Ikulu ilizuia Vigogo 3 Kufikishwa Mahakamani

Ibrah,

Hii habari yako inaonekana wazi kuwa sio ya kweli maana
  1. Haitaji jina la mhusika yeyote ingawa imeshaelezwa kuwa walionekana mahakamani.
  2. Either umeitunga kutokana na yale tunayoyafahamu juu ya mafisadi au umedanganywa maana kila kilichoandikwa ni cha kufikirika, including majina.
  3. Inaelekea aliyeitunga hii habari nia yake ilikuwa ni hilo hitimisho la kuwa CCM wana njama za kutumia ufisadi kuwafaa wao wenyewe kama ulivyoandika otherwise utueleze zaidi conclussion ilivyofikiwa;

Kama wahusika walikuwa wameshafikishwa mahakamani kama ulivyosema, ina maana hakuna aliyewaona huko mahakamani mpaka ikawa siri hadi leo? Ina maana hata huyo aliyekupa hizo 'nyeti' na yeye pia kayafanya hayo majina yao kuwa ni siri? Nanukuu ulivyoripoti hapa chini;

Ingawa tungependa hawa mabwana wafikishwe mbele ya kaisari, lakini nafikiri hilo halijafanyika kama ilivyosimuliwa, ila hii ni nyepesi ilitungwa kwa sababu anazojua mtungaji na haifai kuendelea kukaa katika jukwaa la siasa.

Mod hii ipelekwe kwenye nyepesi.

Hizo habari chanzo chake siwezi kukitaja hapa ingawa ungependa nitaje lakini iko siku habari hii itatoka live kwenye vyombo vingine vya habari. Si unajua Mafisadi ndo madai yao hayo (Remember Mwanahalisi kuambiwa watoe chanzo cha habari ili wapate sababu ya kuwasulubu watu? Hata madai ya EPA Spika si alitishia kumpeleka Polisi Dk. Slaa ili awakilishe huo ushahidi kwenye ofisi yake? LAkini mwisho wa siku ilikuwaje, si ilibainika kuwa ni kweli hata bila Dk Slaa kupeleka ushahidi Bungeni na badala yake akaendeleza libeneke Mwembeyanga Tandika?
 
Sidhani kuwa kuna anayetaka chanzo chako cha habari ila sidhani kama kutaja majina ya waliofikishwa mahakamani (hao mawaziri), kuwa nayo ni siri. Hii habari yako ina mapungufu mengi sana, ni nafuu ukaulizie tena huko ulikoipata kama hukutunga au uachane nayo maana inakuharibia sifa yako kuwa mzushi.

PCCB au polisi hawawezi kumchukulia hatua waziri au PS yeyote, wa sasa au wa zamani, bila kuwasiliana na bosi wao, JK, kwanza hata kama yuko Iceland.
 
Mkuu Ibrah, binafsi nimekusoma sana. Hivi hii habari si mpya na iliandikwa katika magazeti ikiwamo RaiaMwema na nimeweka link katika post yangu hapo juu page ya kwanza. na watu waliichangia hapa JF... Binafsi nina uhakika mkubwa na hiyo habari hadi wahusika na kila tukio. Kuhusu kwenda mahakamani, si kesi zote watu wanaonekana na kwa hili si kwamba waliotinga mahakamani ni watuhumiwa bali wanasheria wa DPP office na PCCB na baada ya mawasiliano ndipo Luhanjo akaingilia. Habari ndio hiyo, kwa kuwasaidia someni post za mwanzo
 
Ibrah,
Sidhani kuwa kuna anayetaka chanzo chako cha habari ila sidhani kama kutaja majina ya waliofikishwa mahakamani (hao mawaziri), kuwa nayo ni siri. Hii habari yako ina mapungufu mengi sana, ni nafuu ukaulizie tena huko ulikoipata kama hukutunga au uachane nayo maana inakuharibia sifa yako kuwa mzushi.

PCCB au polisi hawawezi kumchukulia hatua waziri au PS yeyote, wa sasa au wa zamani, bila kuwasiliana na bosi wao, JK, kwanza hata kama yuko Iceland.

