Ikulu hawajui Kiswahili fasaha?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,647
Jana wkati taarifa ya uteuzi ya wabunge watatu iliyotoka Ikulu,
kuna kitu kimenishangaza.
Hivi lugha iliyotumika hapo chini ni sahihi? au Ikulu hawajui kiswahili?

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010

Hapo kwenye red ndipo ningeomba kuelimishwa.
Hapo mwandishi anakusudia kutueleza kuwa yeye ni raisi msaidizi au ni mwandishi wa raisi msaidizi (means yupo rais msaidizi) kama alikusudia kutueleza yeye ni mwandishi msaidizi wa raisi alipaswa kuandika hivyo alivyoandika??
 
Kiswahili fasaha ni janga la taifa. Kuanzia ikulu, ofisi za serikali hadi vyama vya upinzani.

Ilani ya uchaguzi ya Chadema ilikuwa na makosa ya Kiswahili yaliyokithiri.

Sikuisoma ya Cuf lakini naamini hali ilikuwa vivyo. Ya Ccm ndo hayo tunayaona
 
Sasa unategemea nini kwa wtoto wanaokua sasa, hapohapo watu wataka kiswahili hikihiki kitumike hadi chuoni kufundishia, safari bado ni ndefu, kaaaaazi kwelikweli.
 
ni balaa kabisa maana naona hapo huyo jamaa (Premi Kibanga) yeye ni kama raisi Msaidizi, hii inanikumbusha hizi sentesi

1) Mke wa kwanza wa Raisi
2) Mke wa Raisi wa Kwanza
 
Jana wkati taarifa ya uteuzi ya wabunge watatu iliyotoka Ikulu,
kuna kitu kimenishangaza.
Hivi lugha iliyotumika hapo chini ni sahihi? au Ikulu hawajui kiswahili?

MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010

Hapo kwenye red ndipo ningeomba kuelimishwa.
Hapo mwandishi anakusudia kutueleza kuwa yeye ni raisi msaidizi au ni mwandishi wa raisi msaidizi (means yupo rais msaidizi) kama alikusudia kutueleza yeye ni mwandishi msaidizi wa raisi alipaswa kuandika hivyo alivyoandika??

Inachekesha. Lakini nafikiri si tatizo la kutojua kiswahili. Ila ni tatizo la Kiswahili chenyewe. Ni kigumu lakini tunafikiri ni rahisi mpaka tunafanya tafsiri wenyewe kutoka kwenye maneno ya kiingereza. BAKITA nao ndio wamezubaa tu. Kimsingi, hicho cheo cha "Mwandishi wa Rais Msaidizi" ni tafsiri kutoka kwenye Scheme of service ambako kuna (sina uhakika) State House Press Secretary, Assistant Press Secretary, n.k. Sasa wakitengeneza scheme of service ya kiswahili, wanaweka maneno wanayofikiri yanasikika vizuri. Ndio tunaishia na kuwa na Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi. Hiyo ipo kwenye idara nyingi za serikali.
 
Kiswahili fasaha ni janga la taifa. Kuanzia ikulu, ofisi za serikali hadi vyama vya upinzani.

Ilani ya uchaguzi ya Chadema ilikuwa na makosa ya Kiswahili yaliyokithiri.

Sikuisoma ya Cuf lakini naamini hali ilikuwa vivyo. Ya Ccm ndo hayo tunayaona

Gaijin hayo sio makosa ya CCM ni makosa ya Serikali........au kuna kitu sikifahamu unataka kuniambia?
 
Gaijin hayo sio makosa ya CCM ni makosa ya Serikali........au kuna kitu sikifahamu unataka kuniambia?

Ccm ndo ilotuwekea wazembe serikalini bila ya kujali uwajibikaji. Uzembe wa aina hii kwa nchi za wenzetu hamna kwa sababu Chama kinachoongoza serikali hakiwezi kuruhu watu wafanye makosa ya kizembe aina hii.

Tena Ikulu!
 
Ndio yale yale ya rais kupewa chek ambayo tarakimu ni 2,000,000 lakini maneno ni milioni tatu na rais akakenyua tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom