Ikulu, Dodoma: Rais Magufuli amewaapisha Viongozi Wateule mbalimbali, amewasisitiza kuridhika na nafasi walizoteuliwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533



Viongozi Wateule walioapishwa Leo ni:
1.
Bw. Aboubakar Kunenge- Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

2. Bw. Joseph Joseph Mkirikiti - Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

3. Bw.Paulo Mshimo Makanza - Kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam

4. Bw. Gabriel Pascal Malata- Kuwa Wakili Mkuu wa Serikali

5. Dkt. Boniface Luhende-Kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali

6. Dkt. Maduhu Isaac Kazi - Kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

Pia Mhe. Rais atashuhudia Uapisho wa Wakuu wa Wilaya za Kongwa, Chunya, Kiteto, Moshi na Hanang

Eneo: Viwanja vya Ikulu Chamwino.
===

UPDATES
-
Rais Magufuli ameshafika katika viwanja hivi kwa ajili ya kuapisha

- Zoezi la kuwaapisha Viongozi mbalimbali walioteuliwa linaendelea.

- Zoezi la kuapa kwa Kiongozi mmoja mmoja limekamilika. kwa sasa Viongozi Wateuliwa watatoa ahadi ya Uadilifu ya Viongozi wa Umma ambapo viongozi hao wanaapa kwa makundi.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la uapishaji kwa sasa Viongozi wachache wamepewa nafasi ya kutoa salaam. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Chalamila amepewa nafasi ya kutoa salam kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ambapo amemshukuru Rais Magufuli kutokana na fedha mbalimbali zilizotolewa ili kutekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa wa Mbeya na kuahidi kuendelelea kutimiza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa katika jiji hilo.

Katika kueleza hili Mh. Albert Chalamira anasema "Katika jiji la Mbeya wachache wamesema hakuna maendeleo yanachotekelezwa lakini hivi karibuni tumepokea zaidi ya bilioni 3.6 kwa ajili ya miundombinu ya Elimu. Hili ni moja ya mambo yaliyonifanya nibaki jiji la Mbeya bila kwenda kugombea"

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kutoa salamu kwa sasa amekaribishwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi General Salvatory Mabeyo ambaye anatoa salamu kwa niaba ya Vyombo vya Ulinzi na usalama. General Mabeyo ambapo ameshukuru kwa kupewa nafasi hiyo pamoja na kuwapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuwasisitiza kwenda kutimiza majukumu yao.

General Mabeyo amesema "Kwa niaba ya wenzangu nawapongeza walioapishwa kwenda kushika madaraka yao. Lengo kubwa ni kwenda kuwatumikia wananchi lakini kubwa ni kujitafakari na kujitambua kuwa tunapotumikia nafasi zetu tujue dhamana hiyo ni kwa ajili ya maendelo ya Taifa na Wananchi"

Waziri wa Tamisemi Mh. Seleman Jafo amekaribishwa kwa ajili ya kutoa salamu. Aidha, Mh. Jafo amewapongeza Viongozi wote walioteuliwa pamoja na kuwasisitiza wote kwenda kutimiza majukumu yao.

Katika hili Mh. Seleman Jafo amesema "Viongozi mlioapishwa tukamsaidie Rais, tusiende kutafuta umaarufu bali umaarufu uwafuate ninyi. Wanaotafuta umaarufu mara nyingi mwisho wao sio mzuri sana. Nendeni mkahakikishe zile fedha ambazo Rais amezielekeza huko mnazisimamia"

Sambamba na hilo, Jafo amesema Tangu Rais ameingia, ‘trend’ ya udhibiti wa fedha za mamlaka za Serikali za Mitaa umeongezeka kwa umakini mkubwa. Nendeni mkatimize majukumu yenu. Huwa haipendezi unatoka hapa unafika ‘site’ jukumu alilotakiwa kufanya Mkuu wa Wilaya hajafanya. Tembeleeni miradi"

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amewapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuapishwa katika nafasi mbalimbali. Pia, Mh. Samia amewasisitiza viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao.

Zaidi ya hayo, Mama Samia Suluhu amewaonya viongozi na kuwasisitiza viongozi kuridhika na madaraka wanayopewa. katika hili Makamu wa Rais amesema Imempendeza Rais kuwapa madaraka akiamini mtakwenda kuwatumikia watu. Mwanadamu unapoishi unatakiwa kutosheka. Utawala wetu sasa hivi sio utawala wa kuhaha na madaraka. Kuwatumikia watu sio kuwaongoza, nendeni someni na angalia wapi pa kurekebisha

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote walioapishwa siku ya leo pamoja na kuwasisitiza kwenda kuwatumikia Wananchi wote kwa bidii. Zaidi ya hayo Rais Magufuli amewasisitiza Viongozi walioteuliwa kuridhika wanapopewa madaraka mbalimbali.