Dpp Kuridhia Mashtaka Dhidi Ya Vigogo Kesi Za Pccb?

Raia Mwema - Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mramba na Yona kushitakiwa!! | Jambo Blog Network
 
Mbona hii habari siyo ngeni jamani... tumejua kwa miezi sasa kuhusu ugumu wa Ikulu kuridhia hawa jamaa kushitakiwa. Majina yalishawekwa hata hapa hakuna cha siri tena. Halisi amewawekea link sidhani kama watu wanajaribu kuangalia... hakuna jipya, hatuhitaji maneno tena, tunachohitaji kuona ni jamaa wamesimama kizimbani! Hayo mengine ni irrelevant.
 
Yaani mwizi anaomba asikamatwe hadi muda wake wa kustaafu utakapofika?

Wote wezi!!! Hivi we hujapita Kariakoo au pale Jangwani, kibaka akikuibia simu anakimbizwa na vibaka wenzake na wewe ukiwafuata wanakwenda kukumalizia walivyobakisha. Luhanjo ana yake kwa hiyo sikushangaa kusikia hayo. Nimesema nitaanza baadaye ya Luhanjo kwa wakati wake mwafaka.
 
Ibrah,
Sidhani kuwa kuna anayetaka chanzo chako cha habari ila sidhani kama kutaja majina ya waliofikishwa mahakamani (hao mawaziri), kuwa nayo ni siri. Hii habari yako ina mapungufu mengi sana, ni nafuu ukaulizie tena huko ulikoipata kama hukutunga au uachane nayo maana inakuharibia sifa yako kuwa mzushi.

PCCB au polisi hawawezi kumchukulia hatua waziri au PS yeyote, wa sasa au wa zamani, bila kuwasiliana na bosi wao, JK, kwanza hata kama yuko Iceland.

Mheshimiwa Kubwajinga,

Ile interview ya Mbowe vipi? utafanya lini?
 
Mbona hii habari siyo ngeni jamani... tumejua kwa miezi sasa kuhusu ugumu wa Ikulu kuridhia hawa jamaa kushitakiwa.

Mkuu,

Unakumbuka uliwahi kukataa kwamba Rais hayuko juu ya hawa ma DPP, na Wanasheria Wakuu, na law enforcers wengine ? Sasa Ikulu kuridhia na kutoridhia mashitaka wamepata wapi nguvu hizo ?
 
Mkuu nakupa tano: Vigogo hao ni: Mawaziri wa zamani, Daniel Yona kwa kesi ya Kiwira, Basil Mramba kwa kesi ya exemption ya Corporate Tax katika kampuni ya Alex Stewarts na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ia-mashtaka-dhidi-ya-vigogo-kesi-za-pccb.html

Raia Mwema - Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mramba na Yona kushitakiwa!! | Jambo Blog Network

Kwa ujumla ni kwamba kisingizio cha KAtibu Mkuu Kiongozi, P.Luhanjo ni kwamba, siku waliyokuwa wakitaka kupelekwa mahakamani Mgonja alikuwa akutane na wafadhili ambao wangepoteza imani na serikali kwa hiyo akaomba waahirishe kesi hadi muda wake wa kustaafu utakapofika. Inasemekana atastaafu kati ya mwezi huu na Novembe 08.

Kimsingi Luhanjo naye ni fisadi mkubwa, data zake tutaziweka wakati mwafaka.

Ibrah,

Asomaye na afahamu!

Hii habari yako inaonekana wazi kuwa sio ya kweli maana
  1. Haitaji jina la mhusika yeyote ingawa imeshaelezwa kuwa walionekana mahakamani.
  2. Either umeitunga kutokana na yale tunayoyafahamu juu ya mafisadi au umedanganywa maana kila kilichoandikwa ni cha kufikirika, including majina.
  3. Inaelekea aliyeitunga hii habari nia yake ilikuwa ni hilo hitimisho la kuwa CCM wana njama za kutumia ufisadi kuwafaa wao wenyewe kama ulivyoandika otherwise utueleze zaidi conclussion ilivyofikiwa;

Aliyenipasha alinipa na majina black and white! Kuna ghorofa liliota kama uyoga pale Arusha, gazeti moja likamtaja Muhusika mmojawapo wa ufisadi kuwa ndiye mmliki na baada ya habari hiyo ghorofa likasimama hadi leo!

