Ikulu ilizuia Vigogo 3 Kufikishwa Mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu ilizuia Vigogo 3 Kufikishwa Mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Oct 22, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimepata habari kutoka vyanzo vya kuaminika kuwa DPP alikuwa awafikishe Watuhumiwa wakubwa wa Ufisadi; wawili walikuwa Mawaziri waandamizi wa Awamu ya II na Katibu Mkuu 1 ambaye amekuwa Wizara moja nyeti kwa muda mrefu hadi sasa.

  Habari zinapasha kuwa walishatinga kwenye Jengo la Mahakama lakini haijulikani ni namna gani habari zilimfikia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Katibu Mkuu Kiongozi alipothibitishiwa kuwa ni kweli Watuhumiwa hao wako aliwang'akia PCCB "Mnataka Nchii hii istawalike?" naye akawasiliana na Mkuu wa nchi aliyekuwa ughaibuni ambaye aliagiza kuwa wasisomewe mashitaka!
  Habari zinapasha kuwa ushahidi dhidi ya Watuhumiwa hao uko wazi kabisa ingawa habari zinasema kuwa hata Rais aliyepita wa awamu ya II angejikuta yuko implicated kwenye tuhuma hizo za Ufisadi.

  Habari nyingine zinapasha kuwa Serikali mwakani 2009 itaustua umma wa WaTz kwa kumfikisha Mahakamani Kigogo mmoja naMwanamtandao mkubwa ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na uchaguzi wa 2010 ili kuzima jaribio la kumfanya JK aenguliwe katika kinyang'anyiro cha Urais katika CCM.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Duh Makubwa..
  Hii ishu yawezekana kweli.Sasa kwa nini wanasua sua mbona nchi imesha haribika.
  Nani hajui kuwa viongozi wetu wengi ni mafisadi?Wangelipuliwa tu ili wajisafishe.
  Huyu Luhanjo naye amekalia kuti kavu mwacheni tu siku zake zinahesabika tutamsahau kama ndugu yake Mangula yupo kijijini sasa analima viazi tu.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  "mabangusilo" wanaandaliwa kwa ajili ya sympathy vote 2010.
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Makubwa hayo. Madogo yana nafuu. Yangu macho na masikio. Mengi yamesemwa hatujaona matokeo. Labda hili la 2009 la kushtua umma kama litafanyiwa kazi itakuwa ni exceptional!!!!!
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Si mabangusilo Steve D ni kweli kuwa ni Mafisadi ila kinachofanyika ni kutaka kuwatumia Mafisadi hao kupata kibali cha kuendelea kuwadanganya watanzania ili waendelee kutuongoza tena 2010, na pia ni njia ya kuhakikisha kuwa wanawazima kwa kuwa ni wapinzania wao wa ndani kwa ndani na walishirikiana nao kwenye ufisadi wote isipokuwa kuwa sasa hawana nguvu ya kimadaraka tu.
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  taja majina... this is the forum where we dare to talk openly remember!!!
   
 7. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nadhani tumwambie JK, kuwa kesi zote atakazofungua kuanzia mwakani hatutazitambua -Hizo itakuwa ni mbinu za kifisadi za kushinda uchaguzi! Kama kweli atakuwa anamaanisha basi azifungue na ziishe ndani ya mwaka huohuo ili tuone kama kutakuwa convictions! Safari hii wataishiwa tricks! Miti yote itateleza!
   
 8. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  NImekupata

  Hapo inamaana kuwa huo mtikisiko utakuwa hivi:
  LOWASSA au CHENGE atapelekwa mahakamani 2009, HALAFU UMA WA WATZ UTADANGANYIKA MWAKA 2010 watamchagua tena Joti aka Muuza sura JK halafu baada ya uchaguzi mshtakiwa atashinda kesi maana serikali ndio inamiliki mahakama, umaendesha nchi kimabavu + mwanasheria mkono na wengine toka NJE watamtetea mashtakiwa+ hakima atapewa mabilioni kama rushwa na serikali na mshtakiwa binafsi

  TZ ZAIDI UIJUAVYO
   
 9. Wakunyuti

  Wakunyuti JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmoja wapo si Mkapa..!!!
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Mkuu nakupa tano: Vigogo hao ni: Mawaziri wa zamani, Daniel Yona kwa kesi ya Kiwira, Basil Mramba kwa kesi ya exemption ya Corporate Tax katika kampuni ya Alex Stewarts na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/15738-dpp-kuridhia-mashtaka-dhidi-ya-vigogo-kesi-za-pccb.html

  Raia Mwema - Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

  Mramba na Yona kushitakiwa!! | Jambo Blog Network

  Kwa ujumla ni kwamba kisingizio cha KAtibu Mkuu Kiongozi, P.Luhanjo ni kwamba, siku waliyokuwa wakitaka kupelekwa mahakamani Mgonja alikuwa akutane na wafadhili ambao wangepoteza imani na serikali kwa hiyo akaomba waahirishe kesi hadi muda wake wa kustaafu utakapofika. Inasemekana atastaafu kati ya mwezi huu na Novembe 08.