Rais Magufuli amesema "Mtambue kwamba hizi nafasi mmezipata kwasababu Mwenyezi Mungu alitaka. Mkawatumikie Wananchi hasa Wananchi masikini. Dkt. Luhende umekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar. Kanali Songea tumekupeleka Kiteto migogoro ipo mingi, tumekupeleka ukaishughulikie.

Katika hili Rais Magufuli amesema kuwa "Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Mmefanikiwa kuipata fursa, hivyo makafanye kazi". Aidha, katika hili Rais Magufuli ametoa mifano ya viongozi mbalimbali walioteuliwa na namna walivyovumilia katika majukumu mbalimbali.

Rais Magufuli amesema "Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982. Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais kuwa waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829" .

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa hajamtuma kiongozi yoyote kwenda kugombea nafasi yoyote. Hivyo, viongozi waliochukua fomu ndani ya chama hicho wapimwe inavyostahili.

Katika jambo hili Rais Magufuli amesema "Nataka kuwathibitishia wananchi na wanaCCM hakuna mtu yeyote aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu Dkt. Bashiru. Kama wapo watu kule wanaozungumza huko wametumwa na Rais ni waongo. Wapimeni wagombea itakavyowafaa" Siwezi kutuma mtu nyuma ya mgongo".

"Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma wala nisingehakaika, ningesubiri kwenye viti vyangu 10 nikakuteua. Mtu asijekusema ametumwa na IGP au na CDF, wangetaka wangekuteua kuwa hata Kanali. Nendeni mkatumwe na wananchi huko, kila mahali kuna tatizo lake"

zaidi ya hayo rais Magufuli amesisitiza viongozi hao kwenda kuwatumikia wananchi. Mathalani, akimuongelea Mkurugenzi wa TIC Rais Magufuli amesema amemtaka kiongozi huyo kuhakikisha anatafuta Wawekezaji wengi.

Katika jambo hili Rais Magufuli amesema "Kumekuwa na tabia ya kuwazungusha wawekezaji. Mwekezaji amekuja na pesa lakini wewe mara njoo huku mara njoo kesho. Msiwazungushe wawekezaji maana wakiwekeza tutatengeneza ajira. Kuna mwekezaji anataka kujenga kiwanda cha vifaa vya umeme ila nasikia amezungushwa"

Zaidi ya haya Rais Magufuli amewasisitiza kuwa "Kila mmoja katika eneo lake akafanye ambavyo anaona inafaa sio kwamba tumekuwa tukifanya hivi. Tuongeze ‘speed’ na tunataka twende ‘speed’ kubwa zaidi ‘We used’ inakuwa ‘past tense’ kwenye kiingereza, ‘We do this’ hicho ndicho ninachotaka kila mtu akashughulikie"

Mwisho, Rais amewashukuru na kuwatakia mafanikio mema Viongozi wote walioteuliwa pamoja na kupiga nao picha za kumbukumbu.
 
Rais John Magufuli leo anatarajia kushuhudia uapisho wa Viongozi wapya wateule, utakaofanyika katika eneo la viwanja vya Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

 
Hivi ni kwa nini wakuu wa Wilaya wanaapishiwa Ikulu wakati hawaapishwi na Rais .....!!?
 
“Niwaombe sana msiende kutafuta umaarufu, kafanyeni kazi umaarufu uwatafute ninyi, wanaotafuta umaarufu mara nyingi mwisho wao sio mzuri sana…umaarufu utakutafuta badala ya wewe kuutafuta ” Mhe. Selemani Jaffo - Waziri OR-TAMISEMI

ITV Tanzania

Mpaka leo hii Waziri Jaffo 'Mzee wa Kupiga Nyungu' maneno haya yamekutoka inaonyesha ulikuwa humpendi na umefurahi ' Kang'olewa ' Jijini.
 
Siwezi Kumtuma Mtu Kwa Mgongo Wa Pembeni
Nendeni Mkawapime Wote Sawa Sawa
Kama Ningekuwa Nimewatuma Ningewateua Kwenye Viti Vyangu 10

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Hii kaisema leo?
 
ila sijui kwa upande wangu naona dogo Makonda kama kachemka vile bora angebaki au kanusa harufu ya kutolewa siku zijazo akaona abadili gia angani? angevumilia hapo kwa kuwa ubunge wa kigamboni ni kazi
 
Back
Top Bottom