Kama wahusika walikuwa wameshafikishwa mahakamani kama ulivyosema, ina maana hakuna aliyewaona huko mahakamani mpaka ikawa siri hadi leo? Ina maana hata huyo aliyekupa hizo 'nyeti' na yeye pia kayafanya hayo majina yao kuwa ni siri? Nanukuu ulivyoripoti hapa chini;

Siyo siri Mkuu, 2010 WaTz wakiamka kama walivyofanya wale wa Tarime kwenye uchaguzi mdogo hayo yote yatawekwa nuruni na sijui utauficha wapi uso wako. Salama yao ni CCM kuendelea kutawala kwa miaka 10 baadaye na hilo wanalijua na ndo maana matajiri mafisadi wako tayari kuichangia CCM mabilioni ili iendelee kutawala na wapate kuishi, vinginavyo CCM ikon'goka na giza la ufisadi na hao Mafisadi wataumbuka. Si unajua mashangingi karibu 80 yaliyeyuka Tairm usiku kwa usiku baada ya kujua WanaTarime wamewagomea? Unajua aliyekuwa anawalisha Polisi kule Tarime? Unafikiri ni kwa sababu gani alichukua jukumu la seriakali (kuwalisha Polisi)?

Akili mukichwa Mkuu!
 
Ni kweli kabisa, lazima kuna mpango wa kutoa baadhi ya mafisadi kafara kwa ajili ya uchaguzi wa 2010

Patamu patakuwa pale ambapo mabangusilo watatolewa na bado watabwagwa kwa kishindo!

Kwani bilioni moja Tarime si wameiramba bado wakafanya kweli? kinachotakiwa hapa ni watu waelewe, pesa wakileta wailambe afterall ni hela yetu wenyewe waliyo tufisadi, baada ya hapo kwenye sanduku la kura wanafanya kweli, ikifuatiwa na ulinzi madhubuti ili kura zisiibiwe!
 
Nimepata habari kutoka vyanzo vya kuaminika kuwa DPP alikuwa awafikishe Watuhumiwa wakubwa wa Ufisadi; wawili walikuwa Mawaziri waandamizi wa Awamu ya II na Katibu Mkuu 1 ambaye amekuwa Wizara moja nyeti kwa muda mrefu hadi sasa.

Habari zinapasha kuwa walishatinga kwenye Jengo la Mahakama lakini haijulikani ni namna gani habari zilimfikia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Katibu Mkuu Kiongozi alipothibitishiwa kuwa ni kweli Watuhumiwa hao wako aliwang'akia PCCB "Mnataka Nchii hii istawalike?" naye akawasiliana na Mkuu wa nchi aliyekuwa ughaibuni ambaye aliagiza kuwa wasisomewe mashitaka!
Habari zinapasha kuwa ushahidi dhidi ya Watuhumiwa hao uko wazi kabisa ingawa habari zinasema kuwa hata Rais aliyepita wa awamu ya II angejikuta yuko implicated kwenye tuhuma hizo za Ufisadi.

Habari nyingine zinapasha kuwa Serikali mwakani 2009 itaustua umma wa WaTz kwa kumfikisha Mahakamani Kigogo mmoja naMwanamtandao mkubwa ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na uchaguzi wa 2010 ili kuzima jaribio la kumfanya JK aenguliwe katika kinyang'anyiro cha Urais katika CCM.

Hii habari inaonyesha wazi vita ya ndani kwa ndani...Ukiangalia kwenye red highlight utaona ni mzee Rukhsa wanamwambia anyamaze kwani na yeye wanaweza kumweka kwenye chain yao ya ufisadi..Na msisitizo wakaweka kwenye kauli mbiu yao kuwa nchi HAITATAWALIKA kama wakishughulikiwa....Na kurudia kuwa awamu ya pili this and that..Ya tatu wala haina noma na ya nne.