  Kimsingi Luhanjo naye ni fisadi mkubwa, data zake tutaziweka wakati mwafaka.
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama kawaida, kigugumizi
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ...........No doubt............... Daniel Yona na Gray Mgonja ndani
   
 13. R

  Raia Member

  #13
  Oct 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh, haya anayobashiri Tuandamane tyaweza kutokea kweli siku moja. Na si mbali sana.
   
 14. R

  Raia Member

  #14
  Oct 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki kigugumizi hawakujua kama ipo siku wadanganyika tutachoka kudanganyika?
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hizi nyepesi nyepesi za mafisadi wakitaka kutuhadaa ili tuamini kuna progress. Nadhani kwa kuwa wameamua kuwadharau watanzania kwa kuamua kuulinda ufisadi kwa gharama yeyote basi wanaweka mazingira magumu ya nchi kutawalika hapo mbeleni. I mean tutawanyima kura zetu hata wakiamua kuziiba wataiba mapaka wataona aibu wenyewe...
  Hakimu ni Fisi na mtuhumiwa ni Fisi je swala ahatapa haki yake??
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,197
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo matatizo ya kuwa na kiongozi wa nchi aliyeingia madarakani kwa kuwatumia mafisadi na kutoa rushwa kwa wapiga kura wa chama chake ili wampitishe kama mgombea wa chama chao. Hao mafisadi waliokuwa wafikishwe mahakamani wanajua fika aliyoyafanya Kikwete ili aingie Ikulu na kamwe hawatakuwa tayari kuadhirika pekee yao. Kuna uwezekano mkubwa wakaamua kuongea yaliyofanywa na mkuu pale Dodoma na hatimaye kuibuka kidedea na hili litamfanya mkuu aombe kuachia ngazi. Hivyo alivyosema kwamba nchi inaweza kushindwa kutawalika ni kweli kabisa. Lakini je tutalinda maslahi ya viongozi uchwara na mafisadi mpaka lini? Nchi sasa hivi inateketea kama kiongozi ni fisadi basi ni lazima aanikwe ili aachie ngazi na tupate kiongozi atakayeweka maslahi ya Watanzania mbele badala ya kwake binafsi.
   
 17. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ibrah,  Hii habari yako inaonekana wazi kuwa sio ya kweli maana
  1. Haitaji jina la mhusika yeyote ingawa imeshaelezwa kuwa walionekana mahakamani.
  2. Either umeitunga kutokana na yale tunayoyafahamu juu ya mafisadi au umedanganywa maana kila kilichoandikwa ni cha kufikirika, including majina.
  3. Inaelekea aliyeitunga hii habari nia yake ilikuwa ni hilo hitimisho la kuwa CCM wana njama za kutumia ufisadi kuwafaa wao wenyewe kama ulivyoandika otherwise utueleze zaidi conclussion ilivyofikiwa;
  Kama wahusika walikuwa wameshafikishwa mahakamani kama ulivyosema, ina maana hakuna aliyewaona huko mahakamani mpaka ikawa siri hadi leo? Ina maana hata huyo aliyekupa hizo 'nyeti' na yeye pia kayafanya hayo majina yao kuwa ni siri? Nanukuu ulivyoripoti hapa chini;
  Ingawa tungependa hawa mabwana wafikishwe mbele ya kaisari, lakini nafikiri hilo halijafanyika kama ilivyosimuliwa, ila hii ni nyepesi ilitungwa kwa sababu anazojua mtungaji na haifai kuendelea kukaa katika jukwaa la siasa.

  Mod hii ipelekwe kwenye nyepesi.
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Sitataja, lakini ni Mawaziri 2 wa awamu ya II na walishatajwaga sana huko nyuma, na katibu mkuu mmoja wa wizara nyeti (ileile ) tangu awamu ya ii hadi leo.
   
 19. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  vipi mkuu!!! Umeshikiwa bunduki wakati unaandika hii taarifa maana una mis lead kwa makusudi, awamu ya pili mgonja alikuwa bot na si katibu mkuu pengine uniambie rutabanziba hapo nitakuelewa ila tayari jf ime doubt credibility ya story hii mkuu.

  Tusubiri kuona pccb wakifanya kweli na si taarifa ya kughushi kama hii.
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ni habari nzuri kwa masikio, lakini katibu mkuu wa wizara kuandaliwa mashitaka hadi hatua ya kufika mahakamani bila Luhanjo (Mkuu wa utumishi serikalini) kujua basi kutakuwa na tatizo kubwa sana kiutendaji kuliko tunavyojua!
   
Loading...