Ikulu imegeuzwa "chaka la ujambazi wa kiserikali" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu imegeuzwa "chaka la ujambazi wa kiserikali"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bakari Maligwa, Jan 5, 2011.

 1. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kusema kwamba, "IKULU NI MAHALA PATAKATIFU". Wapo watu walimuona Mwalimu Nyerere kama amekosea kusema vile...nadhani ilikuwapo haja ya kujiuliza: KWA NINI IKULU IWE TAKATIFU? Utakatifu wa Ikulu unatokana na ukweli kwamba ndiyo inayotoa muelekeo wa uongozi na menejimenti ya shughuli zote za kuongoza nchi.

  Kwa jinsi hiyo, lazima IKULU iwe takatifu kwa kuwatumikia wananchi na si kuwatumia majambazi wa kisiasa. Hapa natakata kuandika kwamba, IKULU ya Magogoni imevamiwa na "wanefili" wanaotafuna nchi bila woga huku wakiwatukana wAnanchi kwa kejeli kubwa. Nataka nimzungumzie Salva Rweyemamu!

  Salva Rweyemamu mwanzoni nilijiuliza kwa nini yupo IKULU ya Magogoni! Sikushangaa kwa vile Salva Rweyemamu ana sifa hizi:
  1. Ndiye aliyetumiwa na wamiliki wa Richmond kuzuia ueneaji wa habari "chafu" dhidi ya kampuni hilo la kitapeli;
  2. Ndiye anayejua akina nani wanamiliki Richmond kwa vile alishawahi kuajiriwa na wamiliki wake;
  3. Ndiye aliyepewa dhamana ya kuingia IKULU ili amsaidie JK kulinda mafisadi; na
  4. Ndiye muongo wa karne anayemdanganya JK kwa habari za uzushi na potofu.
  Na lipo suala moja nyeti na la muhimu sana kuliuliza: HIVI NI NANI ALIYEPENDEKEZA AAJIRIWE IKULU? Jibu ni rahisi sana: ROSTAM ABDUL'RASUL AZIZ! Kwa jinsi hii, IKULU imegeuzwa "chaka la ujambazi wa kiserikali" kwA vile majambazi wa kiserikali ndipo wanapokutana katika kupanga mikakati na mbinu za kuihujumu nchi kama hali inavyoendelea kutisha na kudhoofisha hali za wananchi wa Tanzania.

  IKULU ya Magogoni imekuwa ikitumiwa na watu binafsi matajiri wenye uchu, uroho na ubarakala wenye nia ya kuwaneemesha mataJIri wa CCM na wale wa nje ili kwa jinsi ya kutumia taasisi mbalimbali ndani ya IKULU kufanikisha ujambazi wa kuimaliza nchi na kuwatia "nira" wananchi.

  Watendaji wa IKULU akiwemo Salva Rweyemamu wamekuwa wakitumika sana na majambazi wa kiserikali katika kufanikisha mipango ya wizi na uzuvendi wa kisiasa na uporaji wa mali ya umma kwa kutumia habari "nyepesi" za kijasusi ilhali ukweli wa habari ni kwamba: KIKWETE ANAWAJUA MAFISADI (NA WA WAMILIKI) WA RICHMOND! IKULU INAJUA NJAMA ZOTE ZA UFISADI NA INAENDELEZA UFISADI WA KIMFUMO KW NJIA ZA KIJAMBAZI...
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  habari ndefu kweli kweli,ntarudi jioni kusoma
   
Loading...