Watazunguruka sana lakini nadhani hawazisomi alama za nyakati..Kwamba hata ndani ya miaka kumi ijayo udhalimu waliokwisha ufanya ambao wananchi sasa wanaufahamu hauwezi kupita hivi hivi tu bila uwajibikaji.

Wakidhani porojo zitamaliza haya mambo..Then wanaishi kwenye dunia yao ya kufikirika.
 
Siyo siri Mkuu, 2010 WaTz wakiamka kama walivyofanya wale wa Tarime kwenye uchaguzi mdogo hayo yote yatawekwa nuruni na sijui utauficha wapi uso wako.

Ibra,
Hii nyepesi yako ni nzuri lakini inahitaji mtu asiyefikiria sana au mshabiki tu ndio aamini. Kama huwezi hata kuandika majina ya mawaziri au angalau kuelezea huo mkakati wa 2010 umeamuliwa na nani kulingana na hiyo source yako, uliyoandika yanabakia kuwa ni porojo tu.

Kuna muungwana mmoja hapa alituambia kuwa Tarime CCM walikuwa na mpango wa kuiba ng'ombe, kuleta mtafaruku n.k., ili washinde kura. (Isome hapo chini) Hatukuyaona yote hayo. Sasa hii nyepesi yako ambayo iko hovyo zaidi unataka kwa nini tuiamini kama hata huwezi kuipa siha kidogo?? Tuachane na uzushi ili tuangalie mambo mazito yanayoikabili nchi.

1. Kuna mabasi mawili ya Zakaria yanatokea jijini mwanza yakiwa yamewabeba wafanyakazi wa kiwanda cha Coca cola ambacho ni cha Gachuma na huku wakisindikizwa na escort ya magari mawili ya polisi moja nyuma na jingine mbele yanaelekea Tarime , kufanya nini , stay tuned.
2.Jana usiku ziliandaliwa hujuma eneo la mgodi kule Nyamongo na wamekamatwa vijana zaidi ya 120 , kwa kile kilichoitwa kuwa mgodi ulivamiwa .......
3.Usiku wa leo maeneo ya vijijini zimeandaliwa hujuma kuwa mifugo itaibiwa na haswa Ngombe ili kesho wanatarime badala ya kwenda kupiga kura basi wawe wanafuatilia mifugo yao na kata hizo zitakazohusika ni zile ambazo CHADEMA wananguvu kubwa na hilo ni kuhakikisha kuwa wapiga kura wanapungua.
4.Hujuma nyingine ambayo imeandaliwa kufanyika maeneo ya mijini ni kuwa CCM wamehimizana kwenda kupiga kura asubuhi na ikifika saa tano basi polisi watazua mtafaruku na kuanza kutumia nguvu kuhakikisha kuwa hakuna watu kwenda kupiga kura na hivyo kuipa CCM ushindi.
 
Jamii Forum isiwe ni siri. Sasa Vigogo watatu maana yake nini. Inatakiwa isemwe wazi kuwa Mafisadi watatu Mgonja, Yona na Mramba.

Hii serilkali ni ya mambo madogo madogo tu ambayo ni none issues. yale maissues yenyewe haina usemi wowote..
 
Unaelewa nyani hucheka mkia wa mwenzake. Hata uzushi wa taarifa ni sehemu ya ufusadi.kila la kheri kwa uzushi.wengine twapenda habari za ukweli na zenye uhakika ndipo tuweze kuchangia mawazo yetu
 
Kubwajinga,
Lisemwalo li.. kama halipo, la..
Kila jambo uanza kama tetesi na kukutwa limekuwa jambo.
Moto uonekana kwa kuona moshi kwanza.
Tusubiri tuone!
 
Nadhani tumwambie JK, kuwa kesi zote atakazofungua kuanzia mwakani hatutazitambua -Hizo itakuwa ni mbinu za kifisadi za kushinda uchaguzi! Kama kweli atakuwa anamaanisha basi azifungue na ziishe ndani ya mwaka huohuo ili tuone kama kutakuwa convictions! Safari hii wataishiwa tricks! Miti yote itateleza!

Mkuu you are very right.they must stop playing us.
 
Back
Top Bottom