Ikulu ilivunja Tume ya Katiba kimya kimya bila wajumbe kujua

Kwani tume ya Warioba haikupewa hadidu rajeo. Nauliza hivi nikijua kuwa mh huyu ana historia ya kutofuata hadidu rajeo. Mulize rais Mkapa anaushahidi wa hili.
 
Kwani tume ya Warioba haikupewa hadidu rajeo. Nauliza hivi nikijua kuwa mh huyu ana historia ya kutofuata hadidu rajeo. Mulize rais Mkapa anaushahidi wa hili.

Hadidu za rejea ina maana zilitolewa na ofisi ya rais. Nadhani sasa unaweza kuiona jinsi ilivyo. Hapo kuna hadidu hapo? Alipewa lakini matumaini yao yalikuwa tofauti. Tena siyo ajabu kwamba wao walidhani Warioba atatuelewa kwamba tunataka serikali mbili na lazima mawaziri tuendelee kuwa wabunge.

Tunaongozwa na misheni tauni!


Lkn mkuu haya mambo yanafanyika wtz wanaona nihuuni bei gani.tume imetumia mkuu anza kuchukua hatua wengine watafuata

Kuna wakati fact lazima lisemwe. Kwa ujumla TZ tulijisahau, tukadhani kila anayeingia ikulu ni nyerere. Sasa hata chawa wameingia. Tatizo wanajifahamu kwamba hawakuwa na stahili hiyo na ili kujilinda wanatumia nguvu nyingi sana. Kutoboa macho ya watu, kutoweka na meno ya watu, nk. Na hiyo ni ile ile staili ya Idd Amin. Kumbe hakuwa mbali na wengi. Utajitoa muhanga ktk serikali ya Idd Amin?
 
kutupiwa virago mheshimiwa ndugu yetu, kipenzi chetu ndugu jaji Warioba, Naombeni kujua nini umuhimu wa tume yake ?
jeee bunge la katiba tunajua lengo lake?
jee ccm wanaposema msimamo wao ni serikali mbili jee hayo ndio matakwa ya wananchi au matakwa ya ccm.
 
kutupiwa virago mheshimiwa ndugu yetu, kipenzi chetu ndugu jaji Warioba, Naombeni kujua nini umuhimu wa tume yake ?
jeee bunge la katiba tunajua lengo lake?
jee ccm wanaposema msimamo wao ni serikali mbili jee hayo ndio matakwa ya wananchi au matakwa ya ccm.
Kila siku na jambo jipya
 
RAIS Jakaya Kikwete ameivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika hatua ambayo imewashutukiza wajumbe wa Tume hiyo, imefahamika.

Taarifa ya kuvunjwa kwa Tume hiyo, maarufu sasa kama Tume ya Warioba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, ilisambazwa jana Jumatano na Ikulu ikieleza kwamba Rais aliivunja Jumatano iliyopita, Machi 19, siku moja tu baada Warioba kuwasilisha kwenye Bunge la Maalumu la Katiba, Rasimu ya Katiba, katika hotuba iliyoeleza kwa uwazi, pamoja na mambo mengine, matatizo ya Muungano yatokanayo na muundo wake.

Katika taarifa yenye kichwa cha habari: Tangazo la Serikali kuhusu kuvunjwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema:

"Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalumu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na. 81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014".

Jumanne wiki hii, Jaji Warioba aliliambia Raia Mwema kwamba hawakuwa wamepata taarifa rasmi za kuvunjwa kwa Tume hiyo mapema, na ilibidi wafuatilie wenyewe Ikulu baada ya kuona katika mitandao na baadhi ya waandishi wa habari kuwapigia simu.

Alisema Jaji Warioba: "Mpaka sasa (saa 7:30 mchana-Jumanne) tulikuwa hatujui. Tumeuliza baada ya kusikia. Wametuletea taarifa nadhani ni kama mliyonayo ninyi na barua ya Ikulu kutueleza hilo.

"Tuna wajibu sasa kukabidhi. Maana hapa tuna mali nyingi ya Taifa. Kuna ofisi, lakini pia kuna wafanyakazi na magari. Wajumbe wote wana magari, na wale ambao hapa si majumbani kwao, walikuwa wamepangishwa. Naona kama muda wa kufanya yote hayo ni mfupi mno."

Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo, Profesa Mwesiga Baregu aliliambia Raia Mwema: "Mimi ndiyo kwanza unaniambia wewe kwamba Tume imevunjwa. Ndiyo, nilijua itavunjwa kwa mujibu wa sheria, lakini uamuzi umefanyika lini sikuwa na taarifa."

Taarifa zaidi kuhusiana na Tume hiyo zilieleza kwamba wajumbe wengi hawakuwa wameridhishwa na kilichoonekana kuwa ni majibu ya Rais Kikwete kwa maoni yaliyowasilishwa na Jaji Warioba katika kuwasilisha Rasimu ya Katiba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, maoni ya baadhi ya wanaTume yalikuwa ni kwamba watafute wasaa wa kuweza kujibu baadhi ya hoja alizoibua Rais Kikwete ili zieleweke vyema.

"Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haimpi Rais nafasi ya kufanya kile alichofanya. Kwamba amekwenda kuhutubia Bunge baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya uwasilishaji. Kitendo hicho hakikidhi matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba hata kidogo. Kwa hiyo, wamefanya uchakachuaji tu ili kuvuruga matakwa ya kisheria na shughuli za Bunge," alisema Baregu katika mahojiano na Raia Mwema na kuongeza:

"Alichofanya Rais Kikwete ni kama amefanya kuvamia Bunge...ni uvamizi hivi na taratibu zilipangwa kinyemela ili azungumze baada ya Warioba. Huu mchakato wa Katiba umekuwa na matatizo tangu kwenye mabaraza ya wilaya, kulikuwa na njama za kuuvuruga," alisema Baregu na kuonya kwamba yanaweza yakatokea ya nchi jirani ya Kenya ambapo rasimu ya Katiba ilichakachuliwa na ilipopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni ilikatatiliwa.

Mjumbe mwingine wa Tume akizungamza kwa sharti la kutokutajwa gazetini alisema: "Baada ya hotuba ile ya Rais, yalizuka mawazo katika kikao cha kuhitimisha. Ilizungumzwa kwamba palihitajika ufafanuzi katika maeneo fulani fulani.

"Maana sasa imekuwa kwamba viongozi wengi wanawasema sana wajumbe wa Tume, lakini wao hawawezi kujibu. Wajumbe wa Tume wameambiwa wasijibu, wasiseme. Hatujui kwa nini wao wasemwe halafu waambiwe wasiseme.Halafu hata ukiangalia siku ya kuvunjwa kwa Tume ni siku ambayo wajumbe walikuwa safarini kutoka Dodoma baada ya Mwenyekiti kuwasilisha, mambo haya hayajakaa sawa."

Upepo mbaya kuhusu Tume ya Warioba ulianza bungeni Dodoma wakati alipotaka kuwasilisha kwa mara ya kwanza Rasimu ya Katiba Machi 17, mwaka huu.

Katika tukio hilo, Jaji Warioba alijikuta akisimama kwa dakika tatu mbele ya kipaza sauti, lakini akashindwa kuwasilisha Rasimu ya Katiba kutokana na vurugu zilizojitokeza bungeni.

Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kumwalika kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa ndani ya muda wa dakika 120.

Hata hivyo, kabla ya Jaji Warioba kuanza kusoma hotuba yake ya kuwasilisha Rasimu hiyo, baadhi ya wajumbe walisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti.

Profesa Ibrahimu Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu walikuwa miongoni mwa wajumbe waliosimama kuomba mwongozo kabla ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu yake bungeni.

Mwenyekiti Sitta aliwakatilia wajumbe hao kuomba mwongozo kwa kuwambia: "Hakuna mwongozo hapa, naomba Mwenyekiti uendelee…waheshimiwa wabunge, hakuna mwongozo naomba Mwenyekiti uendelee kwa ajili ya hansard."

Kauli hiyo ya Sitta ilizidi kuchafua hali ya hewa bungeni humo na hivyo Jaji Warioba kulazimika kusitisha uwasilishaji wa Rasimu, tukio ambalo hata hivyo alilitekeleza kesho yake asubuhi baada Bunge kuahilishwa ya siku hiyo.


Chanzo: Raia Mwema
Mbowe, lissu, lipumba kumbe hawajaanza Leo vurugu? Wakasababisha rasimu ya warioba isipite
 
Back
Top Bottom