personal Protective Equipments na Infection Prevention ni muhimu sana kwa watoa huduma za afya pamoja na wateja wanowahudumia.Kama Wizara husika ndiyo inayotengeneza miongozo na kujikanganya hivi Wananchi wafanyeje?
Kuvaa gloves ingekiwa lazima kwa sababu kuna uwezekano ikamsaidia mtoa huduma maana nimeona wanatumika swab wakati wa kuchoma na baada ya sindano,wanakuwa katika<than one meter distance.
Pia baadhi ya wateja wanakuwa katika hofu ya sindano&chanjo yenyewe na hawajatulia kiasi inaweza kutokea ajali.
Why kukanusha bila kufafanua kwa kina?Kama ni ukosefu/upungufu wa gloves tuambiwe.Mtoa sindano katika kumgusa Mteja A na B na C;Bado mnataka kusema ni salama kwa COVID-19 transmission!
 

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
481
1,000
Na wewe iga Mkuu , maana hata hiyo statement "Unaiga kuandika yanayozunguka mitandaoni!" na yenyewe umeiga hakuna kitu kipya ambacho kizazi cha leo kitazungumza ambacho hakijawai kuandikwa.

Gwajima aka Mkono wa Baunsa ni TAPELI ,Chanjo zilizokuwa approved na WHO ndio zinatumika kwahiyo kuna option JJ ,Pfizer ,Astazenica etc kwahiyo kama Majaliwa kachanjwa JJ na mimi pfizer ni kweli tofauti.
Jitahidi kuangalia spelling za unachoandika. JF inaruhusu editing ya text.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,975
2,000
VYETI FEKI WALIO SALIA NDIYO MAANA WANAMCHUKIA MAGUFULI
Elimu ya hapa na pale wako Ikulu
Kikwete katorokea wapi? Alistahili apate chanjo ili kama mambo yakiwa mazuri, tuanze upya kutafuta wanasiasa wanaofaa.
 

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,265
2,000
Mimi ni muhudumu wa Afya, nafanya kazi RCH. Ni kawaida tu na ninatoa sana chanjo bila globes wala si ajabu, kwaiyo ni swala la kawaida usijari
Pale medical attendant anavyojichoresha incompetency yale mbele ya ma-great thinkers, kama unaandika globes badala ya gloves ...sishangai kutozingatia IPC SOP na kujitapa kabisa, ila yawezekana hata haujui IPC SOP.
 

DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,265
2,000
Au sisi wengine ni washamba jamani?
View attachment 1871735

View attachment 1871734

---
View attachment 1871367
Rais wa USA, Joe Biden akichomwa chanjo

===

Wizara ya Afya watoa ufafanuzi kuhusu hoja hii, soma hapa chini:
-
Halafu anachoma sindano bila kuvuta bomba, ye anapeleka tu.
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,650
2,000
View attachment 1872655
DA HUSTLA

ujumbe ndio huo nafikiri sasa utajipima mjinga ni nani kati ya wewe na mimi,


jibu liko wazi mjing ni wewe vaccine ni kawaida sana kutolewa bila PPE over
Wewe ulisema ni kawaida, ila hii taarifa haiongelei ukawaida au mazoea. Kama ulimaanisha ulicholeta, siku nyingine uandike vizuri kwa kuzingatia maana halisi ya maneno.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,115
2,000
Mimi ni muhudumu wa Afya, nafanya kazi RCH. Ni kawaida tu na ninatoa sana chanjo bila globes wala si ajabu, kwaiyo ni swala la kawaida usijari
Wewe muhudumu wa afya utakuwa mjinga, hujui madhara yake! Umeishia darasa la 7 eeeh? Huwa wanatumia "Globes?"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom